SADC Mungu anawaona jinsi mnavyoitenga Msumbiji na matatizo yao

MakinikiA

JF-Expert Member
Jun 7, 2017
5,011
6,542
1607940368994.png

Ureno imejitolea kuisaidia Msumbiji kupanga mkakati na kuiwezesha jeshi la nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wanaotishia usalama katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado wenye utajiri wa gesi.

Mwezi uliyopita wanamgambo waligeuza uwanja wa michezo kuwa "kichinjio", ambako walikata watu vichwa na miili, kwa mujibu wa ripoti.

Waziri wa Ulinzi wa Ureno, Joao Gomes Cravinho, amesema kundi la wanajeshi wa nchi hiyo kuanzia mwezi ujao litaanza kufanya kazi na wenzao wa Msumbiji.

Wikiendi iliyopita Bw Gomes Cravinho alikamilisha ziara ya kikazi ya siku tatu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Alisema Ureno, ambayo itakuwa rais wa Muungano wa Ulaya kuanzia mwaka 2021, itaunga mkono ombi la Msumbiji la kupewa msaada ambalo tayari limewasilishwa Brussels.

Ghasia katika mkoa wa Cabo Delgado umesababisha mzozo wa kibinadamu, huku zaidi ya watu 2,000 kuuawa na wengine 560,000 kufurushwa makwao.
 
Tatizo viongozi wa Africa karibia wote ni matatizo wanaangalia matumbo yao tu

Akipita kiongozi kwa njia haramu wenyewe wanashangilia,, watu wakiuana wenyewe wapo bize

Tatizo Africa hamna democracy angalia yaliyotokea Tanzania, uwizi wa kura na mwisho wakabariki eti ulikuwa uchaguzi huru
 
Ureno imejitolea kuisaidia Msumbiji kupanga mkakati na kuiwezesha jeshi la nchi hiyo kukabiliana na wanamgambo wa Kiislamu wanaotishia usalama katika mkoa wa kaskazini wa Cabo Delgado wenye utajiri wa gesi.

Mwezi uliyopita wanamgambo waligeuza uwanja wa michezo kuwa "kichinjio", ambako walikata watu vichwa na miili, kwa mujibu wa ripoti.

Waziri wa Ulinzi wa Ureno, Joao Gomes Cravinho, amesema kundi la wanajeshi wa nchi hiyo kwanzia mwezi ujao litaanza kufanya kazi na wenzao wa Msumbiji.

Wikendi iliyopita Bw Gomes Cravinho alikamilisha ziara ya kikazi ya siku tatu katika nchi hiyo ya Kusini mwa Afrika.

Alisema Ureno, ambayo itakuwa rais wa Muungano wa Ulaya kuanzia mwaka 2021, itaunga mkono ombi la Msumbiji la kupewa msaada ambalo tayari limewasilishwa Brussels.

Ghasia katika mkoa wa Cabo Delgado umesababisha mzozo wa kibinadamu, huku zaidi ya watu 2,000 kuuawa na wengine 560,000 kufurushwa makwao.
 
Attachments

  • 1607942141122.gif
    1607942141122.gif
    42 bytes · Views: 2
Basi! Mission accomplished,

Hao Ureno sasa ndio wafadhili wa huo ugaidi na sasa wanaenda kuchota gesi kiulainiii,

Ukiona kifaranga kipo sehemu ujue mamaake hayupo mbali sana. Ni vizuri sasa mama kifaranga kajitokeza.
 
Naishauri serikali ya Tanzania iangalie namna ya kuivamia Msumbiji kama walivyoivamia Zanzibar na kuiweka kwenye muungano fake wa Tembo na sisimizi
 
Majeshi ya Ureno yanarudi tena Msumbiji tangu yaondoke 1975 baada ya Msumbiji na Angola kupata uhuru.

Ila hayarudi kama majeshi ya kikoloni ila yanakuja kuyasaidia majeshi ya Msumbiji kupambana na wanamgambo wa Isis, kweli zama zimebadilika.

Adui wa jana,leo kawa rafiki.
 
Basi! Mission accomplished,

Hao Ureno sasa ndio wafadhili wa huo ugaidi na sasa wanaenda kuchota gesi kiulainiii,

Ukiona kifaranga kipo sehemu ujue mamaake hayupo mbali sana. Ni vizuri sasa mama kifaranga kajitokeza.
Umenifikirisha !!!
 
Back
Top Bottom