Elections 2010 Sabodo aichangia CHADEMA Milioni 100 (tena)

kwa sasa chadema kinahitaji fedha za kutosha mawakala wakati wa kupiga kura tuwe wazalendo tusiwakatishe tamaa wanaojitokeza kuchangia vyama vinavyoonyesha kukomboa nchi yetu.:peace:
 
Other business people don't dare to do what Sabodo does because of ther dubious financial dealings, that is why they give to CCM without disclosing themselves to the public. Ukiwa unafanya vitu haramu the great likelihood ni kwamba utaenda CCM maana hiyo ndo save heaven. I pray from the bottom of my heart to God to enlighten Tanzanians to discern the evil of the current ruling party so that on 31/10/2010 we install the leadership adhering to norms of good conduct as far as the running of the country is concerned.
 
Fidelis Butahe na Hussein Issa
CHADEMA imeongezewa nguvu tena katika wiki ya mwisho ya kampeni baada ya kada wa CCM, Mustafa Sabodo kuichangia tena Sh100 milioni, huku akidai kuwa chama hicho tawala kimepoteza mwelekeo wa kisiasa.
Sabodo, ambaye ni mfanyabiashara maarufu, alitoa tena kiasi kama hicho cha fedha Julai 12 mwaka huu kabla ya kuanza kwa kampeni za uchaguzi na kuahidi kuwa atakuwa tayari kukichangia fedha chama hicho wakati mwingine wowote.
Ikiwa imebakia wiki moja kabla ya kumalizika kwa muda wa kampeni, Sabodo alitimiza ahadi hiyo ya kuendelea kuisaidia Chadema akisema kuwa lengo lake ni kutoa changamoto kwa chama tawala ambacho kimekuwa madarakani tangu mwaka 1961 wakati nchi ilipopata uhuru.
“Upinzani sio uadui na serikali haiwezi kufanya vizuri bila kuwepo kwa vyama vya upinzani kwa sababu vinatoa changamoto mbalimbali bila ya upinzani ufisadi utaendelea,” alisema Sabodo.
Mmiliki huyo wa ukumbi wa kisasa wa sinema unaojulikana kama New World Cinema, aliweka bayana mtazamo wake hasi dhidi ya CCM
“Mimi ni kada wa CCM, lakini naona kama siku hizi CCM inapoteza mwelekeo; sio kama naiunga mkono Chadema wala nataka kuhamia Chadema. Mimi ni kada wa CCM, napenda jinsi chama hiki kinavyotoa changamoto kwa serikali. Hii ni sawa, serikali inakuwa kama inakumbushwa, wapinzani ni watu muhimu,” alisema muumini huyo wa falsafa za kiongozi wa kwanza wa taifa la Tanzania, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.
Hata hivyo, Sabodo alisema kuwa nafasi ya Chadema pamoja na vyama vingine vya upinzani kuibuka na ushindi wa kiti cha urais ni ndogo, lakini alisisitiza kuwa uwepo wa vyama hivyo ni changamoto tosha kwa serikali.
“Napenda sana mnavyotoa changamoto zenu," alisema Sabodo. "Nafasi yenu ya kushinda urais ni ndogo, nyinyi pamoja na vyama vingine vya upinzani lakini uwepo wenu unaleta ushindani na kuiweka serikali sawasawa," alisema Sabodo,
Aliongeza kusema: “Mimi huwa natoa fedha kwa chama hiki, na hii si mara ya kwanza na hiyo haimaanishi kama niko upinzani, bali naangalia chama kinachofanya vizuri kisiasa.”
Mchango huo ambao ulikabidhiwa kwa mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, ni sehemu ya jitihada mpya kutoka kwa wadau wa siasa kuviwezesha vyama vya upinzani ambavyo vimekuwa vikisumbuliwa na ukata kutokana na kutokuwa na vyanzo vya uhakika wa fedha.
Vyama vingi vinategemea fedha zinazotolewa kwa hisani na viongozi au wanachama wake kutokana na ruzuku vinavyopata kutoka serikali kuwa ndogo. Ruzuku hutokana na kiasi cha wabunge wanaoingia bungeni na kutopata kura za kutosha kwenye kinyang'anyiro cha urais.
Lakini CCM imekuwa ikifaidi ruzuku kutokana na kufanya vizuri kwenye uchaguzi huku wafanyabiashara wakitoa misaada mikubwa ya hali na mali kwa chama hicho tawala.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Mbowe alipongeza kitendo cha Sabodo kutoa msaada huo wa fedha kwa Chadema na kuwataka wafanyabiashara maarufu kutosita kuvichangia vyama vya upinzani.
"Wengi wanahisi kuwa wakichangia upinzani wataonekana kama wanakisaliti chama tawala, wanachotakiwa kuiga ni hiki anachokifanya Sabodo," alisema Mbowe.

Mbowe, ambaye pia ni mfanyabiashara na kwa sasa anagombea ubunge wa Jimbo la Hai, alisema fedha hizo zitakisaidia chama hicho kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu.
"Hizi fedha zitatusaidia sana hasa kwa wagombea wetu wa nafasi mbalimbali... kwa kweli tunashukuru sana kwa mchango huu; tunashukuru sana," alisema Mbowe ambaye mwaka 2005 aligombea urais.
Mbowe alisema Sabodo ni kielelezo cha mfanyabiashara safi na mfano wa kuigwa kwa wafanyabiashara wengine kwani amekuwa mstari wa mbele kusaidia watu bila kujali itikadi zao.

Mbali na kutoa fedha hizo, Sabodo pia alitoa dola 20,000 za Kimarekeni kwa ajili ya kuwasaidia watoto wadogo 10 wanapelekwa na Lions Club nchini India kutibiwa maradhi ya moyo. Chadema imeichangia klabu hiyo Sh10 milioni.
“Watu wajitokeze kuchangia hasa watu wenye matatizo kama hawa watoto,” alisema Sabodo.
Mwenyekiti wa Lions Club, Frank Goyayi alisema kuwa watoto hao waliotarajiwa kuondoka jana alasiri watapatiwa matibabu ya moyo katika Hospitali ya Fortis Escortis iliyopo New Delhi

SOURCE: Mwananchi
 
MFANYABIASHARA maarufu nchini na kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mustapha Jaffar Sabodo, kwa mara nyingine amejitokeza hadharani kukichangia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), kiasi cha sh mil. 100.
Sabodo amesema fedha hizo zitasaidia harakati za upinzani nchini kuwakomboa Watanzania na kuimarisha demokrasia, hasa katika wakati huu wa mfumo wa vyama vingi.
Hii ni mara ya pili kwa kada huyo wa CCM kutoa kiasi hicho, ambapo Julai 12, mwaka huu aliichangia CHADEMA ili iweze kushiriki kikamilifu katika kampeni na hatimaye Uchaguzi Mkuu.
Sabodo alikabidhi hundi ya sh mil. 100 jana nyumbani kwake Upanga, jijini Dar es Salaam kwa Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliyeambatana na viongozi wa kitaifa, akiwamo mbunge wa Viti Maalumu anayemaliza muda wake, Suzan Lyimo na Mkurugenzi wa Fedha na Utawala, Anthony Komu.
Akikabidhi hundi hiyo, Sabodo alisema licha ya kuwa mwanachama wa siku nyingi wa CCM angependa kuona upinzani na demokrasia ya kweli inaimarika nchini huku akisisitiza kuwa CHADEMA ni chama makini ambacho kitawakomboa Watanzania.
Sabodo ni mmoja wa wazee wanaoheshimika katika jamii kutokana kutokuwa na misimamo ya kuyumbishwa, ambapo mara kadhaa amekuwa akiikosoa serikali pindi anapoona mambo hayaendi kama inavyotakiwa.
Mfanyabiashara huyo amekuwa akiikosoa serikali kwa kukiuka misingi ya utawala bora, iliyojengwa na mwasisi wa taifa hili, hayati Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere.
“Mimi ni mwanachama wa CCM, lakini napenda kuona demokrasia inakua, huku kambi ya upinzani ikiimarika na kuwa na wabunge wengi bungeni ili kushamirisha maendeleo nchini.
“Leo ninawachangia CHADEMA kwa mara ya pili na ninatambua umakini wenu katika siasa za hapa nchini na hasa bungeni.
“Nitaendelea kuwa mwanachma halisi wa CCM na nitaendelea kukiunga mkono, lakini bila upinzani kama CHADEMA, CCM italala na haiwezi kuwa makini,” alisema Sabodo.


source: Tanzania Daima.




:A S 39:Wadau mnaionaje hii??
 
Sidhani kama ina matatizo yoyote. Nampongeza kwa ujasiri wake wa kujitokeza hadharani na kuchangia opposition. Wapo matajiri wengi sana ambao wanatamani kuchangia lakini hawana ujasiri wa kufanya hivyo kwa hofu ya chama dola
 
Mkuu ni jambo la hekima kufikirika. Ni matumaini makubwa kwa nchi maskini kama Tanzania kuona kuna watu waliokomaa kimaadili na kidemokrasia. Mh.Sabodo ni mfano wa kuigwa pia watanzania wengine wanapaswa kulitazama jambo ili kwa upana,tukiacha ushabiki pembeni tukawa na uzalendo nchi hii itaongozwa kwa maadili. Mkuu,ni aibu kuona wafanyabiashara wengine tena wakubwa wanafanya NJAMA za kuua upinzani kwa kuhusishwa na mambo ya kidikteta kama kusafirisha nyaraka za nchi kuua upinzani. Kuna mifano miovu mingi mno ambapo wafanyabiashara wakubwa ama kwa njia moja au nyingine wanatumika au wanatumia magari yao kubeba nyaraka za kuudhofisha upinzani kisha wanalindwa kwa kuharibu ushaidi,ni aibu muno. Mkuu naomba wanajamii tuige mfano tuache ushabiki wa kisiasa. Sabodo,haijalishi umetumwa na nani,haijalishi kama wewe ni mamluki,daima ntakuona kama mwanga wa kidemokrasia. Chadema itumie ela iyo kuweka mawakala wahaminifu,wasioongeka! Mungu ibariki Tanzania,Mungu mpe huyu Kada wa Ccm maisha marefu. Najua ana mengi ya kusema ila anashindwa ndo anaishia kuonesha kwa vitendo,baada ya jumapili ijayo atauona ukombozi wa nchi na pesa yake itaenda kihalali. Mola tunaomba utujalie uhuru mpya wa Tanzania jumapili ijayo 31.10.2010. Tupo pamoja,tudumishe amani na utulivu. Dr.SLAA ANAWEZA.
 
actually hii habari na mimi ilinccmua nlipoisoma mara ya kwanza...natamani sana viongozi wote wawe na moyo kama huu kwani naamini kuna viongozi wengi wazuri tu ila wapo katika njia isiyo yao(wrong track)..na naamini ipo siku!! kwa swala hili wasiwasi wangu ulikuwa juu ya hiki chama cha dola kitachukuliaje swala hili...sababu najua mammbo yao..si ajabu kesho tu tukasikia jamaa kafanyaje sijui...mara ooooh!! But all in all..God Bless Tanzania..God Bless CHADEMA!
 
hizo pesa ziende zikasaidie wagombea ubunge basi... so tunafurahia hafu zinakoishia hatujui. wagombea hawajapewa sapoti kabisa.

Jamani mumkumbuke na GENDER SENSITIVE kumpelekea hizo pesa kidogo; anapigana vita kali kweli huko Kilombero na muungwana amepitia huko wiki iliyopita!! Mpigeni tafu na sadaka ya SABODO!
 
NAomba wajuzi wanijuze..

Hivi hizi sheria mpya za matumizi ya fedha katika kampeni zinasemaji kuhusu kiasi cha fedha ambazo mtu mmoja anaweza kuchangia? Milioni 100 haijazidi kiwango?

Kumbukeni huyu Mzee Sobodo ndio aliungana na kina Makamba kuwatukana Mwalimu Nyerere Foundation mara baada ya ule mjadala wa Karimjee ambao baada ya kupata ukweli JK akafikia kuwatukana wasaidizi wake kwa kumdanganya.....
 
Kumbukeni huyu Mzee Sobodo ndio aliungana na kina Makamba kuwatukana Mwalimu Nyerere Foundation mara baada ya ule mjadala wa Karimjee ambao baada ya kupata ukweli JK akafikia kuwatukana wasaidizi wake kwa kumdanganya.....[/SIZE]

Oooh! Kwa hiyo ali-react kabla ya kupata ukweli wote!!
 
NAomba wajuzi wanijuze..

Hivi hizi sheria mpya za matumizi ya fedha katika kampeni zinasemaji kuhusu kiasi cha fedha ambazo mtu mmoja anaweza kuchangia? Milioni 100 haijazidi kiwango?

Kumbukeni huyu Mzee Sobodo ndio aliungana na kina Makamba kuwatukana Mwalimu Nyerere Foundation mara baada ya ule mjadala wa Karimjee ambao baada ya kupata ukweli JK akafikia kuwatukana wasaidizi wake kwa kumdanganya.....

Dogo punguza spinning!!!!!!!!!!!
 
Gabachori anapokuwa mzalendo... hapo ndipo utaipenda chadema na unafiki wao!
Wahindi wengi wamekuwa wakiendeleza mbinu za kifisadi serikalini mwetu kupitia ccm ambayo inawakumbatia. Mtu kama Sabodo anageuza mtazamo huo kuwa si Wahindi wote ambao si Wazalendo.
 
Back
Top Bottom