Safari ya kwanza UNO 1955 Nyerere alisafiri bila ya chanjo

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
20,921
30,266
SAFARI YA KWANZA UNO 1955 MWALIMU NYERERE ALISAFIRI BILA YA KUPATA CHANJO

Abdul Sykes anamwambia mdogo wake Abbas, ''Nyerere anasafiri kwenda UNO na lazima adungwe sindano (vaccination).

Mimi siwaamini hawa Waingereza wasije wakamdhuru.

Hakikisha kuwa Nyerere anapata ''vaccination certificate,'' lakini hapigwi sindano."

Hivi ndivyo ilivyokuwa.
Nyerere hakuchoma sindano.

Vaccination Certificate ilipatikana lakini Mwalimu hakupiga sindano na akasafari kwenda New York bila ya kuchanjwa.

Picha hiyo hapo chini nafanya mahojiano na Balozi Abbas Sykes nyumbani kwake Sea View mwaka wa 2012.

1701098190423.jpeg
 
'So what' ! ndivyo nilivyo hamaki.

So what J.K.N hakupigwa chanjo? Kwamba alikuwa na tishio la afya dhidi ya UNO?

Anyways hii taarifa inatueleza ni jinsi gani Nyerere na wenzake walivyokuwa majasiri na washupavu wakiwa tayari kuhatarisha maisha yao ili kufikia malengo yao ya kupata Uhuru.

Ni wazi kwamba Nyerere, Abdul Sykes na wengineo walipenda na kujali Uhuru wa Tanganyika na walikuwa tayari kufanya chochote kinachohitajika ili kuenda UNO.

Hatahivyo, ni muhimu kutambua kuwa Uamuzi huo unaweza kuonekana kuwa ni reckless au ungeweza kuhatarisha afya za waliopo UNO. Wakati kinyume chake, kama alivyo hadithia A.Sykes Waingereza/wazungu ndio wangeweza kumdhuru. Vilevile mkumbuke wakati huo ulaya na kwingineko kulikuwa na magonjwa ya wazungu kama visununu n.k

Kumbe, kumbe wenzake waliogopa/aliogopa asije akadhurika na chanjo.

Picha hii siyo tu inatueleza ni jinsi gani, hawa Ndugu zetu walivyokuwa wamepevuka na wanvyofikiria, bali pia inatuambia character za Wakina Abdul Sykes, Julius Nyerere na wenzao kwqmba walikuwa tayari kwavlelote lile.

Uzuri,pamoja na kuwa kungewezekana kutokea matokeo tofauti, for instance athari hasi kule UNO...nafikiri

...itakuwa sahihi kusema athari na matokeo yake yalikuwa Chanya

Utaona pia hawa ma architect wa Uhuru wa Mtanganyika na Afrika kwa ujumla walikuwa na maono na mafikirio, yaani Inteligence ya hali ya Juu.

Bora hakupigwa hiyo sindano.

Aluta Continua.
 
Syll...
Kuna mengi sana.

Abbas Sykes alinitia simanzi aliponihadithia alipokwenda London kuchukua mwili wa Nyerere akiwa Mwenyekiti wa ATC.

"Wengi hawajui kuwa Nyerere alikuwa kwetu sisi ni ndugu mimi waliokuwa serikalini wakinichukulia kuwa safari ile nafasi yangu ilikuwa Mwenyekiti wa ATC.

Mimi nimemuona Nyerere siku ya kwanza anakuja kuonana na Bwana Abdul na toka siku ile akawa ndugu yetu.

Nilikwenda London kuchukua mwili wa ndugu yangu."
 
Hujaiona sababu ya Nyerere kutokuchanjwa, hata ulete hiyo sababu yako?

Au hujaipenda? Au mradi tu ulete ujuwaji?
 
Mtanisamehe nikiwaza Ujamaa, Muungano fake, kuiba uchaguzi wa Zanzibar 95 namuona Nyerere naye alikuwa na makosa makubwa ya kiuongozi na hastahili hizi sifa tunazompa. Haya ni maoni yangu binafsi.
 
Mwalimu Nyerere alikuwa anaamini kinga ya mwili wake.

Alaaniwe yule aliyemletea tissue zenye sumu kutoka huko kwa Mzee Madiba.
 
Hujaiona sababu ya Nyerere kutokuchanjwa, hata ulete hiyo sababu yako?
Wewe umeiona? Sababu gani ya kwangu madamu tena? Umeona nimepinga sababu aliyoileta Mzee mohamed au basi tu ulitaka kuweka duku duku lako.

Au hujaipenda? Au mradi tu ulete ujuwaji?
Weka ulijuwalo wewe basi. Ati ujuwaji! Hutaki?

Tukienda shule tukafundishwa unasema tunaleta ujuwaji!

Hebu tulia.

Hivi nawewe ulipelekwa shule kufokafoka tu? Shabash.
 
Syll...
Kuna mengi sana.

Abbas Sykes alinitia simanzi aliponihadithia alipokwenda London kuchukua mwili wa Nyerere akiwa Mwenyekiti wa ATC.

"Wengi hawajui kuwa Nyerere alikuwa kwetu sisi ni ndugu mimi waliokuwa serikalini wakinichukulia kuwa safari ile nafasi yangu ilikuwa Mwenyekiti wa ATC.

Mimi nimemuona Nyerere siku ya kwanza anakuja kuonana na Bwana Abdul na toka siku ile akawa ndugu yetu.

Nilikwenda London kuchukua mwili wa ndugu yangu."
...kweli mengi yalikuwepo.

...nakumbuka siku hizo kama jana tu.

Nilielezwa it was logistically challenging, kwani Serikali ilitegemea ujio wa Wakuu wengi wa Nchi za nje na kwasababu walitegemea siku ya kutizama mwili uwanjani taifa kutakuwa na joto, basi waliiamua kuweka, viyoyezi kwenye matenti kupunguza athari juu ya mwili na wageni kutoka nje.
 
Back
Top Bottom