UMASKINI HAPANA
Senior Member
- Jan 3, 2017
- 105
- 47
Kuchelewa kwa mvua msimu huu ulinipa changamoto ya kutafuta mashamba katika Irrigation schemes kwani huko huwa hakutegemi mvua, kulima ni mara mbili kwa mwaka na kuvuna ni uhakika. Katika hangaika hangaika zangu nilipata wasaa wa kufika kijiji kimoja kinaitwa Mkula kwenye Mkula Irrigation scheme. Kwa kweli wanakijiji wa Mkula wana neema, maji ya uhakika pale mashamba yao yana rutuba kuvuna ni uhakika kwa kweli ni raha wana Mkula wamependelewa kwa kiasi chake sidhani kama wanaijua njaa kabisa. Tatizo ni kuwa mradi una cover ekari chache sana, niliuliza nikaambiwa ni ekari 600 tu ambazo zinamilikiwa na wanakijiji takribani 148. Mwenye kujua Irrigation schemes zingine wazimwage hapa ili tukipata wasaa watu tunatembelea na kwenda kujifunza kilimo huko.
JF Members, wakulima na wajasiriamali karibuni kuchangia.
Asanteni.
JF Members, wakulima na wajasiriamali karibuni kuchangia.
Asanteni.