SADC yaingia makubaliano na AFC/M23

SADC yaingia makubaliano na AFC/M23

Kwenye mkutano wa viongozi wakuu wa majeshi ya nchi wanachama wa SADC, huko Goma, Serena Hotel, badhi ya makubaliano yamefikiwa, ikiwa ni pamoja na haya:

-AFC/M23 kusaidia majeshi ya SADC kuondoka nchini
-SADC kuondoka na silaha zao, huko za serikali ya DRC zikikabidhiwa AFC/M23.

-wataalam wa SADC na M23 kukagua hali ya uwanja wa ndege wa Goma kwa sasa

-SADC imekubali kukarabati uwanja wa ndege wa Goma

-AFC/M23 imeikubalia SADC, kwamba, baada ya ukarabati, itumie uwanja huo kuondoka wanajeshi wake na silaha zao (SAMIDRC).


Kwa kifupi, AFC/M23 ndo mshindi wa vita, na eneo ililopigania, ni haki yake.
Chanzo cha taarifa, tafàdhali!
 
Hiyo ni mbinu ya kivita. Inaitwa military retreat. Ubelgiji imepeleka commandos wanaokadiliwa kufika 400 na zana za kivita kama vifaru, drones na zana mbalimbali. Commandos wa Ubelgiji wanaenda kutoa mafunzo kwa jsshi la Congo na makundi ya wanamgambo yanaiunga mkono serikali ya Kinshasa. Inasemwa pia kuwa commandos wa Ubelgiji wataingia mzigoni direct.

Hawataweza kufanya lolote.
 
28 March 2025
Goma, Kivu ya Kaskazini
Congo DR

1743339779650.jpeg

Jenerali Rudzani Maphwanya mkuu wa majeshi ya ulinzi wa Afrika ya Kusini SANDF akisalimiana na askari wa SAMIDRC baada ya makubaliano na M23 ya kuondoa majeshi ya nchi za SADC
 
28 March 2025
Goma, Kivu ya Kaskazini
DR Congo

Viongozi wakuu kijeshi wa SADC SAMIDRC na AFC mubashara katika shughuli ya maridhiano iliyofanyika hoteli ya Serena Goma ...


View: https://m.youtube.com/watch?v=8CaXVcTyRJg
Mmoja wa viongozi wakuu wa kijeshi kutoka nchi za SADC kutoka Tanzania Major General Ibrahim Michael Mhona wa TPDF / JWTZ akiwa ameshika nyaraka za maridhiano.

Makubaliano hayo yalifanyika huku viongozi wakuu wa pande hizo mbili za SADC SAMIDRC na waasi wa AFC / M23 kwa bashasha na kuheshimiana huku furaha ikionekana baada ya maafikiano hayo...

Wengine waliohudhuria hafla hiyo ni General Rudzani Maphwanya, mkuu wa majeshi ya ulinzi ya Afrika ya Kusini SANDF; Lieutenant General Geoffrey C. Zyeele, kamanda wa jeshi la Zambia ; Major General Saiford Kalisha, mwakilishi wa mkuu wa majeshi wa Malawi ; Professor Kula I. wa kamati ya Stroika ya SADC ya siasa, ulinzi na mambo ya usalama



Pia mbali ya Major General Sultani Makenga; alikuwepo Brigadier General Bernard Byamungu, naibu mkuu wa majeshi ya waasi ARC / M2R; na Bahati Musanga Erasto, Governor wa jimbo la Kivu ya Kaskazini DR Congo .


TOKA MAKTABA :
19 January 2022

KOZI USALAMA NA STRATEJIA
Major General Ibrahim Michael Mhona wa TPDF / JWTZ alipata kuwa mkuu wa Chuo cha Ulinzi wa Taifa, chuo mahiri kwa mafunzo ya mapana yanayohusiana na stratejia mkakati mbalimbali

View: https://m.youtube.com/watch?v=YGH4z19yylk
Katika video hii maktaba jenerali Ibrahim Michael Mhona wa anafafanua masomo ya NDC Chuo cha Ulinzi wa Taifa yanayotolewa, ambayo yana mambo mtambuka mengi

Wako hadi na vitambi kabisa hao walikuwa ni kula michemsho ya supu ya mbuzi asubuhi na machapati tu
 
Back
Top Bottom