Mungu kupitia Torati alikataza GMO

hamis77

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,642
19,018
Mungu kupitia Nabii Musa alitoa maelekezo kuhusu uchanganyaji wa mbengu ili kupata kiumbe kimoja.

Kizazi kiovu baadae walichanganya mbegu za wanyama tofauti wakatoa viumbe wa ajabu kina Godzila ,Mungu kupitia Gharika akawaharibu, Kuna watu leo walikuwa wanabisha haiwezekani kuchanganya mbegu ya kiumbe tofauti na Mwingine ukatoa kiumbe tofauti, Lakini Zamani walifanya, na leo wanadamu wamefikia huko

Tusome Hapa, pia usipoelewa pitia Tafsiri mbalimbali , Humo makanisani hao wanaojiita manabii na wachungaji wakisoma hi mistari wanatafsiri kana kwamba Mungu alizuia kupanda shamba moja mahindi na maharage , Lakini maana halisi Ni kuchukua Mbegu ya kiumbe A ukafanya kuunganisha na mbegu B, Kisha upate KIUMBE MMOJA.

Tusome ...

Kumbukumbu la Torati 22:9 SRUV​

Usipande shamba lako la mizabibu aina mbili za mbegu; yasije yakaondolewa matunda yote, mbegu ulizopanda na mavuno ya mizabibu yako.

Mambo ya Walawi 19:19 SRUV​

Mtazishika amri zangu. Usiwaache wanyama wako wa mfugo wakazaana kwa namna mbalimbali; usipande shamba lako mbegu za namna mbili pamoja;

KENYA WAMERUHUSU GMO, Sasa wanazalisha Maparachichi yasiyo na mbegu Kama haya

IMG_20221025_214323.jpg

Tanzania isionje sumu ya GMO kwa kukijaribu kilimo hiki. India walifanya hili kosa na matokeo yalikuwa ni wakulima wadogo laki tatu (300,000) kujiua wenyewe katika muhula wa miaka 20. Hatima kama hii tuiepuke hapo nyumbani kwa udi na uvumba.

# Vinasaba vya epicyte ambavyo vipo kwenye baadhi ya mazao ya vyakula vya GMO (Genetically Modified Organism) kupitia mbegu zake vitazuia ongezeko la watu duniani, kwa sababu kazi ya hiki kinsaba ni kuwafanya wanaume na wanawake wasizae milele -ingawa tendo la ndoa litafanyika kama kawaida. Na kwa kutumia teknolojia inayoitwa “RNA crop interference technology” wame – “fine-tune” huo uhanithi na ugumba uliowekwa kwenye hiki kinsaba cha epicyte uwaathiri Watu Weusi peke yao. Yes, “…GMO food crops have now been fine-tuned to cause irreversible infertility in black people alone.”

# Kupitia lobbyists waliowekwa kwenye idara zao ziitwazo “Political Action Committees (PACs) makampuni mara nyingi huwa yanaweka mifukoni wasomi pamoja na baadhi ya viongozi wa kitaifa ili kuthibiti, hata kupotosha mataifa lengwa. Nchi yetu iwe macho sana na njama za sampuli hii.

Siku ya Alhamisi ya tarehe 6/10/2022 Dr. Ally, kwenye mtandao wa “Uwanja wa Diplomasia” alichapisha andiko lenye kichwa cha habari kifuatacho: GMO, NDIO AU HAPANA KWA TANZANIA’.
fotolia_66435874_subscription_xxl-1000.jpg
GMO

Kwa mujibu wa matokeo ya tafiti za kitaifa na kimataifa, pamoja na uzoefu (real life experiences) ya watu wanaoishi na kilimo hiki ni vema: “GMO iwe Hapana kwa Tanzania.”

Hili andiko la Dr. Ally nimelisoma kwa kina. Katika kutoa tafsiri za GMO na misamiati mingine ya bayolojia andiko lake limekaa vizuri; lilipopwaya ni katika kujibu hofu za watu kuhusu faida na hasara za kilimo cha uhandisi jeni.
  1. Watu wanasema kwamba tafiti baada ya tafiti zimefanywa na taasisi kadha wa kadha zinazozijitegemea (yaani ambazo hazipokei fedha kutoka kwa ‘bio-tech industry’) na zote zimejiridhisha kuwa hiki kilimo hakifai na hatarishi kwa afya za watu na mazingira pia kinafuta uhuru wa chakula wa mataifa (national food sovereignty), hivyo basi hakihitajiki. Katika tafiti iliyokuwa kubwa kupita zote, yenye kutoa hayo matokeo ni ile ya Umoja wa Mataifa – Agriculture at a Crossroads” – ambayo nchi za Tanzania, Kenya na Uganda ziliidhinisha (ratified it).
ILI KULINDA AFYA ZA WATANZANIA NA MAZINGIRA PAMOJA NA UHURU WA TAIFA WA CHAKULA, “KILIMO CHA GMO KIWE NI MARUFUKU TANZANIA.”
IMG-20221011-WA0240.jpg

Swali la msingi ni hili: Kwa nini taasisi zetu za taifa za utafiti za Tanzania, Kenya na Uganda zinapoteza fedha na wakati kutafiti jambo ambalo limekwisha fanyiwa utafiti “exhaustively” na Umoja wa Mataifa na matokeo yake yapo wazi? Hii, si sawa na kusema baada ya huu utafiti wa Umoja wa Mataifa watu wasitishe tafiti katika fani ya kilimo. La hasha. “Public crop-breeding programmes” ambazo hazirudishi mataifa kwenye utumwa-mamboleo ziendelee, tumekuwa nazo tangu kilimo kiwepo duniani miaka zaidi ya 10,000 iliyopita. Lakini kwa nini tunang’ang’ania GMO ambayo imethibitika: (i) Ina kila aina ya madhara na (ii) Hizo tafiti zetu zenyewe wala hazijitegemei?

(i) Madhara: “In 2009 the American Academy of Environmental Medicine called for a moratorium of GM foods, safety testing and labelling. Their review of the available literature at the time noted that animal studies show serious health risks associated with GMO food consumption including infertility, immune dysregulation, accelerated aging, dysregulation of genes associated with cholesterol synthesis, cell signalling and protein formation, and changes in the liver, kidney, spleen and gastro-intestinal system.” Na madhara haya yamejitokeza katika kila tafiti yenye kujitegemea kutoka kila kona ya ulimwengu.

(ii) Tafiti zetu Hazijitegemei kivipi?
Kwa taarifa, Co-ordinator au Mratibu wa utafiti unaofanywa huko Makutopora ni taasisi moja inayojulika kwa jina la AATF – African Agricultural Technology Foundation – makao makuu yake yapo Nairobi, nchini Kenya. Nani wanafadhili hii “Foundation”? Ni hawa hapa: Bill & Belinda Gates Foundation, Howard G. Buffet Foundation, The Rockefeller Foundation, UKAID, USAID, Feed: Future, Syngenta Foundation & PEPSICO.

Hawa wote wana maslahi makubwa kwenye ‘Bi0-tech Industry’; ushauri wao au misimamo yao haiwezi kujitegemea wala kuwa ya kujitolea kwenye suala la GMO; ushauri na misimamo yao itakuwa inatetea maslahi yao binafsi.

Na kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknoloji ya Tanzania (COSTECH) ya tarehe 06/11/2018, huu mradi wa ,Water Efficient Maize for Africa’ (WEMA) wa huko Makutopora, Dodoma, unafadhiliwa na wafuatao: Bill and Belinda Gates Foundation, Howard G.Buffet Foundation na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la Marekani (USAID) kupitia African Agricultural Technology Foundation (AATF).

Hivi, katika manzili (circumstances) kama hizi kweli tunawategemea hao wafanyakazi wa huko Makutopora waseme ukweli wa kuwa hiki kilimo cha GMO hakitufai?

Hii ‘scenario’, kwa maoni yangu, haina tofauti na ile ya mtu kujitungia mtihani mwenyewe, kujisimamia mwenyewe, kusahihisha mwenyewe na mwishoni kujitangazia matokeo. Inahuzunisha.

(b) Nadharia na Kweli ya Kilimo cha GMO.

Nadharia.

Dr. Ally kwenye andiko lake amerudia nadharia (theory) zinazotumiwa na “spin doctors” wanaonadi kilimo cha GMO. Mathalani, ameandika:
“… Idadi kubwa ya watu (ambayo inakadiriwa kufika bilioni 9.8 ifikapo mwaka 2050), inamaanisha maeneo ya kilimo yanapungua wakati uhitaji wa kuzalisha zaidi ili kulisha watu unaongezeka; hivyo unahitaji mbegu zinaweza kukupa mazao mengi kwenye eneo dogo.”

Ukweli ni Huu.
Ripoti ya Umoja wa Mataifa inayoitwa “Agriculture at a Crossroads” iliyochapishwa mwaka 2008 chini ya mwavuli (auspicies) wa International Assessment of Agricultural Knowledge, Science and Technology for Development (IAASTD) inajibu hiyo hoja ya Dr. Ally kwa undani.

Utafiti wa hii Ripoti ulichukua miaka minne na washiriki walikuwa ni wataalamu 900 kati yao wakiwepo wanasayansi wabobezi 400 kutoka nchi 110. Na wafadhili walikuwa ni Umoja wa Mataifa kupitia taasisi zake zifuatazo: Benki ya Dunia, UNDP, UNESCO, WHO, UNEP, Global Environmental Facility (GEF), Food & Agricultural Organization (FAO) na wengineo. Aidha makampuni ya Biotech yafuatayo nayo yalifadhili huo utafiti: Monsanto, Syngenta, BASF, Unilever, Crop Life International and Association of Global Agrichemical Companies.

Watafiti walipewa hadimu rejea ifuatayo:
“How can we reduce hunger and poverty, improve rural livelihoods and facilitate equitable, environmentally, socially, and economically sustainable development through the generation of, access to, and use of agricultural knowledge, science and technology? And crucially what role if any the controversial technique of genetic engineering should play in feeding the world’s hungry.”

Matokeo ya utafiti yanasema hivi:
“… Kilimo cha GMO hakina mchango wowote kwenye malengo ya kupunguza njaa na umaskini duniani, kuleta lishe bora, afya kwa wanavijiji au maendeleo endelevu ya jamii na mazingira. … Na mfumo unaopiga marufuku wakulima kuhifadhi mbegu utaua uhuru wa chakula wa mataifa.” Ripoti hiyo inaendelea kuuhimiza ulimwengu kujikita katika kilimo cha kikaboni (organic farming) na kuachana na kilimo hiki cha GMO.

Aidha, Dkt. H. Harren, Mwenyekiti Mwenza (Co-chair) wa hiyo Ripoti ya Umoja wa Mataifa “Agriculture at a Crossroads” akijibu Waandishi wa Habari hoja iliyokaririwa na Dr. Ally hapo juu, alikuwa na haya ya kusema:
“… Kwa kweli sioni matumizi yoyote ya maana ya GMOs, hivi sasa au siku za usoni. Tunazalisha chakula cha kuweza kulisha kikamilifu watu bilioni 14, na hiyo ni zaidi ya chakula kitakachohitajika kulisha watu bilioni 9 ambao wanatarajiwa duniani ifikapo mwaka 2050.”

Huu ndio ukweli wa kilimo hiki cha GMO – hakina tija, si muhimu na hakihitajiki; siyo tu hapo nyumbani, bali Afrika na dunia nzima. Tafiti zote za kitaifa na kimataifa zilizokwishafanywa zenye kujitegemea (kwa maana ya kutofadhiliwa na makampuni ya bio-teknolojia) zote zinasema kama hii ripoti inavyosema.

Baada ya ripoti yenye hadhi ya upeo huu kutolewa, katika ulimwengu wa kawaida kilichotakiwa kufanyika ni Umoja wa Mataifa kupiga marufuku kabisa hiki kilimo duniani kote. Kwani haiswihi Umoja wa Mataifa kuwa na “Article” nambari 1 ya “Charter” yake inayohimiza suala liitwalo ‘self-determination of nations’ halafu iunge mkono kilimo ambacho utafiti wake yenyewe unasema kinaua uhuru wa mataifa, yaani inaua hiyo, “self-determination of nations.”

Mgawanyiko wa wadau kwenye Ripoti ya Umoja wa Mataifa.

Baada Ripoti ya Umoja wa Mataifa, Agriculture at a Crossroads kuchapishwa mwezi Aprili 2008 huko Johannesburg, Afrika ya Kusini, wadau waligawanyika katika makundi matatu.

Kundi la kwanza, lilikuwa ni la mataifa 58 ambayo yaliunga mkono na ku – “ratify” hii ripoti, ikiwa ni pamoja na Tanzania, Kenya na Uganda.

Kundi la pili, lilikuwa ni la yale makampuni ya bioteknolojia ambayo yalichangia huu utafiti. Hili kundi lilikataa kusaini au ku – “ratify” ripoti kwa sababu matokeo yalipiga vita maslahi yake.

Kundi la tatu, lilikuwa ni la mataifa mama ya haya makampuni ya GMO, yakiongozwa na Marekani, Kanada na Australia. Kundi hili nalo lilikataa kuunga mkono ripoti; lakini haya mataifa yalikiri kuwa pamoja na kutokusaini kwetu ripoti ni kuntu.

Maswali yanayolilia majibu kwa Afrika ya Mashariki ni haya: Baada ya kusaini hii “comprehensive Report” ya Umoja wa Mataifa dhidi ya kilimo cha GMO, kwa nini hizi nchi bado zinakumbatia hiki kilimo? Je, walikuwa hawajui nini wanasaini? Je, wamenunuliwa na makampuni ya GMO? Au je, wametiswa na mataifa mama ya makampuni haya?

Fauka ya hayo, je, viongozi wa Tanzania na Afrika Mashariki, wanafahamu kuwa: “Genetic Engineering Approval Committee (GEAC)” ya India, iliitahadharisha Serikali yake kuwa: “Bt cotton is not recommended for small farmers” Na GEAC ikapuuzwa? Viongozi wetu wanalifahamu hili?

Sasa hebu tuangalie uzoefu “experience” wa wakulima wadogo walioshurutiswa na serikali yao kukumbatia hiki kilimo cha uhandisi jeni huko India.

India: Maswali karibu hayo hayo ambayo yanaulizwa na wananchi wa Afrika Mashariki yanaweza kuulizwa na wananchi wa India. Mwaka 1970, India iliweka katika Katiba yake katazo la ku – “patent” mimea au “life form.” Lakini miaka ya 1990s Monsanto waliingia India na kuleta hizo sera zilizokatazwa kwenye Katiba ya nchi. Baada ya Monsanto kukamata soko la Bt Cotton kwa asilimia 90, wakulima walipandishiwa bei ya mbegu za hiyo pamba kwa asilimia alfu nane (8,000%).

Wakulima waliposhindwa kununua mbegu, wakawa wanakopeshwa kwa makubaliano ya kulipa baada ya mavuno. Lakini mchanganyiko wa uzorotaji wa ubora wa pamba ya GMO, uliosababisha kushuka kwa bei, pamoja na kuporomoka kwa mavuno kulikotokana na ardhi kuchujuka kwa sababu ya matumizi makubwa ya madawa ya kilimo yanayoendana na mbegu za GMO – kuliwafanya wakulima wadogo wa India washindwe kulipa madeni yao.

Uamuzi wa makampuni ya GMO ulikuwa ni kuwanyang’anya wakulima hao mashamba yao pamoja na mali zingine walizokuwa nazo. Baada ya kujikuta wamepoteza kila kitu ndipo kipupwe cha wakulima wadogo wa pamba za GMO kujiua wenyewe kilipopamba moto. Wakulima wadogo 300,000 walijiua wenyewe katika muhula wa miaka 20. Hivi sasa wakulima wadogo wa pamba walio wengi wameachana na kilimo cha Bt cotton kwa sababu hakina faida.

Mwaka 2018 ndipo Mahakama Kuu ya India ilipoingilia kati na kupiga marufuku ku – ‘patent’ mimea ikinukuu katazo lililopo kwenye Katiba yao tangu 1970. Aidha Mahakama ilifutilia mbali mfumo wa tozo za “royalty or technology surcharges” ambazo Monsanto ilikuwa inawatoza wakulima.

Maswali ambayo Wahindi nao wanajiuliza ni haya: Je, wakati Monsanto wanaingiza hiki kilimo cha kiharamia nchini, hii Katiba ya 1970 ilikuwa wapi? Kwa nini hiyo Mahakama Kuu, ilichelewa kuingilia kati kwa kiasi hiki? Je, Viongozi walinunuliwa, walilaghaiwa au walitishwa?

Kwa wananchi wa Afrika Mashariki swali linguine la kujiuliza ni hili: Iwapo Monsanto walipandisha bei ya Bt cotton kwa asilimia 8,000 huko India, kuna sababu gani ya kuamini kuwa Monsanto hawatatupandishia bei kwa asilimia hizo hapo Afrika Mashariki? Jamani, ndiyo, ubepari ni unyama, lakini unyama ulio kwenye kilimo cha GMO upo katika daraja la peke yake.

Nadharia.
Aidha Dr. Ally anaendelea kusema: “Kuna hoja kwamba GMO si salama kiafya, si sahihi kusema hivyo, maana GMO ni neno la pamoja, hivyo hatuwezi kuhukumu GMOs zote kwa kauli moja.”

Ukweli ni Huu.
Hii kauli ya kuwa hiki kilimo si salama haikutokea kijiweni. Imesemwa na wataalamu baada ya kujiridhisha kwa utafiti. Kwa mfano tafiti za kitaifa za nchi zifuatazo zilithibitisha kuwa GMO si salama: Uingereza, Ufaransa, Austria na Urusi. Na hiyo Ripoti ya Umoja wa Mataifa yenye kurejewa hapo juu, inasema hivyo hivyo.

Pia kutokuwa na usalama kwa GMO kumejitokeza kwenye ‘documents’ 44,000 za siri za Food and Drug Administration (FDA) ambazo zilifunguliwa baada ya hukumu ya Mahakama huko Marekani. Kwenye hizo ‘documents’, wanasayansi wa FDA, yaani wanasayansi wa serikali wanaongelea ukosefu wa usalama wa GMO. Sasa Dr. Ally anaikana hii kauli kwa utafiti upi?

‘Public interest lawyer’, Steven M. Druker, aliyekabidhiwa hizo ‘documents’ 44,000 na Mahakama, baada ya kuzisoma ameandika kitabu kiitwacho:

Altered Genes, Twisted Truth – (How the Venture to Genetically Engineer Our Foods Has Subverted Science, Corrupted Government, and Systematically Deceived the Public).

Na Jeffrey M. Smith, mwandishi wa kitabu cha (Seeds of Deception & Genetic Roulette) kwenye “review” yake ya Altered Genes, Twisted Truth, aliandika hivi:

“Drukers’s brilliant expose catches the promoters of GE food red-handed: falsifying data, corrupting regulators, lying to Congress. He thoroughly demonstrates how distortions and deceptions have been piled one on top of another, year after year, producing a global industry that teeters on a foundation of fraud and denial.”​

Nadharia.
Andiko la Dr. Ally linaendelea kusema:
“Utafiti uliofanywa na watafiti kutoka Shule
Kuu Ya Biashara (UDBS) hapa Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na wadau wengine kama COSTECH (2011), unaonesha kwamba, kama Tanzania ingeanza kulima mahindi ya GMO yanayostahimili ukame na wadudu kuanzia 2016 na miaka sita baadae, basi ingeongeza thamani ya uzalishaji wa zao hilo kwa zaidi ya shilingi za kitanzania trilioni 1.7.”

Ukweli ni Huu.
Utafiti huo si sahihi. Hayo mahindi “yanayostahimili” ukame yamelimwa Afrika ya Kusini kwa muda wa miaka 15, yalisababisha mlipuko wa “super weeds na super bugs” uliofanya kilimo kisiwe na faida na hatimaye kampuni ya Monsanto iliyopeleka hizo mbegu huko, kulipa fidia wakulima wa nchi hiyo kimya kimya. Hivyo basi, matokeo ya hizi tafiti zetu ni za kuzipokea kwa tahadhari kubwa sana.

Jambo la kushangaza ni kwamba kwa mara ya kwanza, Monsanto imejitolea kulipa faida waathirika wake bila kwenda mahakamani. Lakini haishangazi sana; kwa sababu hayo mahindi yenye kuleta hasara Afrika Kusini ndio yaliyosukumiwa Tanzania, Kenya, Uganda na Msumbiji, kwa ahadi ya kutozitoza hizo nchi “royalty”. Sasa kama kungalikuwa na “full-blown court case” juu ya hasara na madhara ya hizo mbegu, hizi nchi zisingeliingia mkenge wa kuzipokea. Marejeo yafanywe kwenye Makala haya: “Failed Monsanto GMO corn Pushed on African Countries with Help of Bill Gates.”

MH. BASHE YUPO SAHIHI, MBEGU ZA GMO ZINAJENGA UTEGEMEZI.

Dr. Ally pia anahoji kauli inayohusu utegemezi ya Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Hussein Bashe, kauli ambayo yamkini haina utata wowote.

Utegemezi unaoongelewa haupo kwenye hizo mbegu zinatoka wapi (nje au ndani ya nchi) utegemezi upo kwenye tabia (characteristic) ya mbegu zenyewe.

Mbegu za asili popote zitakapotoka, ukipanda, mavuno yake unaweza kutumia kama mbegu za kupanda msimu au mwaka unaofuata. Lakini mbegu za GMO popote zitakapotoka, mavuno yake hayawezi kutumiwa kama mbegu, msimu unaokuja – ukipanda mavuno ya GMO hayaoti; ndiyo kusema wakulima wanategemezwa kwa wauza mbegu milele; yaani kunafutwa kujitegemea kwa wakulima. Hilo si suala jepesi.
Utafiti uliofanywa kwa muhula wa miaka 14 wa Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison, uliolenga wakulima wa mahindi wa Wisconsin, Minnesota, Illinois, Iowa na Nebraska ulionyesha kuwa kilimo ambacho siyo cha GMO kina tija zaidi, na ile hali ya kuwa wakulima wasio wa uhandisi jeni hawakulazimika kununua mbegu kila msimu ndio uliofanya faida ipatikane.

Mwaka 2008 Ripoti ya utafiti wa “Organic Agriculture and Food Security in Africa ambayo ilifadhiliwa na United Nations Conference on Trade and Development (UNCTAD) kwa kushirikiana na United Nations Environment Programme (UNEP) ulionyesha kuwa miradi yote ambayo ilihama kutoka kwenye kilimo cha GM na kurudi katika kilimo cha kikaboni “Organic farming” iliongeza mavuno yao. Pia, Ripoti hiyo ilisisitiza kuwa kilimo cha kikaboni (organic) kinaleta lishe (nutrition) bora katika jamii. Hapa napo kutokuwepo kwa utegemezi katika kupata mbegu nako kulichangia kuleta haya matokeo.

Hivyo basi, kauli ya Mh. Bashe kwenye hili, haina dosari, ni kweli tupu.
“Confined field trials” ni kiini macho.

Dhana ya ‘confined field trials’ ni kiini macho, kwani mmea ukishipandwa sehemu ya wazi shambani, hakuna njia ya kuu – “confine” huo mmea; kwa sababu “cross pollination” kupitia upepo, ndege na wadudu haijapata kuwa “confined.”

Na hii “cross pollination” ndio inayofanya uthibiti wa uhakika wa madhara ya kilimo cha GMO ni kukipiga marufuku kabisa, kwani aina hii mbili ya kilimo (GMO and Non-GMO) haviwezi kudumu bega kwa bega – (cannot co-exist).

Mwisho wa andiko lake, Dr. Ally ameandika hivi:
“Hivyo maamuzi haya yanapaswa kufanywa na wataalamu kutoka wizara husika (mfano afya, uvuvi na kilimo) wataalamu hao ndio wanajua zaidi ni wapi wanahitaji nguvu/teknolojia ya ziada (GMOs) kwa maana zile njia za kitaalamu za asili zimeshindwa kutatua changamoto husika.”
  1. Tatizo ni kwamba mara nyingi baadhi ya hao wataalamu ndio wanaowekwa kwenye mifuko ya nyuma ya haya makampuni ya bioteknolojia na kuishia kutoa ushauri ambao haunufaishi umma bali haya makampuni.
  2. Hapo juu nimelezea tafiti zilizoonyesha kuwa kilimo cha asili kina -“out- perform” hicho cha GMO. Mifano mingine ya hii kweli ni hii hapa chini.

“A 2008 United Nations report looked at 114 farming projects in 24 African countries and found that adoption of organic or near-organic practices resulted in yield increases averaging over 100%. In East Africa, a yield increase of 128% was found.”​

Moreover, a 2001 review of 200 developing country agricultural projects involving a switch to agroecological techniques, conducted by University of Essex researchers, found an average of yield gain of 93 per cent.​

HITIMISHO.
Kurejesha kilimo cha uhandisi jeni (GMO) nchini Tanzania ni kuteleza kwa upeo wa juu. Faida nyingi zinazoelezwa za kilimo hiki hazina uhalisia lakini hatari zake zote ni za kweli. Kila walikokijaribu kilimo hiki matokeo yamekuwa si murua – ni vilio: India, Afrika ya Kusini, Burkina Faso, Mexico, United States of America. Na 2018 Burkina Faso imepiga marufuku hiki kilimo kilichokumbatiwa kwa mbwembwe zote 2003.

Watu wanaopigia chapuo kilimo cha uhandisi jeni, wawe ni wanasiasa, watumishi wa serikali (civil servants) au wasomi kwenye vyuo na taasisi mbalimbali -waangaliwe kwa macho mawili: watakuwa aidha hajui wanachokishabikia au wanafanya makusudi. Watatuponza hawa.

Marufuku iliyopitishwa Tanzania tarehe 22/11/2018 dhidi ya kilimo cha uhandisi jeni ni ya kuzingazitiwakwa juhudi zote. Inalinda maslahi mapana ya Tanzania na Watanzania. Ni marufuku ya kishujaa na kizalendo. Idumishwe.

Kufuta hilo katazo, ni kufuta uhuru wetu wa chakula na kuvuruga afya zetu pamoja na za mazingira yetu. Watu waliolambishwa asali hawataweza kuyasema haya ingawa wanayaona.

Hapa chini ni documentary iliyoelezea madhara ya kilimo cha GMO kwa kina:

“Seeds of Death: Unveiling The Lies of GMO’s Full Documentary HD
 
Mkuu all in all tuishi kila mtu na imani yake.
Mimi namuamini Mungu kwa lolote katika maisha yangu.
Tahadhari ni Muhimu sana.
Lakini bila Mungu hatuwezi kumshinda shetani.
 
Mkuu all in all tuishi kila mtu na imani yake.
Mimi namuamini Mungu kwa lolote katika maisha yangu.
Tahadhari ni Muhimu sana.
Lakini bila Mungu hatuwezi kumshinda shetani.
Hakuna imani ya mtu ,Maandiko yanasema IMANI MOJA,MUNGU MMOJA
 
Sio hayo tu, hata kushare uzao wa watu na wanadamu alikataza, ndiomaana mgawanyiko wa rangi na races ukaibuka.

Haya mambo wanajarbu kuficha lkn hayafichiki, walichakachua baadhi ya vitabu kweny biblia kwa kuvificha ili kuficha huu ukweli.

Kitu mnatakiwa kujua ni kuwa, mtu yeyote mweusi hutakiwi kuzaa wala kuoa ama kuolewa na mtu wa jamii za watu weupe wowote wale, na haya maagizo yalipokiukwa ndio haya sasa matatzo tuyapatayo baada ya kuhasi sheria.
 
Hii ni ndefu
Ila nimejifunza kitu hapa. .
Ila hata haya mazao yunayolima kawaida Huwa yanasindikwa na masumu kuua wadudu, na wakati daw haijaisha watu wanapika wanakula mfano mahindi, mchele, kuku wa madawa no. .
 
Sio hayo tu, hata kushare uzao wa watu na wanadamu alikataza, ndiomaana mgawanyiko wa rangi na races ukaibuka.

Haya mambo wanajarbu kuficha lkn hayafichiki, walichakachua baadhi ya vitabu kweny biblia kwa kuvificha ili kuficha huu ukweli.

Kitu mnatakiwa kujua ni kuwa, mtu yeyote mweusi hutakiwi kuzaa wala kuoa ama kuolewa na mtu wa jamii za watu weupe wowote wale, na haya maagizo yalipokiukwa ndio haya sasa matatzo tuyapatayo baada ya kuhasi sheria.
Maandiko yapi yamebadilishwa,yaliyo original yako wap

Mbona biblia niliyonayo Daniel inazungumzia hiyo kuchanganya race
 
Hoja mfu...

Elewa GMO maana yake tu haitoshi... una takiwa kujua zaidi kinacho fanyika ktk GMO na kwa lengo gani?

Mimi narejea mara kwa mara tufanye tafiti, ata wewe ndg mtaalamu na wataalamu wengine wa kilimo aina yako na wamaabara nawashauri pamoja na wasomi wa pale sua udsm na vyuo vya kati wafanye tafiti waje na majibu

Hakuna vyuo kuanzia tanzania hadi afrika nzima na raia wake wamefanya tafiti zaidi ya kusoma maandiko na kuamini bila kujua ukweli na undani wa maandiko hayo

Haya makampuno yana wakaribisha mkafanye tafiti huko au wakupe mbegu ufanye tafiti, ukishindwa una karibishwa kwenye maabara zao ukafanye tafiti

Leo una muona mtu mzima hapo kenya ana simama et EU awali ugali hivyo kwanini sisi tule ugali? Angekuja na tafiti mbalimbali zilizo fanyika na kuieleza dunia na wakenya au angefanya yeye mwenyewe

Tafiti nyingi zilizo fanyika zilikuwa potofu hazikuwa halisia... na majopo wa watafiti duniani kupitia taasisi yao wakazifuta zile tafiti

Huyu anasema andiko la biblia... leo naliendele sua na makampuni kibao wana fanya mambo ya kuchanganya mbegu na mimea

Leo tuna kuku chotara, mbuzi, mbwa nk
Tuna mimea chotara kibao na haya sio ya GMO, lakini hili andiko la kuchanganya mbegu hulikuti huko bali utalikuta ktk GMO tu...

GMO walikuja fanya tafiti ya mimea na viumbe hai (wadudu) wanao shambulia mimea

Darasa hili hulipati popote kwa wana sayansi uchwara na wanasiasa uchwara bali kwa kuingia ktk mradi na kujifunza

Tanzania wamepeleka wataalam wamejifunza wameelewa na nchi zilizo ruhusu afrika hii sio wajinga...

Hii tech inayo tumiwa huko tukitumia sisi na wana sayansi wetu tutafika mbali sana maana ina punguza gharama za uzalishaji kwa kiwango kikubwa...

Kwa leo inatosha...
 
Bandiko zuri na halipaswi kupingwa kwa majibu rahisi rahisi,, kuna nguvu kubwa inaonekana kushamiri ili kukubali gmo katika mazao mengi.
Na kwa maeneo mengi kwa Sasa mazao ya kisasa yanashika kasi.
Mfano Ni Hilo tunda la parachichi.

Swali Ni kuwa;

Baada ya modification uhalisia hubaki kuwa sawa na ule wa zao original lenyewe?

Na je endapo mazao haya ya kisasa yatadominate kwa kiwango kikubwa na kuwa ndio lishe inayopatikana sokoni pekee, itakuwa na athari gani kwa walaji?

Kwenye bandika hili nanukuu, "Ukipanda mavuno ya GMO hayaoti,, ndiokusema wakulima wanategemezwa kwa wauza mbegu milele''

Maana yake umeathirika katika lishe na kiuchumi.
 
Acha kutetea ujinga, umelipwa
 
Acha kutetea ujinga, umelipwa
Kama ulicho komenti ni hoja basi una dhihirisha ujinga ulio nao...

Kama una taka kusaidia basi tafuta ufumbuzi wa tatizo nq usiwaachie wazungu huku ukiwa una lalamika na kupinga juhudi zao huku wewe huoneshi juhudi bali juhudi ipo ktk kulalama

Fanya tafiti njoo nazo, kama kuna tafiti weka hapa, kama kuna mwafrika amefanya tafiti basi iweke pia...

Ila kama una pinga kwa kutumia maneno ya hao hao unao wapinga basi utaonekana juha zaidi... na hauta eleweka kama una waelewa au una wapinga na kwa namna gani...

Nasisitiza, tafuta walio fika kwenye hizo GMO plants waulize, na uzuri tanzania wapo walio kwenda ktk nchi mbalimbali ikiwemo brazil...

Na sizani kama kuna waadhiri walio enda bali walio enda ni kutoka serikali kuu na wataalamu kutoka serikali za mitaa...

Kama wapo kutoka vyuoni basi watakuwa wamepata darasa zuri sana na walifanyie kazi kusogea mbele

Pia wengi hawa fahamu kwanini GMO imeanza yani lengo hasa la GMO... sasa ukifahamu lile wazo lilipo toka na kupatikana GMO ndio hapo na sisi tuna weza anzisha tafiti zetu zaidi...

Kaa hapo hapo na mistali ya biblia sijui msahafu... et mbegu mbili? Yani GMO ni mbegu mbili? Kutoka wapi? Zimefanyikaje hizo mbegu mbili ndugu mtafiti??

Njoo na majibu au kagugo uje na majibu ndugu mtafiti...

Kama hujui jambo ni bora kukaa kimya...

Wachina huko wana tengeneza jua bandia na mwezi bandia, wewe utakaa hapo kwenye sofa ohhh kufuru hizi kufuru, huku wenzio wana piga hatua

Wengine wana kimbizana na mvua bandia za kutengeneza kwa ajili ya kilimo, wewe utakujaa hooo dunia imeisha, wana tengeneza kukabiliana na ukame maeneo ya jangwani na kwenye mvua za wasiwasi ili walime chakula kipatikane

Leo wana lima kilimo cha mpunga jangwani kwenye ardhi ambayo ipo kubwa haina bughuza wewe utakuja na habari za freemasons... mara mpunga haufai...

Watu wana jiongeza kuongeza uzalishaji kukidhi mahitaji wewe una baki chakula kimepanda bei, basi nenda shamba kalime chako maana mapoli ni mengi...

Una kaa hapa et una tetea ujinga... hakuna ujinga... tuna takiwa tukimbie tusikae tu hapa hapa tulipo tuna piga kelele alafu hatufanyi kitu....

Tuamke tuanze kupambana kukuza uchumi...
 
Huo utafiti umefanyika wapi? Na kipi kina fanya hiyo mbegu isiote lakini ya GMO iote?

Ebu tupe hiyo sayansi kidogo tafadhari...!
 
Kenya wana upungufu wa mvua na maeneo mengi ni kame... lakini GMO ina enda kufanya kazi zaidi ya 100% una fahamu kwanini? Ndio maswala ya kujiuliza na kuja majibu... na haya yote yapo wazi... na ndio walicho shughulikia mpaka kuipata GMO

Yani kama katika mpera una weka kichipukizi cha mchungwa ili ukiota upate chungwa ktk mpera

Au kile kinacho fanyika pale sua na wale darasa la saba pale krbu na apopo, nenda pale uambiwe jinsi wale darasa la saba ambao wana zalisha miche ya miti ndio wana wafundisha wanafunzi kwa vitendo...

Waliopo sua waje hapa waseme... wanafunzi wala profesa hawana hata kajaruba au tuta... na wengi wana saidiwa kufanyiwa hizo research na hao la saba

Wengi wa wale wakufunzi na wahitimu ndio wengi wao waliopo humu wana piga story tu...

Fika pale katika zile bustani utaelewa ninacho sema

Au nenda kaulize sua kama wana weza kukuuzia miche 200 ya matunda! Watachukua oda yako na kwenda kwa hawa wakulima wenye vibustani na kununua kwao na kukupa hiyo miche...

Yule jamaa aliyewahi kuwa head pale mjengoni anafahamu kilicho tokea alipo enda nunua miche ya matunda....

Na halmashauri moja waliagiza miche kibao hahahahahahaha...

Tufanye tafiti zenye tija, tuqche kulialia
 
GMO inaenda kuzalisha mashoga wakumwaga

Kwa mkulima mdogo, GMOs ni kitanzi. Ni mbegu ambazo, ukishazipanda shambani, utahitaji kutumia pembejeo zingine (yaani dawa za wadudu na mbolea) zilizotengenezwa na kampuni husika. Lakini huwezi kuhifadhi mbegu toka msimu mmoja au mwingine wala kumgawia jirani yako. Baadhi ya mbegu za GMOs, zikishapandwa, huifanya ardhi isikubali mbegu za aina nyingine tena. Hilo ndilo kaburi la GMOs, ambalo sasa linachimbwa hapa nchini.
 
Kama ulicho komenti ni hoja basi una dhihirisha ujinga ulio nao...

Kama una taka kusaidia basi tafuta ufumbuzi wa tatizo nq usiwaachie wazungu huku ukiwa una lalamika na kupinga juhudi zao huku wewe huoneshi juhudi bali juhudi ipo ktk kulalama

Fanya tafiti njoo nazo, kama kuna tafiti weka hapa, kama kuna mwafrika amefanya tafiti basi iweke pia...

Ila kama una pinga kwa kutumia maneno ya hao hao unao wapinga basi utaonekana juha zaidi... na hauta eleweka kama una waelewa au una wapinga na kwa namna gani...

Nasisitiza, tafuta walio fika kwenye hizo GMO plants waulize, na uzuri tanzania wapo walio kwenda ktk nchi mbalimbali ikiwemo brazil...

Na sizani kama kuna waadhiri walio enda bali walio enda ni kutoka serikali kuu na wataalamu kutoka serikali za mitaa...

Kama wapo kutoka vyuoni basi watakuwa wamepata darasa zuri sana na walifanyie kazi kusogea mbele

Pia wengi hawa fahamu kwanini GMO imeanza yani lengo hasa la GMO... sasa ukifahamu lile wazo lilipo toka na kupatikana GMO ndio hapo na sisi tuna weza anzisha tafiti zetu zaidi...

Kaa hapo hapo na mistali ya biblia sijui msahafu... et mbegu mbili? Yani GMO ni mbegu mbili? Kutoka wapi? Zimefanyikaje hizo mbegu mbili ndugu mtafiti??

Njoo na majibu au kagugo uje na majibu ndugu mtafiti...

Kama hujui jambo ni bora kukaa kimya...

Wachina huko wana tengeneza jua bandia na mwezi bandia, wewe utakaa hapo kwenye sofa ohhh kufuru hizi kufuru, huku wenzio wana piga hatua

Wengine wana kimbizana na mvua bandia za kutengeneza kwa ajili ya kilimo, wewe utakujaa hooo dunia imeisha, wana tengeneza kukabiliana na ukame maeneo ya jangwani na kwenye mvua za wasiwasi ili walime chakula kipatikane

Leo wana lima kilimo cha mpunga jangwani kwenye ardhi ambayo ipo kubwa haina bughuza wewe utakuja na habari za freemasons... mara mpunga haufai...

Watu wana jiongeza kuongeza uzalishaji kukidhi mahitaji wewe una baki chakula kimepanda bei, basi nenda shamba kalime chako maana mapoli ni mengi...

Una kaa hapa et una tetea ujinga... hakuna ujinga... tuna takiwa tukimbie tusikae tu hapa hapa tulipo tuna piga kelele alafu hatufanyi kitu....

Tuamke tuanze kupambana kukuza uchumi...
Tayari kampuni ya Monsanto, kwa kutumia taasisi za serikali kama Tume ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH) inazalisha mbegu zijulikanazo kama WEMA (Water Efficient Maize), ambazo zipo katika hatua ya majaribio. Mbegu hizo hazina wema wowote, ni mbegu za UBAYA. Ni mbegu zenye kitanzi kwa Watanzania. Je, unajua nani yupo nyuma ya Monsanto? Serikali ya Marekani, kwa kutumia shirika lake la misaada la USAID. Lile jambazi la kidijitali, liitwalo Bill Gates, linamiliki hisa laki tano ndani ya Monsanto, na upo uhusiano wa kikazi kati ya Monsanto na AGRA, ambayo ni taasisi ya Bill Gates (na Rockefeller Foundation). AGRA imeanzishwa mahsusi kwa ajili ya kupigia chapuo GMOs, na serikali ya Tanzania imeshalegeza masharti yaliyokuwa yakizibana kampuni za GMOs ili kuruhusu mbegu hizo zitumike nchini.

Kwa hiyo, usione vijisenti vya Bill Gates hapa nchini ukadhadhani eti “ana roho nzuri” au “anatupenda sisi maskini”. Hapana. Kwa kila dola moja inayoingia Afrika kama msaada, au mtaji, mabepari wa nje huvuna dola mbili za ziada. Halafu, Bill Gates mwenyewe alishasema kuwa sisi Waafrika tunazaliana kwa wingi kama wanyama, na amedhamiria kutupunguza. Unadhani anatupunguzaje kama sio kwa kutuchimbia kaburi? GMOs ni kaburi moja wapo. Jingine ni chanjo anazotoa ambazo zimeonyesha kabisa zinaathiri mfumo wa uzazi na kupunguza uwezo wa watu kuzaliana. Huko India, watoto wapatao 50,000 waliopigwa chanjo hizo wamepooza! Chanjo za kifo.
 
Huo utafiti umefanyika wapi? Na kipi kina fanya hiyo mbegu isiote lakini ya GMO iote?

Ebu tupe hiyo sayansi kidogo tafadhari...!
Kwa mkulima mdogo, GMOs ni kitanzi. Ni mbegu ambazo, ukishazipanda shambani, utahitaji kutumia pembejeo zingine (yaani dawa za wadudu na mbolea) zilizotengenezwa na kampuni husika. Lakini huwezi kuhifadhi mbegu toka msimu mmoja au mwingine wala kumgawia jirani yako. Baadhi ya mbegu za GMOs, zikishapandwa, huifanya ardhi isikubali mbegu za aina nyingine tena. Hilo ndilo kaburi la GMOs, ambalo sasa linachimbwa hapa nchini.
 
Huo utafiti umefanyika wapi? Na kipi kina fanya hiyo mbegu isiote lakini ya GMO iote?

Ebu tupe hiyo sayansi kidogo tafadhari...!
Miradi ya kampuni nyingi hujikita zaidi kwa manufaa binafsi,, Kwa kuwa hii Ni science endapo ikitumika "Terminator Gene technology " inayoweza kuonyesha matokeo labda baada ya mfano miaka 20, Hilo linawezekana.
 
Hoja mfu...

Elewa GMO maana yake tu haitoshi... una takiwa kujua zaidi kinacho fanyika ktk GMO na kwa lengo gani?

Mimi narejea mara kwa mara tufanye tafiti, ata wewe ndg mtaalamu na wataalamu wengine wa kilimo aina yako na wamaabara nawashauri pamoja na wasomi wa pale sua udsm na vyuo vya kati wafanye tafiti waje na majibu

Hakuna vyuo kuanzia tanzania hadi afrika nzima na raia wake wamefanya tafiti zaidi ya kusoma maandiko na kuamini bila kujua ukweli na undani wa maandiko hayo

Haya makampuno yana wakaribisha mkafanye tafiti huko au wakupe mbegu ufanye tafiti, ukishindwa una karibishwa kwenye maabara zao ukafanye tafiti

Leo una muona mtu mzima hapo kenya ana simama et EU awali ugali hivyo kwanini sisi tule ugali? Angekuja na tafiti mbalimbali zilizo fanyika na kuieleza dunia na wakenya au angefanya yeye mwenyewe

Tafiti nyingi zilizo fanyika zilikuwa potofu hazikuwa halisia... na majopo wa watafiti duniani kupitia taasisi yao wakazifuta zile tafiti

Huyu anasema andiko la biblia... leo naliendele sua na makampuni kibao wana fanya mambo ya kuchanganya mbegu na mimea

Leo tuna kuku chotara, mbuzi, mbwa nk
Tuna mimea chotara kibao na haya sio ya GMO, lakini hili andiko la kuchanganya mbegu hulikuti huko bali utalikuta ktk GMO tu...

GMO walikuja fanya tafiti ya mimea na viumbe hai (wadudu) wanao shambulia mimea

Darasa hili hulipati popote kwa wana sayansi uchwara na wanasiasa uchwara bali kwa kuingia ktk mradi na kujifunza

Tanzania wamepeleka wataalam wamejifunza wameelewa na nchi zilizo ruhusu afrika hii sio wajinga...

Hii tech inayo tumiwa huko tukitumia sisi na wana sayansi wetu tutafika mbali sana maana ina punguza gharama za uzalishaji kwa kiwango kikubwa...

Kwa leo inatosha...
Gmo ni sumu acheni uchawa
 
Back
Top Bottom