SADC yaingia makubaliano na AFC/M23

SADC yaingia makubaliano na AFC/M23

TOKA MAKTABA :

Jeshi imara la South Afrika tangu 2016 misheni zake Congo zimeshindwa pamoja na kuwa wana zana kali za kisasa :

View: https://m.youtube.com/watch?v=x6BYYyukjDI
Hii 𝘀𝘁𝗼𝗿𝘆 ilirushwa mara ya kwanza 𝟭𝟴 𝗦𝗲𝗽𝘁𝗲𝗺𝗯𝗲𝗿 𝟮𝟬𝟭𝟲.

Akisindikizwa na helikopta maarufu ya Rooivalk mfano wa ngome yenye ulinzi uliosheheni silaha kali , Carte Blanche anasafiri hadi kambi ya kijeshi iliyotekwa hivi majuzi ndani ya misitu ya tropiki kaskazini mwa Beni katika Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.

John Webb anapata ruhusa ya kipekee kuvifikia vituo vya mstari wa mbele vya jeshi la South Africa SANDF katika eneo maarufu la liliopachikwa jina la kuogofya la Pembe Tatu ya Mauti (Triangle of Death) katika Mkoa wa Kivu Kaskazini tunapowatembelea wanajeshi wetu walio mstari wa mbele katika vita dhidi ya waasi wa ADF.

Tunakutana na wanajeshi ambao uMauti umeshindwa kuchukua roho zao katika uwanja wa vita na vile vile katika majukumu muhimu ya usaidizi wa mapigano, na marubani wa SANDF wanaofanya kazi kama sehemu ya kitengo cha anga cha Umoja wa Mataifa ambao wamekuza sifa ya ustadi na ujasiri wa kufika maeneo haraka kupambana na adui.

Carte Blanche pia anakutana na Jenerali wa SANDF Derrick Mgwebi ambaye aliteuliwa kuongoza operesheni ya jumla ya Umoja wa Mataifa ya kulinda amani nchini DRC - ambayo bado ni Misheni kubwa zaidi ya kulinda amani duniani.

View: https://m.youtube.com/watch?v=x_SYts84EGM

Huelewi unachotetea. Unajua mwenyekiti wa troika ni nani?
 
Hakuna jeshi lililowahi kushinda vita vinavyopiganwa maelfu ya kilometa kutoka nchi yake, kwanza ni gharama kubwa na pili uwanja wa vita hautabiliki.
Kwasasa hata Marekani haiwezi kushinda vita hii, M23 wamejichanganya raia ni vigumu jupigana na kwa kinga na ngao ya raia
 
Hapo wanachofanya ni kuwatoa wanajeshi wao na zana na baada ya hapo mpango mpya unaanza. SADC haiwezi kuwaacha watutsi wa Rwanda waisumbue Congo.
Yaani utoe wanajeshi wako kwenye uwanja wa vita baada ya kushindwa Kisha uende kujipanga tena kurudi kupigana ? Gharama hizo anabeba nani?
 
Yaani utoe wanajeshi wako kwenye uwanja wa vita baada ya kushindwa Kisha uende kujipanga tena kurudi kupigana ? Gharama hizo anabeba nani?
hao sio rahisi kurudi tena. ila izo sehem ziangaliwe aisee naona warundi wanaongelea vita ya ukanda. sijui wanaota au kuna kitu wameshakiona.
 
Kwani tactical retreat maana yake nini?
Huwezi kuwazia tactical retreat baada ya kushindwa lengo kuu la vita. Retreat ilitakiwa kufanyika mwezi wa pili wakati M23 walipoamua kuiteka Goma na Sake ambapo ndio ngome ya SADC... Badała yake walizidiwa na matokeo yake ni kunyoosha bendera nyeupe.... Unaelewa maana yake ni nini... Kushindwa vita!
Plan kuu ya SADC ilikuwa kuwashambulia M23 kule misituni kwa mabomu ya grad na kuwafuatilia M23 kutokea angani kwa ndege vita za DRC na RSA. Tanzania walirusha mabomu ya hatari hadi M23 wakalalamikia kitendo cha Tanzania ndani ya SADC kutumia silaha kali hivyo kwa watu wanaodai haki yao kutoka kwa Serikali yao.
Matokeo yake M23 walibadilisha mbinu na kuamua kuhama misituni ambapo ingekuwa rahisi kuteketezwa bila kujitetea, wakaamua kuuteka mji wa Goma, ambao kimsingi ni mji uliounganika na mji mwingine wa Rwanda uitwao Gisenyi. M23 walitoa taarifa ya kuja kuuteka Goma ndani ya masaa 48.... Hawa SADC walishitukizwa na hata wale mercenaires wa ulaya walijikuta wako kwenye vita kamili bila kujiandaa.....
Mpango wowote wa kurudi DRC kutatua mgogoro wa mashariki ya Congo kwa kutumia silaha hauwezi kufanikiwa. Ili kuwang'oa M23 ndani ya mji wa Goma itabidi kuibomoa Goma yote kama inavyofanya Israël kule Gaza...
Hili sidhani kama Kagame atakaa tu akiangalia jinsi mji wake wa Gisenyi ambao umeunganika na Goma ukiteketea bila kujibu mapigo.... Tanzania tuache kucheza mchezo huu wa hatari kwani utatugharimu sana.
 
Huwezi kuwazia tactical retreat baada ya kushindwa lengo la vita kuu. Retreat ilitakiwa kufanyika mwezi wa pili wakati M23 walipoamua kuiteka Goma na Sake ambapo ndio ngome ya SADC... Badała yake walizidiwa na matokeo yake ni kunyoosha bendera nyeupe.... Unaelewa maana yake ni nini... Kushindwa vita!
Plan kuu ya SADC ilikuwa kuwashambulia M23 kule misituni kwa mabomu ya grad na kuwafuatilia M23 kutokea angani kwa ndege vita za DRC na RSA. Tanzania warusha mabomu ya hatari hadi M23 wakalalamikia kitendo cha Tanzania ndani ya SADC kutumia silaha kali hivyo kwa watu wanaodai haki yao kutoka kwa Serikali yao.
Matokeo yake M23 walibadilisha mbinu na kuamua kuhama misituni ambapo ingekuwa rahisi kuteketezwa bila kujitetea, wakaamua kuuteka mji wa Goma, ambao kimsingi ni mji uliounganika na mji mwingine wa Rwanda uitwao Gisenyi. M23 walitoa taarifa ya kuja kuuteka Goma ndani ya masaa 48.... Hawa SADC walishitukizwa na hata wale mercenaires wa ulaya walijikuta wako kwenye vita kamili bila kujiandaa.....
Mpango wowote wa kurudi DRC kutatua mgogoro wa mashariki ya Congo kwa kutumia silaha hauwezi kufanikiwa. Ili kuwang'oa M23 ndani ya mji wa Goma itabidi kuibomoa Goma yote kama inavyofanya Israël kule Gaza...
Hili sidhani kama Kagame atakaa tu akiangalia jinsi mji wake wa Gisenyi ambao umeunganika na Goma ukiteketea bila kujibu mapigo.... Tanzania tuache kucheza mchezo huu wa hatari kwani utatugharimu sana.
Hawa SADC hawatokubali mkuu, wanamvutia pumzi M23, wakishapata intel ya kutosha na mbinu, ni week moja tu M23 wanaondoka.
 
hao sio rahisi kurudi tena. ila izo sehem ziangaliwe aisee naona warundi wanaongelea vita ya ukanda. sijui wanaota au kuna kitu wameshakiona.
Na hapa ndipo lilipo tatizo! Warundi wana ubaguzi wao wa asili kati ya watusi na wahutu, na upuuzi huu unaendelezwa na Rais wa sasa wa Burundi dhidi ya Rwanda ambao wanajitahidi sana kutoruhusu mambo haya ya ubaguzi wa ukoo.

Kule Musoma kuna wakurwa wa koo zinazogombana hadi kuuana, Hawa ni warinchoka na wanyanchari. Hawa waliuana sana miaka ya 90 kati kwa mambo madogo madogo tu.
Ndayishimiye ndio anataka kuleta vita vya kiukoo vienee EAC.
 
Hawa SADC hawatokubali mkuu, wanamvutia pumzi M23, wakishapata intel ya kutosha na mbinu, ni week moja tu M23 wanaondoka.
Mkuu SADC ni ushirikiano wa kikanda unaogharamiwa na kodi zetu wananchi au rasilimali za nchi mwanachama. Mpaka sasa wamejiingiza katika vita ambavyo havikuwa na sababu, hizi gharama za vita ni kutoka kwenye mifuko yetu, ndio maana raia wa RSA wameshinikiza jeshi lao liondoke DRC.... Wewe unasema watarudi kwa bajeti gani?
Kwanza washukuru tu kuwa M23 wamewaruhusu waondoke na Silaha walizoingia nazo, vinginevyo wangekaza silaha zote za SADC na FRDC ni mali ya M23 baada ya kushinda vita.
 
Mkuu SADC ni ushirikiano wa kikanda unaogharimiwa na kodi zetu wananchi au rasilimali za nchi mwanachama. Mpaka sasa wamejiingiza katika vita ambavyo havikuwa na sababu, hizi gharama za vita ni kutoka kwenye mifuko yetu, ndio maana RSA wameshinikiza jeshi lao liondoke DRC.... Wewe unasema watarudi kwa bajeti gani?
Kwanza washukuru tu kuwa M23 wamewaruhusu waondoke na Silaha walizoingia nazo, vinginevyo wangekaza silaha zote SADC na FRDC ni mali ya M23 baada ya kushinda vita.
M23 na wao wanaelewa wangefanya hivyo pasingekalika..

Mimi nionavyo SADC hawajakaza, walijitokeza kuonyesha tu wameshiriki kuipambaia DRC kama mwanachama mwenzao tokana na makubaliano ya umoja huo.
 
M23 na wao wanaelewa wangefanya hivyo pasingekalika..

Mimi nionavyo SADC hawajakaza, walijitokeza kuonyesha tu wameshiriki kuipambaia DRC kama mwanachama mwenzao tokana na makubaliano ya umoja huo.
Mkuu, nikusanue kitu?... Mpango mzima ni tamaa tu ya utajiri, uwepo wao kule ni pesa inayolipwa na UN. Angalia video ya ugeni wa M23 kwenye kambi ya SAMIDRC1 utagundua kitu walikokuwa serious kwenye hili ni kina nani....
 
Ina maana msimu huu itakuwa hawajapata pesa ya kutosha kutoka kutoka UN, ina maana hili suala lina connection ya moja kwa moja na uongozi wa Trump/siasa za US..

Nakubaliana na wewe, ukiwepo msukumo, iwe fedha, mali n.k sidhani kama SADC watazidiwa na hao M23...
 
Mkuu vita inapangwa na lengo kuu ni kumshinda adui Ili kulinda maslahi ya taifa lako, ndio maana watu wanajitoa kufa. Kwenye hii issue ya DRC, aliyetayari hata kufa, ni M23 ndio lengo lao ni kushinda kwa gharama yoyote maana wana maslahi pale....

Naomba unitonye maslahi ya SADC kupitia SAMIDRC1, wana maslahi gani hasa hadi kufikia hatua ya askari wake kuifia DRC? 🤔
 
Hakuna maslahi lakini M23 inaleta tishio kiusalama katika ukanda huu..
 
Ina maana msimu huu itakuwa hawajapata pesa ya kutosha kutoka kutoka UN, ina maana hili suala lina connection ya moja kwa moja na uongozi wa Trump/siasa za US..

Nakubaliana na wewe, ukiwepo msukumo, iwe fedha, mali n.k sidhani kama SADC watazidiwa na hao M23...
Mkuu SADC waliwahiwa na shabulio la kushitikiza kabla hata hawajatekeleza mpango wao wa mashambulizi. Nina hakika kama wasingenyoosha bendera ingekuwa kilio kikubwa kwa SADC.
 
Hakuna maslahi lakini M23 inaleta tishio kiusalama katika ukanda huu..
Hapana mkuu, fuatilia vizuri utaona M23 ni raia wa Congo wanaobaguliwa na kuuawa kikatili bila kusikilizwa. Jiulize kabla ya wakoloni kuigawa Afrika ina maana watu hawakuwepo na tawala za asili?
 
Mkuu SADC waliwahiwa na shabulio la kushitikiza kabla hata hawajatekeleza mpano wao wa mashambulizi. Nina hakika kama wasingenyoosha bendera ingekuwa kilio kikubwa kwa SADC.
Hata kama M23 wangewamaliza hapo, haikuwa mwisho kwa SADC kupambana zaidi na zaidi, labda hawakutaka kuendelea na vita kwa kipimo cha faida itakayopatikana dhidi ya gharama watakazotumia.

Vita ina levels tofauti, jeshi linaweza kuamua kutumia nguvu kiasi na jeshi linaweza kuongeza nguvu zaidi tokana vita ilivyo na malengo waliyonayo.
 
Hapana mkuu, fuatilia vizuri utaona M23 ni raia wa Congo wanaobaguliwa na kuuawa kikatili bila kusikilizwa. Jiulize kabla ya wakoloni kuigawa Afrika ina maana watu hawakuwepo na tawala za asili?
Kwang mimi naichukulia tofauti kidogo..
Rwanda inatumia upenyo kuidhoofisha zaidi DRC, kuchota mali asili za DRC... na pengine kuingilia siasa za DRC..

Inaanza DRC baadae itafuata sehemu/nchi zingine..
 
Back
Top Bottom