Ufaransa yapoteza madini ya manganese Gabon baada ya uranium Niger

kimsboy

JF-Expert Member
Oct 17, 2016
9,000
17,909
Ufaransa yapoteza madini ya manganese Gabon baada ya uranium Niger

Wakati dola la kikoloni la Ufaransa likiwa bado limeemewa kwa kupoteza madini ya urani ya Niger, ghafla moja imepigwa pute na kupoteza madini ya manganese baada ya kutokea mapinduzi ya kijeshi nchini Gabon.

Ufaransa imekuwa ikidhibiti rasilimali za madini ya manganese kwa muda mrefu nchini Gabon. Manganese ni moja ya madini ya kimkakati katika sekta ya uhunzi na uzalishaji wa chuma na feleji, utengenezaji wa betri na kazi nyingine nyingi. Lakini saa chache tu baada ya mapinduzi ya Gabon, kampuni kubwa ya uchimbaji madini ya Ufaransa iitwayo Eramet lilitangaza kuwa limesitisha shughuli zake zote nchini Gabon.

Wataalamu wa mambo wanaofuatilia matukio yanayoendelea kutokea barani Afrika hasa magharibi mwa bara hilo wanaamini kuwa hivi sasa limeingia kasi wimbi la Waafrika wanaopinga uporaji wa kitaasisi wa rasilimali za nchi zao unaofanywa na mkoloni kizee wa Ulaya, yaani Ufaransa.

Madini ya manganese
Wataalamu hao wanaamini kuwa, ijapokuwa kinachoshuhudiwa hivi sasa ni kupigwa teke Ufaransa katika nchi hizo, lakini pia mapinduzi yanayotokea ni dhidi ya tawala vibaraka ambazo Ufaransa ndiyo iliyoziweka madarakani kwa njia ya moja kwa moja au ya nyuma ya pazia ili kufanikisha malengo ya dola hilo la kikoloni na kuangamiza rasilimali za mataifa hayo ya Afrika.

Hivi sasa majeshi ya nchi za Afrika yana jukumu zito la kulinda maslahi ya wananchi wao.Ni jambo lililo wazi kwamba demokrasia inayotakiwa na Wamagharibi kwa nchi hizo za Afrika ni ile inayolinda maslahi ya madola ya kibeberu kama Ufaransa na inapotokea kiongozi yoyote kupingana nao, madola hayo yanaeneza madai ya uongo ya kupigania demokrasia kumpiga vita na yanahakikisha kuwa serikali kama hiyo haitawali barani Afrika
 
Back
Top Bottom