Kigarama
JF-Expert Member
- Apr 23, 2007
- 2,492
- 1,230
Kila uchao nguvu ya ushawishi ya wanaoendesha BODABODA inaongezeka kwenye jamii ya watanzania, Bodaboda ni usafiri lakini sasa ni hadhi (status) kwenye Jamii yetu. Matukio ya hivi karibuni yameonyesha kwamba kuna wajanja wachache wameanza kuiona nguvu hiyo ya waendesha Bodaboda kwenye masuala ya kijamii hasa siasa na wameanza kuwekeza huko.
Kwa hali ilivyo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 BODABODA itakuwa ni kete muhimu sana kwa wanasiasa wetu na muda si mrefu tutaanza kuona wanasiasa wakinyang'anyana vikundi vya waendesha Bodaboda kwa kugombea kuwa "walezi" wao!!