Sabodo: Kikwete ni kiongozi anayecheka na rushwa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Sabodo: Kikwete ni kiongozi anayecheka na rushwa!

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Rutashubanyuma, Feb 8, 2011.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Sabodo amchambua Kikwete

  • Asema ni kiongozi anayecheka na rushwa

  na Waandishi wetu

  MFANYABIASHA maarufu na Kada wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mustafa Sabodo, amesema tatizo la rushwa limezidi kushamiri nchini katika zama hizi kutokana na upole wa Rais Jakaya Kikwete.

  Sabodo ambaye amejipambanua kama mdau mkubwa wa harakati za kimaendeleo, alisema kwa hilo, ni rahisi kumlaumu Rais Jakaya Kikwete kwani wanaomponza ni watendaji wake.

  Aliyasema hayo jana nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam wakati wa hafla ya kuzawadiwa na wanafunzi wa Shule ya Michezo ya Tanzania Sports Catalyst TASCA) iliyopo Kigamboni, kutokana na mchango wake kwa shule hiyo.

  Alisema watendaji wa Kikwete hawaonyeshi dhamira ya dhati kuichukia rushwa kama ilivyo kwa Rais huyo.

  Sabodo ambaye katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010, alikipa Chama cha Demokrasi na Maendeleo jumla ya sh mil. 200, alisema ingawa rushwa ilikuwepo hata katika Awamu ya Kwanza ya Hayati Mwalimu Julius K. Nyerere, lakini si kama ilivyo hivi sasa.

  Alisema, hali hiyo ilitokana na ukali wa mwasisi huyo wa Taifa la Tanzania ambaye katika utawala wake, alipigania haki, usawa na utu.

  "Kwa sasa hali imekuwa mbaya sana, yote hii inachangiwa na upole alionao Kikwete, hivyo hata watendaji wa juu sio wakali na hawapo tayari kuichukia rushwa na kuepukana nayo," alisema.

  Akisisitiza kile anachokiamini, Sabodo ameonyesha kusikitishwa na adhabu ya faini ya sh 700,000 kwa aliyekuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Andrew Chenge, iliyotokana na kesi ya tuhuma za mauaji ya watu watu wawili.

  Sabodo alikwenda mbali zaidi na kusema upole wa JK pia umekuwa ukilalamikiwa na wananchi ambao wamekuwa wakimwona kama anawalea mafisadi.

  "Kuna kipindi nilikwenda Rombo, kukabidhi moja ya shule nilizojenga, lakini nilishangazwa na Rais Kikwete kumnadi hadharani Basil Mramba anayekabiliwa na kesi ya ufisadi.

  "Watu wamekuwa wakimlalamikia JK kuwa anawakumbatia mafisadi na hata Mramba pia, lakini yeye alimnadi hadharani huku akijua bado ana kesi inayomkabili!" alisema.

  Kwa upande mwingine, Sabodo aliunga mkono pendekezo la Katiba mpya na kupendekeza ziwe tatu; yaani ya Tanganyika, Zanzibar na Tanzania.

  Katika hatua nyingine, Sabodo aliwasisitiza wanafunzi hao kuzingatia elimu kwani maendeleo ya nchi yanawategemea wao, kinyume na hapo watashindwa kutimiza ndoto zao.

  Naye Mhadhiri Mwandamizi Profesa Mwesiga Baregu amesema Rais Jakaya Kikwete anapaswa kuwaomba radhi Watanzania kutokana na viongozi wa serikali yake kutoa kauli za kuwachanganya Watanzania kuhusiana na suala la Dowans.

  Akizungumza na Tanzania Daima kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam, Profesa Baregu, alisema kuwa matamko mbalimbali juu ya suala hilo yaliyokuwa yakitolewa na serikali yameonyesha ni kwa kiasi gani viongozi hao wamekosa nidhamu kwa umma.

  Alisema kauli hizo zimewagonganisha Watanzania, hivyo ni wakati muafaka kwa Rais Kikwete kusimama na kuomba radhi kwa umma juu ya suala hilo.

  Alisema haoni umuhimu wa suala hilo kwenda kujadiliwa na Kamati Kuu ya Chama cha Mapinduzi (CCM) kwa kuwa linaihusu nchi nzima na si chama hicho pekee.

  "Inawezekana Rais Kikwete anataka kuueleza umma kuwa suala hilo alinamhusu yeye au ni mzigo wa chama chake ndiyo maana akalipeleka huko; au anafikiria bado yuko kwenye uchaguzi akiamini ni jambo la utekelezaji wa ilani ya CCM," alieleza Profesa Baregu.

  Alisema hata hivyo tamko hilo halijajitosheleza hivyo ni muhimu akalifafanua kwa uwazi kuliko kutumia maneno yanayohitaji ufafanuzi mpana.

  Naye Katibu Mkuu wa Chama cha Wafanyakazi wa Shughuli za Meli na Bandari (DOWUTA), Abdallaha Kibunda, alipongeza hatua ya Kikwete kutegua kitendawili kuhusu suala la kampuni ya Dowans ingawa amechelewa.

  Alisema kimya chake cha muda mrefu kuhusu sakata hilo ndicho kilichowafanya watu wengi kuzungumza mambo mengi juu yake na Dowans.

  "Maelezo aliyoyatoa Kikwete yalikuwa yakisubiriwa kwa muda mrefu na alitakiwa kuyatoa kabla watu hawajamchafua kwa suala hilo na hiyo ingesaidia kushusha imani ya watu kwake lakini badala yake alikaa kimya kwa muda mrefu," alisema Kibunda.

  Alimshauri kutoyachelewesha mambo yanayoshusha hadhi yake kwani kufanya hivyo kunajenga dhana mbaya.

  "Anapokaa muda mrefu bila kushughulikia tatizo mwisho wake huwa mbaya kwani hata utakapokuja kutatua tatizo hilo baadaye unakuwa umejenga maswali mengi," alisema Kibunda.

  Naye Mwenyekiti wa Taasisi ya Masuala ya Haki za Binadamu na (Aford), Julius Miselya, alisema kauli ya Kikwete si ya ukweli kutokana na kuwepo kwa mitazamo tofauti ndani ya serikali yake.

  Alisema kuwa kauli tata zilizotolewa na viongozi hao ni za kutaka kuwachanganya Watanzania hivyo hakuna ukweli unaoweza kuonekana juu ya kutaka kulipwa au kutolipwa kwa kampuni hiyo.

  Alisema kutokana na kushindwa kuwa wazi juu ya kampuni hiyo ni wakati muafaka kwake kujiuzulu nafasi hiyo ili kuepuka kuendelea kuudanganya umma.

  "Kumekuwa na kauli za kutofautiana hata katika hiyo Kamati Kuu; hakika kama ililijadili lile alilolisema Rais Kikwete maana haiwezekani Waziri wa Nishati na Madini asimamie kulipwa halafu wadai katika kikao hicho walipinga malipo hayo," alisema.
   
 2. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #2
  Feb 8, 2011
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 158,345
  Likes Received: 418,748
  Trophy Points: 280
  Huu siyo upole wa JK kama Sabodo anavyodai bali JK ameukumbatia ufisadi ....sote tukilitambua hilo safari imeanza ya kuuthibiti ufisadi....
   
 3. mundo

  mundo JF-Expert Member

  #3
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 200
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Mzee mzima hakumaanisha upole kama upole..ametumia lugha laini tu, kwa jinsi alivyoongelea suala la mramba ni kwamba ameshindwa kazi!
   
 4. N

  Ndinani JF-Expert Member

  #4
  Feb 8, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 5,413
  Likes Received: 734
  Trophy Points: 280
  Sabodo ni kweli anatumia lugha laini[ diplomatic language] kumuongelea Kikwete lakini anajua fika kuwa jamaa ni fisadi nambari one!!
   
 5. anti-fisadi

  anti-fisadi JF-Expert Member

  #5
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 369
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Mimi naona watu wanaocheka na rushwa ni wale wanaonufaika nayo moja kwa moja. Sio jambo la kuficha, ndio maana ubabaishaji wa hoja unaendelezwa na viongozi wakuu wa nchi hii.

  Tujiulize kwanini baraza la mawaziri halikai ili litoe tamko moja kuhusiana na hili?

  wizi mtupu huu, na hili ndilo linamkandamiza mwananchi wa hali ya chini.
   
 6. Somoche

  Somoche JF-Expert Member

  #6
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 3,827
  Likes Received: 929
  Trophy Points: 280
  Hivi ni upole ama uwezo mdogo?!! hawezi kuongoza na ni muoga sasa eti mnasema ni mpole,utaongeleaje suala zito kama la Dowans huku unacheka!! duh hii ipo hapa tz tu
   
 7. Bujibuji

  Bujibuji JF-Expert Member

  #7
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 4, 2009
  Messages: 35,330
  Likes Received: 22,172
  Trophy Points: 280
  JK= Jinga Kabisa
   
 8. MartinDavid

  MartinDavid JF-Expert Member

  #8
  Feb 8, 2011
  Joined: May 22, 2009
  Messages: 876
  Likes Received: 46
  Trophy Points: 45
  Siyo upole bali yeye ni fisadi sasa kuwaonya wenzake mafisadi ambao kwa kutumia mtandao ndani ya ccm walimwingiza madarakani lazima awalinde..

  Jk hakuwa chaguo sahihi la watanzania na nadhani sasa wengi wanajuta kwa hilo...
   
 9. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #9
  Feb 8, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Sabodo anamwambia Kikwete apambane na rushwa wakati kikwete ndio mfalme wa madisadi na anawalinda, tangu lini mwizi akajifunga mwenyewe jela. :twitch:
   
 10. Mallaba

  Mallaba JF-Expert Member

  #10
  Feb 8, 2011
  Joined: Jan 30, 2008
  Messages: 2,560
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 133
  yaani kweli tu raisi..
   
 11. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #11
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280
  welln said mzee na mwanamapinduzi wetu saibodo
   
 12. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #12
  Feb 8, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  sio kaukumbatia mkuu bali UWEZO WA JK MDOGO SAANA!
   
 13. RealMan

  RealMan JF-Expert Member

  #13
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 9, 2010
  Messages: 2,352
  Likes Received: 160
  Trophy Points: 160
  Sijui ni tajiri gani mwingine anayeweza kuikoromea serikali kama anavyofanya Sabodo.
  Huyu mzee inaonekana anaendesha biashara halali na kulipa kodi maana kwa sisiem tunayoijua, wangesha mkamua siku nyingi ama wanamvutia pumzi.

  Waziri mkuu mmoja aliwahi kuwaambia wafanyabiashara wajiunge na ccm ili mambo yao yawanyookee.

  Hata kama Sabodo umeamua kutumia lugha ya kidiplomasia bado ujumbe wako umeeleweka.
   
 14. M

  Mchekechoni JF-Expert Member

  #14
  Feb 8, 2011
  Joined: Apr 24, 2008
  Messages: 280
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  JK= Janga Kuu (kitaifa)
   
 15. U

  Utatu JF-Expert Member

  #15
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 31, 2008
  Messages: 436
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 60
  Wakuu,

  Kwa maana halisi ya neno UHAINI. Huyu Rostam Aziz, na JK ni wahaini. Ni sisi tu kutafuta njia ya kuwawajibisha.
   
 16. E

  Elifasi Senior Member

  #16
  Feb 8, 2011
  Joined: Nov 1, 2010
  Messages: 180
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ngumu sana kujipeleka kituo cha polisi kujishtaki...
   
 17. Elia

  Elia JF-Expert Member

  #17
  Feb 8, 2011
  Joined: Dec 30, 2009
  Messages: 3,442
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 135
  Ni uwezo mdogo, Tatizo mtu aliyetakiwa kuwa mchungaji/shehe anakua Askari, aliyetakiwa kuwa jambazi ana kuwa shehe/mchungaji, mchumi-mwanasheria, dereva-konda, polisi-mwinjilisti, mgambo-secretary, mwizi-polisi, mkuu wa wilaya-raisi. Kunakitu hapo? ahsante sabodo ujumbe umefika kwa mwenye upeo amekuelewa..
   
 18. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #18
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Anajua anachofanya wala sio mpole wala nini
   
 19. The Finest

  The Finest JF-Expert Member

  #19
  Feb 8, 2011
  Joined: Jul 14, 2010
  Messages: 21,709
  Likes Received: 43
  Trophy Points: 145
  Hahaha!! Labda kama umelogwa
   
 20. IGWE

  IGWE JF-Expert Member

  #20
  Feb 8, 2011
  Joined: Feb 3, 2011
  Messages: 7,752
  Likes Received: 1,326
  Trophy Points: 280

  basi tumloge kama itasaidia wakuu au mnasemaje
   
Loading...