Safari ya kuelekea Ikulu imeanza kwa kasi ya kuwapumbaza waendesha bodaboda?

Kigarama

JF-Expert Member
Apr 23, 2007
2,492
1,225
Kila uchao nguvu ya ushawishi ya wanaoendesha BODABODA inaongezeka kwenye jamii ya watanzania, Bodaboda ni usafiri lakini sasa ni hadhi (status) kwenye Jamii yetu. Matukio ya hivi karibuni yameonyesha kwamba kuna wajanja wachache wameanza kuiona nguvu hiyo ya waendesha Bodaboda kwenye masuala ya kijamii hasa siasa na wameanza kuwekeza huko.

Kwa hali ilivyo kwenye uchaguzi wa mwaka 2015 BODABODA itakuwa ni kete muhimu sana kwa wanasiasa wetu na muda si mrefu tutaanza kuona wanasiasa wakinyang'anyana vikundi vya waendesha Bodaboda kwa kugombea kuwa "walezi" wao!!
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,151
2,000
alianza Lowasa , sasa kavamia january ! Bali cha kufurahisha ni kwamba wote hawa wanatoka kwenye kile chama chakavu , na uzuri wa bahati ni kwamba kila mtanzania anafahamu vizuri kuhusu uchakavu wa ccm .
 
kill

JF-Expert Member
May 21, 2013
1,830
0
ccm watahangaika sana hizo boda boda ni kama wanatoa sadaka kiama cha chama chakavu ccm 2015 kama meli titanic ilipozama watu hawakuamini kama meli ile inaweza kuzama ndivyo ccm itakavyokufa bila wao kuamini
 
Feedback

JF-Expert Member
Mar 14, 2011
7,995
1,500
Serikali imesahau madhara ya kuruhusu machinga kufanya biashara holela kwa sababu za kisiasa.

Leo inawalea bodaboda wanaovunja sheria wazi wazi kwa sababu hizo hizo, siku wakianza kutunisha misuri kama wamachinga wa mtaa wa Kongo serikali isianze kulialia.
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,502
2,000
[h=5]2003-2006, Wamachinga walikuwa ndo talking ya kampeni na baada ya kampeni wanasiasa waliojinadi kuwasaidia wakakaa kimya ukitaka kusikia habari zao hadi muda wa Bunge la Bajeti,
2013-2015 Ni zamu ya waendesha Pikipiki alimaarufu BODABODA, kama kawaida ya wanasiasa wetu wanajua ongezeko la vijana ni kubwa hivyo wengi wataishia kuwa kuwa waendesha bodaboda, sasa najiuliza kwanini hao wanasiasa wahajengi kiwanda chapikipiki hapa Tanzania? Ili tuone kama kweli wanania ya kuwasaidia vijana wawe na pikipiki zao au ndo Daraja la kupitia kuelekea MAGOGONI?[/h]
 
Kiboko.

JF-Expert Member
Jul 31, 2013
2,838
2,000
We n kitasa hujui ukisemacho zaid ya chuki ya kisiasa tu uliojazwa huku jf paspo kuchanganya na akili zako bnafssi,nkwambie tu kama wataka kiwanda cha pikipiki kipo kwenye mchakato wa awal,kitakuwa maeneo ya kurasin,shimo la udongo,ufund na mivinjen kule.........Watanzania tuache kulalamika ebu tuamke kwan nnchi n yetu sotee
 
Baba Joseph17

JF-Expert Member
Jul 15, 2013
8,502
2,000
We ndo kitasa mpango wa kiwanda cha pikipiki ni wa kampuni ya Honda ya Japani nachozungumzia hapa ni hao jamaa zako kuwatumia bodaboda kama daraja lao la kuingia magogoni, msipende ubwete, leteni mipango ya kuwasaidia waondokane na kupata ajali kila siku madaktari wameshachoka.

We n kitasa hujui ukisemacho zaid ya chuki ya kisiasa tu uliojazwa huku jf paspo kuchanganya na akili zako bnafssi,nkwambie tu kama wataka kiwanda cha pikipiki kipo kwenye mchakato wa awal,kitakuwa maeneo ya kurasin,shimo la udongo,ufund na mivinjen kule.........Watanzania tuache kulalamika ebu tuamke kwan nnchi n yetu sotee
 
Ulukolokwitanga

JF-Expert Member
Sep 18, 2010
8,403
2,000
Ndugu zanguni,

Naomba mnisamehe, lakini hili wazo la kugawa boda boda naliona sawa na kugawa vifo na ulemavu kwa vijana wetu tu .

KWANI HAKUNA AJIRA NYINGE YA KUJIAJIRI ZAIDI YA BODA BODA?

Tanzania inaelekea kuzimu, kuna ajira nyingi tu zaidi ya boda boda

JITAMBUE!

Big up brother umeongea pointi ya uhakika Sana.

Tihongidze
 
Marire

JF-Expert Member
May 1, 2012
12,062
2,000
tunatafuta kura mambo ya vifo baadae.
Bugando kuna wodi maalum ya ajali za bodaboda sasa inabidi waje wajengewe hospital yao kabisa.
mzee wa rambirambi leo umetisha
 
nngu007

JF-Expert Member
Aug 2, 2010
15,869
1,225
Ndugu zanguni,

Naomba mnisamehe, lakini hili wazo la kugawa boda boda naliona sawa na kugawa vifo na ulemavu kwa vijana wetu tu .

KWANI HAKUNA AJIRA NYINGE YA KUJIAJIRI ZAIDI YA BODA BODA?

Tanzania inaelekea kuzimu, kuna ajira nyingi tu zaidi ya boda boda

JITAMBUE!

Hapo nimekuunga MKONO... Kuendesha BODABODA sio kuelewa chochote; Wangevichukua VILE VIWANDA walivyoviuza ambavyo sasa hivi ni MAGOFU na kuvifufua na pesa za GAS then kuajiri hao VIJANA wetu na kuwapa SKILLS...
 
BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
105,207
2,000
Nakuunga mkono ndio maana nikaandika niliyoyaandika. Haya ni maswali ya kumuuliza fisadi Lowassa anayepigia debe boda boda katika jitihada zake za kujisafishia njia kuelekea Ikulu 2015.

No mkuu laikini boda boda kwangu ninavyoiona ni sawa na ile movie ya death wish...
 
Madela Wa- Madilu

JF-Expert Member
Mar 24, 2007
3,070
1,195
Mnyakolo muyangu.

Kugawa pikipiki ni dhambi tu kama nia ni kujijenga kisiasa kwani hiyo itakuwa ni rushwa ya moja kwa moja.
Ili kuepusha vifo, huyo mgawaji ni vema atoe mafunzo au ahakikishe waendeshaji wamehitimu mafunzo ya uendeshaji pikipiki.
Ukweli ni kwamba hakuna binadamu anayekufa kabla ya wakati wake.
Remember we are spiritual being experiencing life in physical body, we clock out when it is our time.

Ndugu zanguni,

Naomba mnisamehe, lakini hili wazo la kugawa boda boda naliona sawa na kugawa vifo na ulemavu kwa vijana wetu tu .

KWANI HAKUNA AJIRA NYINGE YA KUJIAJIRI ZAIDI YA BODA BODA?

Tanzania inaelekea kuzimu, kuna ajira nyingi tu zaidi ya boda boda

JITAMBUE!
 
Fitinamwiko

JF-Expert Member
Aug 13, 2012
4,804
1,500
Ndugu zanguni,

Naomba mnisamehe, lakini hili wazo la kugawa boda boda naliona sawa na kugawa vifo na ulemavu kwa vijana wetu tu .

KWANI HAKUNA AJIRA NYINGE YA KUJIAJIRI ZAIDI YA BODA BODA?

Tanzania inaelekea kuzimu, kuna ajira nyingi tu zaidi ya boda boda

JITAMBUE!
Ulichosema ni kweli kabisa, huo ndio mtaji wa CCM kupata kura za vijana. Chris hongera kwa uona uozo w chama chako
 
measkron

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
3,783
2,000
No mkuu laikini boda boda kwangu ninavyoiona ni sawa na ile movie ya death wish...
Chris Lukosi naungana na wewe bila kupinga na kikumbwa hawa vijana hakuna training ya uendeshaji wanayoenda kwenye tafiti iliyofanyika Muhimbili among more than 200 boda boda accident clients involved huwezi amini waliokuwa na leseni were only 30s. Ripoti ilihusisha hadi polisi ili kuweza kusaidia but hiyo ndo vijana inawapa ajira but kwa kweli ni death sentence giving a youth boda boda
 
Last edited by a moderator:

Mag3

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,670
2,000

Sijui heri ni ipi; kugawa boda boda ama kugawa pipi!Masikini Tanzania; taratibu tutafika tu!

dolevaby

JF-Expert Member
Aug 25, 2013
11,535
2,000
Ulichosema ni kweli kabisa, huo ndio mtaji wa CCM kupata kura za vijana. Chris hongera kwa uona uozo w chama chako

Ndugu yangu NCH hii haifikiriwi kupungukiwa na WAJINGA kila cku wanaibuka wapya! watu wa CCM wameona Jamaa wa Boda boda uwezo wao wa kufikir ni DUNI ndomana wamewageukia kwa ahadi za kiPUUZI kabisa! Utashangaa watoa AHADI watashinda kwa mambo km hayo yakijinga! Wakiingia madarakani wakianza kurudisha PESA wa2 watalalamika kaz kweli kweli,,!
 
Ngonepi

JF-Expert Member
Jun 2, 2013
1,723
2,000
Ndugu zanguni,

Naomba mnisamehe, lakini hili wazo la kugawa boda boda naliona sawa na kugawa vifo na ulemavu kwa vijana wetu tu .

KWANI HAKUNA AJIRA NYINGE YA KUJIAJIRI ZAIDI YA BODA BODA?

Tanzania inaelekea kuzimu, kuna ajira nyingi tu zaidi ya boda boda

JITAMBUE!

Tukuulize wewe na maCcm wenzio!
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom