Saddam Hussein, C.I.A & Italian Intelligence Service: Tuhuma za wizi wa Uranium Powder (Yellowcake) kutoka migodi ya kampuni za Ufaransa nchini Niger!

Kule kwa Bold akitoa story haiishi mara moja pia anachelewa kutoa ufafanuzi mwisho wana jf wanaishia kugombana
Okay sawa mkuu. Ila The Bold ninamkubali sana namna anavyopangilia story zake. The guy is so talented. Yeye kuchelewa kujibu labda ni kutokana na wingi wa majukumu ya kazi zingine pamoja na familia. But all in all, I love his stories.
 
Okay sawa mkuu. Ila The Bold ninamkubali sana namna anavyopangilia story zake. The guy is so talented. Yeye kuchelewa kujibu labda ni kutokana na wingi wa majukumu ya kazi zingine pamoja na familia. But all in all, I love his stories.
Dr Magufuli ni mtu mwenye huruma nami nakubaliana naye kabisa. Wanaomuogopa Rais Magufuli ukiwafuatilia kwa makini utagunduza kuwa ni watenda maovu na wanashikwa na uwoga kutokana na uovu wanaoutenda.
 
Saddam Hussein, C.I.A & Italian Military Intelligence Service (SISMI): Tuhuma za wizi wa Uranium Powder (Yellowcake) kutoka migodi ya kampuni za Ufaransa nchini Niger!

View attachment 1547984

UTANGULIZI SEHEMU YA KWANZA
===========
Nyaraka za kughushi za mkataba wa kuuziana madini ya uranium huko chini Niger hapo awali zilitolewa mnamo mwaka 2001 na SISMI (Idara ya Ujasusi ya Jeshi la Italia), ambayo inaonekana kuangazia jaribio lililofanywa na aliyekuwa Rais wa Iraq ndugu Saddam Hussein kutana kununua yellowcake uranium powder kutoka nchini Niger wakati wa mzozo wa silaha za sumu huko Iraq.

Kwa misingi ya hati hizi na viashiria vingine, serikali za Marekani pamoja na Uingereza zilisisitiza kwamba Iraq ilikuwa inakiuka vikwazo vya Umoja wa Mataifa (UN) kwa kujaribu kununua vifaa vya nyuklia kwa madhumuni ya kuunda silaha za maangamizi (WMDs). Idara ya usalama ya Uingereza (MI6) ilikuwa sahihi kuwaeleza ndugu zao wa Washington kuhusu athari hiyo.

View attachment 1547986

Iraqi - licha ya kuwa na "yellowcake" ya kwake mwenyewe - ilikuwa imenunua vifaa kutoka Niger mapema mwaka 1981 na wakati huo haikuwa imewajulisha Shirika la Kimataifa la Nishati ya Atomiki (wakaguzi wa silaha walisitisha uzalishaji wa "Yellowcake" ndani ya Iraq baada ya mwaka 1991). Mnamo mwezi Oktoba 31, mwaka 1998, Iraq ilitangaza kumalizika kwa ushirikiano wake na wakaguzi wa U.N., ambao walizuiliwa kutoingia nchini humo.

BACK TO THE TOPIC
========
Ili kuhalalisha uvamizi wa Marekani wa mwaka 2003 nchini Iraq, maafisa wa Ikulu ya White House walitumia taarifa za uongo na za kuungaunga za kiintelijensia ili kutoa shutuma hadharani kwa madai kwamba Iraq ilikuwa na mpango wa kutengeneza silaha za nyuklia.

Shutuma nzito na za kutatanisha zaidi ni kwamba Iraq ilitafuta na kununua kwa siri tani karibia 500 za madini ya uranium kutoka nchini Niger kwa lengo la kuyasafisha na kutengeneza silaha za nyuklia. Zilikuwa ni shutuma zinazofanana na ukweli kwa maana kwamba Iraq ilikuwa na matumizi ya namna moja tu ya uranium - kutengeneza silaha za nyuklia.

View attachment 1547994

Wissam al-Zahawie, mwanadiplomasia wa Iraq aliyekuwa akifanya shughuli zake huko Vatikani alisafiri kwenda mpaka mji mkuu wa Niger Niamey mnamo mwezi Februari 1, mwaka 1999. Al-Zahawie aliomba msaada wa serikali ya Niger kwa kuondoa vikwazo vya biashara vya UN vilivyowekwa dhidi ya Iraq baada ya Vita vya Ghuba (Vita ya Kwanza ya Iraq).

Mnamo mwaka 2000 Rocco Martino, askari polisi wa zamani wa Italia, alidaiwa kuulizwa na afisa wa shirika la ujasusi la Italia (SISMI), Antonio Nucera ikiwa ana nia ya kupata pesa za haraka na chap chap.

Martino alikubali na akatambulishwa kwa Laura Montini, afisa ujasusi wa Jeshi la Italia (SISMI) aliyekuwa anafanya kazi ndani ya ubalozi wa Niger huko jijini Rome, ambaye alianza kuiba na kutoa hati kuhusu uuzaji wa Niger wa uranium kwenda Iraq - ikidaiwa ya kuwa ndio lilikuwa kusudi la kweli la safari ya bwana Wissam al-Zahawie - Kwa Martino kuzunguka katika mashirika ya ujasusi ya nchi zingine za bara la Ulaya ambao ndio wateja wakubwa wa nyaraka zile.

View attachment 1548047

Hati hizo zilikuwa zimetumwa kwa njia ya fax kwa kutumia namba za simu za kutoka nchini Niger, labda ili Wafaransa, Waingereza pamoja na njia zingine za kijasusi za kusikiliza mawasiliano ya elektroniki waweze kuzinasa na kuzichukua.

Mwishoni mwa mwaka 2000 tume ya ujasusi ya Uingereza walipata ripoti ya kughushi iliyokuwa inadai kwamba, "taarifa zisizo rasmi za kijasusi zilionyesha ya kuwa kuna nia ya Iraq kupata madini ya uranium." Uingereza baadaye ilitoa waraka wake ikidai ya kuwa Iraq "ilikuwa ikitafuta idadi kubwa ya madini ya uranium kutoka Afrika, licha ya kukosa mpango wowote wa matumizi ya amani ya nguvu za nyuklia ambao ungeweza kuyahitaji."

Kufikia majira ya msimu wa joto wa mwaka 2001, Rocco Martino alikusanya nakala kamili (dossier) ya hati za madini ya uranium za Niger zilizokuwa zimeghushiwa kutoka katika karatasi zilizoibwa za ubalozi wa Niger nchini Italy na files za idara ya Ujasusi wa Jeshi nchini Italy (SISMI). Report kamili iliandikwa kwa lugha ya kifaransa kwenye stationery ya serikali ya Niger kilichowekwa alama ya "nyaraka ya siri."

View attachment 1548055

Barua hiyo bandia ya mwezi Julai 27, mwaka 2000 ilikuwa kutoka kwa Rais wa Niger kwenda mwenzake wa Iraq, iliyosainiwa na muhuri wa Rais (seal of the President) wa Niger.Ilisomeka, "Nina heshima ya kurejelea kifungu Na. 381-N1 2000, kuhusu utoaji wa madini ya uranium, uliotiwa saini jijini Niamey mnamo mwezi Julai 6 kati ya Serikali ya Jamhuri ya Niger na Serikali ya Iraq.

Barua ile ilielezea usafirishaji wa tani 500 za uranium powder. Mkusanyiko tofauti wa nakala nzima ya Niger ilisambazwa huko ulaya yote, zingine zilizoandikwa kwa maandishi ya mkono ili kusahihisha makosa yaliyokuwa dhahiri na wazi, na bei ya kuanzia ya manunuzi ni hadi $ 100,000 euro kwa wakati ule.

Mnamo mwezi Oktoba 15, mwaka 2001 kituo cha CIA huko Rome kilipokea ripoti za idara ya Ujasusi wa Jeshi Italy (SISMI) za mpango wa kuuziana madini ya uranium kati ya nchi za Niger na Iraq, na kupeleka habari hizo mpaka ikulu ya Washington ikiwa na onyo kwamba report ile ilikuwa bado haijathibitishwa na vyanzo vingine vya taarifa.

View attachment 1548057

Wamarekani baadaye walipigwa na butwaa na shutuma za maafisa wa serikali yao miezi michache kuelekea uvamizi wa U.S.A huko Iraq kwa madai ya uuzaji wa madini ya uranium kutoka nchini Niger. Makamu wa Rais ndugu Dick Cheney alijitokeza hadharani, akimuambia mwanahabari Wolf Blitzer wa CNN mnamo mwezi Machi 14, mwaka 2001 kwamba Saddam Hussein alikuwa akitafuta kwa nguvu zote kumiliki silaha za nyuklia.

Mnamo mwezi Desemba 7, mwaka 2002, Iraq ilitangaza kwa wakaguzi wa silaha wa umoja wa mataifa (UN) kwamba haina mpango wowote wa kutengeneza wala kumiliki silaha za nyuklia.

Lakini waziri mdogo katika wizara ya mambo ya nje anayehusika na masuala ya Udhibiti wa Silaha na Usalama wa Kimataifa bwana John Bolton alisimamia majibu rasmi ya U.S., yaliyotolewa mnamo mwezi Desemba 19, mwaka 2002 akiishutumu Iraq kwa kujifanya kutokomeza "juhudi zake za kupata uranium kutoka nchini Niger."

View attachment 1548006

Mnamo mwezi wa Januari mwaka 2003, Mshauri wa masuala ya Usalama wa taifa Condoleezza Rice alimuunga mkono Bolton, akidai katika gazeti la New York Times ya kwamba Iraq "ilishindwa kuielezea jumuiya ya kimataifa juu ya juhudi zake za kupata madini ya uranium kutoka nje ya nchi zilikuwa na malengo yapi."

NITAENDELEA NEXT TIME. NIPO KWENYE MSIBA HAPA NYUMBA YA JIRANI.....!!!!!

USISAHAU
: ENDELEA KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USICHAFUE TASWIRA NJEMA YA TAIFA LAKO. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO.

Pia soma makala hii>>> Kanisa Katoliki Vatican na ushawishi wake juu ya msamaha kwa Waziri Tariq Aziz. Mkristo kindakindaki na swahiba mkuu ( Inner Circle) wa Saddam Hussein
Hahaha hizo hasira watazionyesha kwa lissu kutokana na kusaliti Nchi yetu.
 
Utakuwaje mzalendo kwenye nchi ambayo haitendei Haki Wananchi wake,hakuna uhuru wa kuchagua wanaemtaka..

Tanzania chini ya utawala wa CCM ni janga kwa Taifa..

Sheria tunazipanga Wenyewe,tunazipinga Wenyewe

Watawala wanaanza kuuwa ikiwa sheria haziwabebi wao
 
Back
Top Bottom