SoC02 Safari ya Dar es Salaam

Stories of Change - 2022 Competition

mzeelazaro

New Member
Aug 25, 2022
2
2
Safari Ya Dar es Salaam

Dar es Salaam ni moja mkoa kati ya mikoa 33 na moja ya jiji kati ya majiji 5 katika nchi ya Tanzania. Dar es salaam ina wilaya 4 ambazo ni Kinondoni, Ilala, Temeke na Kigamboni. Dar es Salaam ni jiji mashughuli linalozungumziwa Zaidi katika mikoa mingine kuwa ni jiji la biashara likiwa limetawaliwa na majengo mazuri na shughuli mbalimbali ikiwemo biashara halali na siyo halali.

Moja kati ya ndugu zangu alikwisha kufika Dar es salaam hapo awali na kurudi mkoani kisha kutueleza jinsi gani jiji hilo linavyovutia chini ya usimamizi wa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam mhe. Amos Makala. Ndugu yangu uyo alilipamba sana jiji hilo hadi kufikia hatua ya mimi kutamani Zaidi kufika na sikusita kumueleza ndugu yangu uyo matamanio yangu ya kufika katika jiji hilo, ila alisisitiza sana juu ya mimi kusoma kwa bidi ili kuweza kufika uko na bila ivo basi kwangu itakua kama ndoto tu kufika jijini Dar es Salaam na alisisitiza nikienda pasipo kuwa na elimu nzuri basi nitaishia kuwa mtoto wa mtaani na baadae nitajiingiza katika vikundi vya ujangiri. Nilimhaidi ndugu yangu uyo nitasoma kwa bidii na kufika Dar es salaam. Hapo awali nilikuwa nasoma masoma ya sayansi nikiwa kidato cha nne na nilitamani sana kusoma elimu yangu ya juu nikiwa jijini Dar es salaam.

Nilipomaliza kidato cha nne nilimpigia simu ndugu yangu aliekuwa tayari yuko Dar es salaam na kumueleza sasa niko tayari kuja jijini Dar es salaam na alikubali na ndipo safari yangu ilipoanzia kutoka mkoani mpaka Dar es salaam.

Niliwasili stendi ya Magufili ikiwa ni saa 7 usiku na ndugu na ilikuwa tumechelewa sana kuwasili kwa sababu gari liliaribika njiani. Na ndugu yangu ilipofika mida ya saa 4 alirudi kwake na mimi pia wakati nawasili stendi simu yangu ya kiganjani ilikuwa imekwishaishiwa chaji hivyo niliposhuka kwenye gari niliona bado stendi imechangamka sana kama bado ni mchana nilijiuliza sana usiku huu niende wapi kwenye usalama zaidi ila cha kushangaza nilikutana na vijana wengi pale nje wakiwa na rika kama mimi na wengine wadogo Zaidi. Nilijiuliza maswali mengi sana yakiwemo,

  • Je , familia za hawa watoto zimewatelekeza?
  • Je, jamii hii ya stendi inawachukuliaje hawa vijana na Watoto?
  • Je, hawa vijana walipata kweli elimu?
  • Je, misingi ya ajira inaruhusu mtoto mdogo kuanza kufanya biashara?
  • Je, sasa ni usiku hawa Watoto wanapata wapi muda wa kupumzika?

Nilijaribu kutafuta mtoto mmoja na kukaa naoi li kupata taarifa iliokamilika ya kisa cha wao kujihusisha na biashara ya kuuza vitu usiku pale stendi, japo haikuwa rahisi katika kuwakusanya maana walihisi nawafanyia uovu, ila niliwahakikishia watatakuwa salama. Na wakaanza kunipa taarifa kamili ambapo Watoto wanakuwa wengi sana muda wa mchana na jioni ila inapofika mida ya usiku wengi huingia katika majumba mabovu na nje ya fremu za maduka na kujiegesha. Na chanzo kikuu cha wao kufika jijini ni kuitwa na baadhi ya watu kutoka Dar es salaam ili kuja kufanya kazi za ndani na punde tu wanapofika basi wanazima mawasiliano na kuwapoteza Watoto hao hivyo kusababisha Watoto wengi kubaki stendi na kujiunga na vikundi visivyofaa. Mtoto yule alisisitiza kuwa sisi unaotuona stendi mida hii ya usiku sio wote ni wema na baadhi ya Watoto wameshajiunga na makundi ya ovyo na wengine kukamatwa. Kiukweli niliishiwa nguvu niliwaza pengine na ndugu yangu atakuwa amenifanyia hivyo hivyo na kunileta Dar es Salaam kuwa mtoto wa mtaani.

Kulivyokucha ilibidi nifike ustawi wa jamii wa stendi hiyo na kujua taratibu za kwanini hawa Watoto wanafanya kazi hapa stendi umri wao hahuruhusu wao kufanya kazi. Japo umri wangu pia ulikuwa mdogo ila nilikuwa najiamini sana kwa sababu sikuwa na nidhamu ya uoga. Na ustawi wa jamii ulisisitiza kuwa watu wengi wanawafanyia utapeli sana watu walioko mkoani hasa kwa kuwaaminisha kuwa jijini kuna nafasi nyingi sana za kazi na wengi wao uanza safari kwa mawasiliano mazuri na punde tu wanapofika mawasiliano ukata kabisa na Watoto hao kubaki kutangatanga mjini na mwisho wa siku wengi wanaishia kubaki stendi. Ustawi wa jamii ulitoa pia elimu na kunifanya kuwa balozi na kusema jamii inapaswa kuwaheshimu sana Watoto na kuzidi kuwapa elimu maana wanapowanyima elimu na utulivu wa akili ni kumkosesha haki zake za msingi katika maisha.

Na kumaliza kwa kusema Serikali inachukua hatua kwa Watoto hao katika kuhakikisha inawarejesha nyumbani kwao kwa kuwalipia nauli na kuwarejesha katika familia zao na kuendelea na masomo. Punde sio punde na ndugu yangu alifika ustawi wa jamii kuripoti kupotea kwangu, alitahamaki sana alipokuta namhoji afisa ustawi wa jamii wa eneo hilo. Na alifurahi sana aliponiona napata ubalozi na aliniambia elimu hii ndio nilikuwa nakwambia siku zote inahitajika.

Funzo

Vijana na Watoto wengi katika umri mdogo wamekuwa wakijihusisha na matumizi ya mitandao ya kijamii na kuingia katika sitofahamu ya kuahidiwa vitu vizuri katika miji mikubwa hivyo kuwapelekea kuacha masomo na kukimbilia kwenye majiji wakioyajua vizuri na matokeo yake kutelekezwa na ndoto zao kuishia njiani. Neon moja kwa wazazi ni , sawa tunahitaji Watoto wetu waijue teknolojia lakinikuwe na kipimo na teknolojia ya mawasiliano kwa Watoto yapaswa kuwa ni kwaajili ya masomo yao tu na siyo vingine kwani vinapelekea hartari kubwa sana.

Asanteni.
 
Back
Top Bottom