ranchoboy
Member
- Feb 22, 2022
- 61
- 94
Mwaka juzi, kama mwezi wa kumi, nilikuja hapa JamiiForums kuomba ushauri kuhusu kusoma Masters mara tu baada ya kumaliza Degree yangu ya kwanza.
Asilimia kubwa ya wadau waliniponda.
Baadhi waliniambia, “Another jobless”, wengine, “Degree ya kwanza haijakulipa, unatafuta nyingine?”
Lakini kulikuwa na watu baadhi na mmoja wao namkumbuka , anaitwa HollySpirit walinipa moyo hadi nikajihisi tena kuwa mtu. Hata kwenye familia yangu wengine walipinga, ndugu pia walikataa. Lakini mzee wangu hakujali – akanirudisha shule.
Changamoto zilikuwa nyingi. Kusoma Masters bila ajira si jambo rahisi, hasa ukiwa na wenzako wenye check number vyeo na mishahara, na wewe huna lolote kiukweli kejeri zilikuwa nyingi sana wengine waliona kama tunapoteza muda kwa sababu ya hali ya sasa ya ajira nchini. Changamoto zilikuwa nyingi ikiwemo Kukosa hela ya kula, hata kulala njaa kwa sababu wazazi nao wanamajukumu mengi pia utu uzima sometime aibu kuomba omba hela, Kutoka geto saa 12 asubuhi na kurudi saa 4 usiku nikisoma kwa bidii. Nilijua haya yote ni sehemu ya njia ya mafanikio. Basi bwana Mungu si athumani alisikia maombi yangu na bidii yangu akaiona – nikamaliza mwaka wa kwanza ( coursework)na GPA ya 4.3 . Baba yangu alifurahi sana kwa kweri. Kisha mwezi wa kumi mwaka jana, dunia yangu ilibadilika. Baba yangu – mtu aliyekuwa nguzo yangu – alifariki. Nilihisi nimeanguka. Nilifikiria kuacha masomo. Lakini marafiki walinitia moyo. Wengine waliniahidi kuchangia ada yangu. Niliona wazi Mungu hutuma watu wake mahali anapotaka. Baada ya hayo kupita mambo yalikaa sawa Niliendelea na research. Bila kutarajia, mwezi uliopita nikaitwa kazini. Huzuni pekee – baba yangu hajaona matunda kwenye mti alioupanda mwenyewe. Lakini naendelea kwa heshima yake.Leo Nakaribia kukamilisha publications zangu. Siku moja nitazileta hapa JamiiForums kama ushuhuda wa kwamba
Hata ukiwa umedharauliwa, ukiwa na njaa, ukiwa na upweke – ukiendelea kusonga mbele, milango itafunguka.
Funzo
Usikubali maoni ya watu yakupangie maisha. Changamoto zako ni mbegu za ushindi wako. Marafiki wa kweli hujitokeza wakati wa dhoruba. Mungu hufanya mambo kwa wakati wake, bila kutarajia. Uvumilivu ni urithi wa mashujaa.
Mwisho wa thread.
Kwa yeyote anayepitia giza sasa – endelea kutembea. Asubuhi inakuja. 🌅