Yaliyoikuta US kwa Taliban yamewafika Ufaransa nchini Niger

Webabu

JF-Expert Member
Apr 29, 2010
7,192
10,928
Taifa la Marekani liliingia vitani nchini Afghanistan kwa kisingizio cha kuitia adabu kwa vile ilikataa kumkababidhi Osama kwao aliyetajwa kuongoza uripuwaji wa majengo pacha ya New York.Vita vilikuwa ni vikali sana vilivyouwa maelfu kwa maelfu ya watu nchini Afghanistan.

Matekani hakuna ilichopata isipokuwa hasara kwa miaka karibu 20. Wananchi wa nchi hiyo waligawanyika mpaka wakawa maadui wao kwa wao. Baada ya yote hayo kile kikundi kidogo cha wanamgambo waliotajwa kumhifadhi Osama kwa ufundi kabisa wakaishinda Marekani na kuitimua nchini mwao kwa aibu kabisa kwani walikimbia kwa mfadhaiko mkubwa huku wakiwacha silaha za matrilioni ya dola za kimarekani.

Hali inayofanana na hiyo imeukuta Ufaransa nchini Niger moja ya taifa maskini sana duniani, kwani hatimae baada ya kutunisha misuli yake kwa zaidi ya mwezi mmoja imebidi ikubali kuondoa askari wake wote na kumrejesha balozi wake nyumbani.

Ili kukazia ushindi wao viongozi wa kijeshi wa Niger wamesema wamefunga anga la nchi yao kwa ndege aina zote za Ufaransa au zile zilizosajiliwa kwa jina la nchi hiyo.Hii imekuja baada ya viongozi wa kijeshi waliompindua raisi Bazoum ambaye ni mshirika mkubwa wa Ufaransa kumuweka balozi wa nchi hiyo kweny kizuizi cha ubalozi hadi kufikia kula chakula cha kiasili cha Niger alichopelekewa na wanajeshi hao.

Awali balozi huyo aliondoshewa hadhi za kibalozi.Sambamba na hilo wanachi nao walipiga kambi kukizunguka kituo cha kijeshi cha Ufarannsa.

Kumbuka kilichowapeleka Ufaransa Niger na nchi jirani ilikuwa ni kisingizio cha kupambana na magaidi wa IS ambao walitajwa ni tawi la Alqaeda iliyokuwa ya Osama bin Laden. Hata hivyo wananchi wenyewe wa Niger waliona vitu hivyo ni kizungumkuti kwani hawakujuwa wapi walipo IS na kila siku wakididimia kiuchumi na huku mauwaji yasiyokuwa na sababu yakiongezeka kila mji.

Niger ni moja ya nchi inayochimbwa madini ya Uranium kwa kiasi kikubwa duniani,Wakati Uranium katika soko la kimataifa ikiwa na thamani ya kilo moja kwa dola 240 lakini Ufaransa walikuwa wakijiuzia kwa senti 80 chini ya dola moja kwa kila kilo.
 
Hali ya usalama hapo Niger sio nzuri sana, mashambulizi yanayofanya na makundi yenye silaha kwa raia na jeshi yameongezeka.
 
Mkuu huko hali bado tete, na wasipoangalia haya mambo ya mapinduzi yatakuwa kitu cha kawaida kwa anayehitaji madaraka.
 
Tunasubiri kuona Niger itakuwaje baada ya hao wafaransa kuondoka. Je amani itarejea na uchumi utaboreka na kuifanya Niger kupiga hatua kimaendeleo?

Lakini kwa kurejea maneno ya yule kaburu marehemu Pieter Bother kwamba hakuna kosa kubwa kama kumpa mwafrika mamlaka ya kutawala basi ni wazi kwamba watu wa Niger wasitegemee miujiza kwani hali itakuwa mbaya zaidi hadi wataichukia hii serikali ya sasa. Tuweke macho.
 
1695888493821.png
 
Back
Top Bottom