Naona CCM hiko kwenye matatizo makubwa , kama kile kilichoandikwa hapo juu ni cha kweli. Na inaonyesha dhahiri ya kuwa CCM ina tatizo kubwa la uongozi kwani message wanazotoa viongozi wa nafasi za juu zinapingana. Hili sio jambo zuri kwa chama ambacho kinataka kuendelea kuongoza. Wapinzani nafasi mliyokuwa mkiiomba, sasa mmeipata.
Ujumbe umefika na lugha iliyotumika ni nyepesi ya darasa la saba.umesema tumekusikia, rudia kusoma tena halafu tafakari halafu utagundua kuwa hujaeleweka na hutaeleweka, wrong avenue!!
sammykm70
Join Date: Sat Aug 2009
Posts: 1
Thanks: 1
Thanked 0 Times in 0 Posts
Rep Power: 0
hiyo si ndiyo hiyohiyo unayoiona?
He deserves itView attachment 5677
Spika akikabidhiwa ngao na mkuki kama ishara ya ushujaa na wazee wa jadi katika baadhi ya vijiji alivyohutubia.
Kumekucha!
Keil,
Nafikiri hapa tusimhukumu JK aka mwenyekiti wa CCM. Kama chama kinaendeshwa kwa msingi wa kidemokrasia then yeye hana kosa kama wajumbe wengi walikuwa wakishabikia, ilikuwa ni jukumu la wajumbe wanaopinga ufisadi kuja juu na kumtetea Sita pamoja na hoja zao. Sasa kinachooekana mafisadi wameiteka NEC, kwa nini hatujiulizi kikao hiki ambacho habari zake ziliriki jijini mapema jinsi mafisadi RA na EL walivyokuwa wamejiandaa, sasa itakuwaje Mzee wetu Tinga tinga na memu sapu wake (Anna Kilango) walale mbele? Hapa JK angesimaa kuwazuia kuzumgumza angeitwa dikteta, na hiyo si CCM tunayoifahamu. Sasa ni jukumu letu tunaopinga ufisadi tusimame na tuseme waziwazi badala ya kujificha na kushindwa kutokea kutetea hoja zetu.
Kinachosikitisha zaidi ni kwamba JK amekaa kimya kabisa na hasemi chochote. Kitendo cha kukubali kuunga kamati ndogo ni kutaka kukwepa kufanya maamuzi mazito ambayo ni kazi ya kiongozi wa juu.
Jana Makamba anasema mafisadi wabebeshwe mizigo yao na siyo kukibebesha chama. Sasa kama NEC yote inatetea mafisadi na CC yote inatetea mafisadi kwanini tusikibebeshe chama sifa ya ufisadi. Kama chama kinataka kujipambanua na mafisadi, kinatakiwa kuchukua hatua ya ama kuwafukuza mafisadi ama kuwaunga mkono wabunge wote wanaopinga ufisadi kwa nguvu zote.
CCM itashindwa kusimama kwenye majukwaa ikifika 2010 kama itakuwa bado inaendelea kuwakumbatia mafisadi, mbaya zaidi timing ya hili tukio ni mbaya sana, angalau ingekuwa ni miaka 2 kabla ya uchaguzi wadanganyika wengi wangesahau, lakini wakisema wamtose Sitta mwezi Novemba, basi watakuwa wanajiweka mahali pabaya zaidi na itawawia ugumu kujitetea.
The bottom line ni kwamba uongozi wote wa juu wa CCM ni ama mafisadi au umewekwa na mafisadi ili kulinda maslahi ya mafisadi. Kwa mwendo huo CCM haiwezi kujipambanua na ufisadi. Njia pekee kuwatosa hao jamaa ama wawabebe lakini wa-risk kupoteza majimbo mengi.
Ngoja tusubiri Mzee Mwinyi na Kamati yake ndogo watakuja na kipi kipya na pia kikao cha Bunge cha Novemba kitatoa mwelekeo.
Malecela alijua nini kitatokea na akaamua kumbeba mkewe na kukimbilia London. Huko London kwenyewe walienda kwa gharama ya nani?
Mafisadi wanawashinda hawa wapiganaji kwasababu wote wana madudu yao mengi na yanajulikana. Sitta hawezi kuhama CCM kwasababu wenzake watammaliza kwa muda mfupi; ana madudu mengi mno ambayo wakiamua kuyatoa hatakuwa hata na pa kutokea nje. Sitta siko Mrema au Hamad, hao hawakuwa na kashfa za kujitajirisha binafsi na ndio maana CCM ilipata shida sana kuwachafua.
Mrema angelikuwa na busara nzuri, alishawashinda CCM.
Ila na nyie moderators ni pumbafu kabisa, kwanini mnafuta posts zangu kwenye hii thread? Kama mnataka nifungieni kabisa nitahamia kwa Michuzi maana hapa JF pamekuwa na mawazo ya upande mmoja. Watu wanapiga makofi utafiri wako kwenye Ze Comedy. Futeni na hii post na sitachangia tena.
Malafyale,Is Kyela's Engineer amongst of JF's Great Thinkers? Namuelewa vyema kijana huyu Engineer wa Kyela na nilijua tu mwisho wake utakuwa ni huu kwani huwa hawezi kushindana kwa mtiririko hoja!MODS kuweni wakali zaidi kwa watu wasio na adabu kama akina Engineer wa Kyela.
Thanks Invisible hawa wanaopollute ukweni dawa yao ni hiyo!Invisible mbona unafuta posts zangu