Safari ya kuelekea Ikulu imeanza kwa kasi ya kuwapumbaza waendesha bodaboda?

Sasa mkuu..unasema boda boda ni hukumu ya kifo ni kutukatisha tamaa vijana..mimi nipo kwenye boda boda mwaka wa 3..sasa na kwa kazi hii namudu kuwatunza mama yangu na wadogo zangu....INGEKUWA POA ungetutajia hizo fursa..mkuu..lakini kiukweli vijana hatuna jinsi na hatuna njia nyingine ya kujipatia ridhiki hasa kwa sisi wenye elimu ya ngumbalu..
 
mm naona hyo idea ni nzur.ukiangalia ufaulu nchini umeshuka,w2 walio mtaani ni wengi sana so kugawa bodaboda itachangia ongezeko la ajira.kwa case ya ajal ni jukumu la kila m2.kutokuwa makini kwa madereva isiwe sababu ya kutofanya maendeleo.ckatai kwamba ajal nying sasa hv ni kwa sababu ya boda boda bt hyo ni challenge ambayo ina 2pasa ku handle,kuweka mbinu ya kupunguza ajal ndio jibu zur.cdhan kama mkiwa wazaz wa familia mtaacha kununua v2 vya thamani kama vyombo vya udongo kisa watoto wanaweza vivunja
 
Mnyakolo muyangu.

Kugawa pikipiki ni dhambi tu kama nia ni kujijenga kisiasa kwani hiyo itakuwa ni rushwa ya moja kwa moja.
Ili kuepusha vifo, huyo mgawaji ni vema atoe mafunzo au ahakikishe waendeshaji wamehitimu mafunzo ya uendeshaji pikipiki.
Ukweli ni kwamba hakuna binadamu anayekufa kabla ya wakati wake.
Remember we are spiritual being experiencing life in physical body, we clock out when it is our time.

wajinga ndio waliwao
 
Nafikiri, kugawa bodaboda sioni kama kuna tatizo. Isipokua wagawiwaji wa bodaboda wapewe darasa la jinsi ya kuzitumia na kuziendesha kwa ufasaha, ili kuepusha ajali. Pia watengewe maeneo maalumu ya hizo boda boda kufika, mfano katika barabara kuu zisi ruhusiwe kuingia, pia wahakikishe boda boda zote wazifungie kidhibiti mwendo ili speed ichezee kwenye 25km/h au 35km/h nafikiri kwa hili litawaokoa ndugu zetu.
 
je hawa waendesha tax hatima yao nini?
maana wamekosa soko huku wakilipa kodi na moter vehicle
 
There is no free lunch.....someone once said! Unadhani hizo pikipiki zinatolewa bure! Unafikirii kwa nini wasingetoa mashamba vijana wakalime?
 
Jiulize swali kama vijana wote wa kada yako watapewa bodaboda ni nani ataendeshwa?

Achilia mbali bodaboda kuwa ni kifo mkononi je ndofurusa pekee ya vijana kujiajili?

Shule zinakufa wanaongeza divisions kwa nini wasiimarishe shule ili mkajitafutia ajira mkiwa na akiri ya ujadiria mali kuliko hii ya sasa
mm naona hyo idea ni nzur.ukiangalia ufaulu nchini umeshuka,w2 walio mtaani ni wengi sana so kugawa bodaboda itachangia ongezeko la ajira.kwa case ya ajal ni jukumu la kila m2.kutokuwa makini kwa madereva isiwe sababu ya kutofanya maendeleo.ckatai kwamba ajal nying sasa hv ni kwa sababu ya boda boda bt hyo ni challenge ambayo ina 2pasa ku handle,kuweka mbinu ya kupunguza ajal ndio jibu zur.cdhan kama mkiwa wazaz wa familia mtaacha kununua v2 vya thamani kama vyombo vya udongo kisa watoto wanaweza vivunja
 
Kugawa bodaboda sio tatizo kwa vijana walio wengi tatizo ni hao wanaogawiwa hizo pikipiki wengi wao hata leseni hawana na hata walionazo hawajui hata veta iliko sasa unategemea nini? Serikali iweke sheria kali na isimamie kwamba kila dereva wa bodaboda ni lazima aende veta kujifunza namna ya uendeshaji uliosalama. Tatizo lingine vijana wanachukulia pikipiki kama baiskeli ndo maana zinawaèeruhi na kuwaua sana.
 
Sasa mkuu..unasema boda boda ni hukumu ya kifo ni kutukatisha tamaa vijana..mimi nipo kwenye boda boda mwaka wa 3..sasa na kwa kazi hii namudu kuwatunza mama yangu na wadogo zangu....INGEKUWA POA ungetutajia hizo fursa..mkuu..lakini kiukweli vijana hatuna jinsi na hatuna njia nyingine ya kujipatia ridhiki hasa kwa sisi wenye elimu ya ngumbalu..

Kabla ya bodaboda ulikuwa unafanya nini?! Duniani huko walio na akili wanahubiri fursa zinazoleta ajira maalam kama viwanda n.k. nyie kina EL na J M wanawahubiria bodaboda kwa kujipatia kura halafu mnashangilia!!!!!!!!!
Waulize kama wao na wana wao wanatumia usafiri wa bodaboda. Ninawalaumu china pia kwa kutoionea huruma nchi kama tz.
 
Haya yote ni wanasiasa kutimiza malengo yao.Kweli kabisa,tunawaandaa vijana Kuwa consumers badala ya wazalishaji.wangepewa hata zile bodaboda za kilimo kwanza na mashine za kuzalisha kama za kusindika.Hatukatai zinasaidia usafiri kwa kusikofikika vijijini,kwa nini waangaliwe wa mjini tu?
Mbeligiji aliwapa gitaa wazaire ili kuwapumbaza akili wabaki wanacheza mziki na wao watawale bila kikwazo na kuchuma utajiri.
IPO KAZI 2015
 
Kila uchao nguvu ya ushawishi ya wanaoendesha BODABODA inaongezeka kwenye jamii ya watanzania, Bodaboda ni usafiri lakini sasa ni hadhi (status) kwenye Jamii yetu. Matukio ya hivi karibuni yameonyesha kwamba kuna wajanja wachache wameanza kuiona nguvu hiyo ya waendesha Bodaboda kwenye masuala ya kijamii hasa siasa na wameanza kuwekeza huko.

Kwa hali ilivyo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 BODABODA itakuwa ni kete muhimu sana kwa wanasiasa wetu na muda si mrefu tutaanza kuona wanasiasa wakinyang'anyana vikundi vya waendesha Bodaboda kwa kugombea kuwa "walezi" wao!!

na ndio maana unavyokuwa na timu ya mpira ili uweze kushinda ni lazima ufanye mazoezi,huwezi kutegemea juju kupata ushindi.
na ktk siasa ndio hivyo,huwezi kulala kitandani na mke wako na ukasubiri siku ya kupiga kura ukitegemea utapata ushindi na kuwa rais ama mbunge ama mwenyekiti wa kijiji,kama unandoto hizo basi waache waotaka nafasi za uongozi watumie kila aina ya nafasi inayopatikana kuelekea huko.
wachina wana usemi wao
"kama wewe unasema haiwezekani basi usiwazuie wanaotaka kufanya iwezekane"
 
Ndugu yangu NCH hii haifikiriwi kupungukiwa na WAJINGA kila cku wanaibuka wapya! watu wa CCM wameona Jamaa wa Boda boda uwezo wao wa kufikir ni DUNI ndomana wamewageukia kwa ahadi za kiPUUZI kabisa! Utashangaa watoa AHADI watashinda kwa mambo km hayo yakijinga! Wakiingia madarakani wakianza kurudisha PESA wa2 watalalamika kaz kweli kweli,,!

Badili usemi kidogo,"Jamaa wa Boda boda uwezo wao wa kufikir ni DUNI"Hapa unawatukana wengine,siyo kauli ya kiungwana.Omba radhi na badili usemi.
 
We n kitasa hujui ukisemacho zaid ya chuki ya kisiasa tu uliojazwa huku jf paspo kuchanganya na akili zako bnafssi,nkwambie tu kama wataka kiwanda cha pikipiki kipo kwenye mchakato wa awal,kitakuwa maeneo ya kurasin,shimo la udongo,ufund na mivinjen kule.........Watanzania tuache kulalamika ebu tuamke kwan nnchi n yetu sotee
Nilitegemea wangeanza kukemea ukiukwaji mkubwa wa sheria za barabarani unaofanywa na waendesha bodaboda,na kwakutumia ushawishi wao kuhakikisha utaratibu mzuri unawekwa kwa waendesha bodaboda,tofauti na ilivyo sasa ambapo kila kitu kinafanyika kiholela.
Bodaboda zinapaki mahali popote,wanabeba abiria zaidi ya mmoja,hawajali wala kuheshimu taa zinzoongoza magari,na matokeo yake ni kusababisha ajali nyingi za kizembe.
Nadhani walio wengi hawana driving licences au hata kama wanazo ni za kimangumashi.
Kama kiwanda cha pikipiki kinajengwa bora wangeimalisha vitengo vya mifupa katika hosipitali zetu kwanza nakupanua motuary kabla ya hicho kiwanda, maanake kiama kinakuja.
Baada ya ujio wa usafiri wa bodaboda,takwimu za ajali zilizo sababisha vifo na ulemavu wa kudumu zimeongezeka kwa kasi ya ajabu na endapo hizo takwimu zingekuwa zinawekwa wazi mara kwa mara wengi wetu tungejiuliza kabla yakupanda bodaboda.
 
Kwa kweli watanzania tuna mawazo negative sana, mi sioni kama kuna ubaya wa kugawa bodaboda kwa vijana. Kwa tatizo la ajira la nchi yetu na ukosefu wa elimu mi naona sio vibaya vijana kuwezeshwa angalau kwa hii biashara ya bodaboda ambayo kwa wastani inaweza kumpatia kijana at least sh. 8000 kwa siku. Kwanini mnaangalia vifo tu, we unafikiri bodaboda zikipigwa marufuku ni asilimia ngapi ya vijana watashift haraka kwenda kwenye biashara nyingine. Ushabiki wa siasa pembeni mi ni CDM ila napongeza vijana kupewa bodaboda zaidi na zaidi, cha kufanya ni kuwapa elimu zaidi kuhusu sheria na usalama wa barabara. That's it
 
me yangu macho tu tumechoshwa na hiz siasa miaka ka 52 hv ya uhuru lakini bado sioni mwelekeo wa taifa hili, nasema tumechoka tunahitaji mabadiliko
 
alianza Lowasa , sasa kavamia january ! Bali cha kufurahisha ni kwamba wote hawa wanatoka kwenye kile chama chakavu , na uzuri wa bahati ni kwamba kila mtanzania anafahamu vizuri kuhusu uchakavu wa ccm .

mimi na ww tunaelewa madudu ya ccm,fanya research watz/vijana wangapi wanaoamini na kuona e.lowasa ndo suluhisho lao??,watu wamemezeshwa sumu na wakameza so usijiamini sana kwamba watz wote waouona uchakavu wa ccm
 
alianza Lowasa , sasa kavamia january ! Bali cha kufurahisha ni kwamba wote hawa wanatoka kwenye kile chama chakavu , na uzuri wa bahati ni kwamba kila mtanzania anafahamu vizuri kuhusu uchakavu wa ccm .

Mkuu usitumie kizungu kutaja majina yule kijana anaitwa MWEZI WA KWANZA na baba yake mdogo ni MAMVI wamechakaa mbaya kiongozi hata ukiwapeleka kwa mchina hawanyooki tena
 
Back
Top Bottom