Mkuu kwa masilahi ya wengi, unafikiri leo EL akipata Urais huo atatelekeza sera za nani? Kwanza siamini ati bado Watanzania wanamhitaji Mh Lowasa kuongoza hii nchi kwa sababu amepata fursa zaidi ya moja kuongoza idara na taasisi mbali mbali za umma ambazo hakutuachia kumbukumbu nzuri za ku-miss huduma yake. Ninachofikiri ni kuwa Mh Lowasa anakusudia kuingia madarakani kwa inda na hila ili atekeleze matakwa binafsi. Kwa muktadha huu sidhani ati atazingatia sera za chama ama kundi lolote atakapokuwa raisi wa nchi hii.
Mpaka sasa anafanya mambo yote haya pekee yake?
Swali zuri sana hili, hata hivyo binafsi sijui kama anafanya harakati zote hizi peke yake. Endapo anafanya harakati zote hizi peke yake basi yatupasa tujiulize ni nini msukumo wa harakati hizi. Ama endapo anafanya harakati hizi chini ya uratibu wa kikundi binafsi ama kikundi fulani ndani ya CCM pia tunalazimika kujiuliza ni nini dhamira inayosukuma mipango na utekelezaji wa harakati hizi. Watanzania tunalo angalizo zuri tuliloachiwa na Mwl Nyerere kuwa 'mtu anayeng'ang'ania kuingia ikulu hatuna budi kumwogopa kama ukoma'. Ingawa kauli hii ya mwalimu inastigmatize wenye ukoma, lakini maudhui ya kauli hii ni kuwa Watanzania tupambane kwa kila mbinu kuepukana na tatizo baya kama la ugonjwa wa ukoma. Hivyo yeyote anayelazimisha kwenda ikulu hatuna budi kumkatalia maana hatujui dhamira yake ya kung'ang'ania kufikia nafasi ya maamuzi ya mwisho katika nchi yetu hii tunayoiita nchi changa.
Achilia wapinzani wake wa ndani ya chama chake na vyama pinzani. Anachofanya Mh Lowasa kinawatia ukakasi baadhi ya wanaCCM ambao hawaridhishwi na harakati zake hizi, hivyo kwanza atalazimika kupata ridhaa ya wanaCCM kabla hajapeperusha bendera ya CCM. Hii sio kazi nyepesi kama wengi wetu tunavyofikiria na kujiaminisha kuwa Lowasa atawabwaga wana CCM wenzake kirahisi kwa vile eti anakubalika sana kwa wajumbe wa NEC na CCM