Sabodo afukuzwe uanachama CCM - Mashishanga

Sabodo afukuzwe uanachama CCM - Mashishanga

Kumfukuza uanachama ndo watamkomoa? Labda kwa hila zao, wawaagize TRA kuingilia biashara zake, la sivyo ndo kwanza watakuwa wameongeza mafuta kwenye utambi. Wataisha tu.

Wanachotakiwa kujihoji, kwa nini hata makada wao wa siku nyingi wamewachoka na kuonesha waziwazi?

Huyu jamaa ni international bussinessman si kwamba amewekeza bongo kihivyo hivyo bringing him down is not easy amerudi bongo baada ya kuzeeka ndo akaona arudi nyumbani kwao kupumzika hawamuwezi kabisa hawa mbwa wenye njaa kali.....
 
mwendelezo wa siasa za chuki!mashishanga mwenyewe alisema anamuunga mkono sumaye kwenye kura za maon za urais(2005) jk akamtosa.lakin pia mashishanga mwanae wa damu ni chadema atangaze basi kua yule c mwanae!nadhan sabodo hafurahshwi na mambo ya chama chake
unajua mzee aliwekwa kabatini na jk sasa anarudi vipi hiyo ni nitoke vipi, sasa anataka toke kisabodosabodo, wamwache mzee wa watu sadaka unatoa sehemu unayo amini mungu yupo sasa kama kahama ccm mwache atoe yule ni mtu mzima.
 
Kwani nani amemdanganya Mashishanga kuwa Sabodo ni mwanachama wa CCM? Utamfukuzaje uanachama mtu ambaye sio mwanachama? Nadhani hawa wazee wa CCM wanazeeka vibaya!
 
tehe tehe tehe mashishanga unataka ukuu wa mkoa tena hutakiwi baba kampumzike na gamba lako
 
Loo huyu mzee anazeeka vibaya.Je yeye ni msafi kuwanyoshea vidole wenzake.
Ji ni upya hupo CCM anayesifia mazuri au anayekemea mabaya.?
 
Mbona mabere marando ni mjumbe wa kamati kuu ya chadema lakini ndie wakili wa majambazi ya pesa za EPA.siasa ndivyo ilivyo so mzee kazeeka vibaya.
 
Katika mshangao mkubwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kada maarufu wa CCM stephen Mashishanga amekitaka chama cha mapinduzi kumfukuza mara moja kada wa chama hicho Mustapha Sabodo kwa kile aklichodai ni usaliti wa waziwazi kwa chama hicho tawala.

Mashishanga amedai maneno aliyotamka alipokuwa na Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ni usaliti mkubwa kwa CCM. Mashishanga hajafurahishwa na kauli ya Sabodo alipomwambia Dr Slaa anatamani CCM ishindwe uchaguzi wa 2015 na akaahidi kumchangia mgombea urais wa Chadema shilingi milioni 500.

SOURCE: MTANZANIA.

Mashishanga atakuja kugundua kila mtu ni msaliti wa CCM coz watu wote watafanya na kunena ukweli dhidi ya CCM.Masishanga amewai kumsikiliza Dr Rwaitama anavyosema kuhusu CCM??
 
Sishangai kuskia kauli kama hii toka kwa magamba, maana huwa wakali sana wanapoambiwa ukweli, maskini mzee wa watu sijui kama watamuacha salama... huyu mzee kweli alikuwa rafiki wa mwalimu, ana uchungu sana na nchi hii, yani ukimsikiliza au kusoma yale anayoyaandika, kweli utakubaliana na ayasemayo. Anapata uchungu sana kuona mafisadi wanavyoitafuna nchi mchana kweupeee na nchi inazidi kudidimia kadri siku zinavyoenda.
 
Hivi wewe unamfahamu mzee Sabodo? Huyu mzee hana shida ya vyeo, ni bilionnaire kati ya mabilionnare. Huyu mzee ana investiment na pesa zke zimetapaaka katika nchi nyingi kama Canada, Singapore, Uingereza n.k. na pia sio fisadi.

Mkuu ID yako tu imenikosha,turudi kwenye mada mimi hapo nilikuwa namzungumzia, huyu babu anayejiita Mashishanga ni kitambo sijamsikia kiasi kwamba nilifikiri hayupo duniani.
 
Mkuu ID yako tu imenikosha,turudi kwenye mada mimi hapo nilikuwa namzungumzia, huyu babu anayejiita Mashishanga ni kitambo sijamsikia kiasi kwamba nilifikiri hayupo duniani.

Ok, nimekuelewa, nadhani miye ndo sikukusoma vizuri. Mashishanga nashangaa sijui kapewa nini na JK, maana alimtosa mara tu alipoingia madarakani.
 
Sebodo anaitegemea serikali ya ccm kw a mengi kuliko serikali ya ccm inavyomtegemea sebodo..unategemea nani ataumia zaidi..sebodo atabalance tu iyo issue iwapo itatokea kufukuzwa ccm/mifano ipo mingi tu..
 
chama cha mafisadi(ccm) wamekwisha hawana jipya Sabodo ana akili mashishanga mjinga hawezi hata kuona chama chake kipo wapi,kwani slaa anapeleka maji kwa mkewe au anasaidia wana igunga wanaokunywa maji pamoja na ngombe kwa sababu ya ccm?unaweza kuwa mtu mzima lakini hoooooovyoooooo!
 
Kwa msioelewa kiswahili cha CCM: Steven Mashishanga anamtuhumu Mustapha Sabodo kukisaliti chama. Badala ya kufuata utaratibu uliowekwa na CCM (wa kuiba mali za umma na kuwakandamiza maskini) yeye ndio kwanza anafanya kinyume chake (anawachimbia wanavijiji visima vya maji safi) bila kutumia akili kuwa:

-Watu wa mashambani wakinywa maji safi hawataugua ugua hovyo
-kama hawaugui manake watapata fursa ya kwenda shule
-kama wakienda shule wataelimika
-na wakielimika hawatachagua CCM tena

Sasa kweli Mustapha Sabodo anaitakia mema CCM?
kweli kabisa mkuu!
 
Mashishanga yupo kundi la fredrick sumaye ktk urais!hivi unaweza mchukia mtu kwa kuchimba kisima cha kusaidia viumbe vya mungu?ccm wauwaji jamani
 
Katika mshangao mkubwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kada maarufu wa CCM stephen Mashishanga amekitaka chama cha mapinduzi kumfukuza mara moja kada wa chama hicho Mustapha Sabodo kwa kile aklichodai ni usaliti wa waziwazi kwa chama hicho tawala.

Mashishanga amedai maneno aliyotamka alipokuwa na Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ni usaliti mkubwa kwa CCM. Mashishanga hajafurahishwa na kauli ya Sabodo alipomwambia Dr Slaa anatamani CCM ishindwe uchaguzi wa 2015 na akaahidi kumchangia mgombea urais wa Chadema shilingi milioni 500.

SOURCE: MTANZANIA.

Huyu naye anaitwa Mzee mwenye busara ndani ya CCM!!:shock: Baba ukiwa na mwanao kisha mwanao akasema kuwa anatamani baba yake afe tu maana hana msaada wowote, baba unatakiwa kujihoji mara saba saba.
Kumfukuza Sabodo uanachama hakuwezi kumnyan'ganya haki yake ya msingi ya kutoa maoni yake kadri aonavyo. Sabodo amechangia mengi katika huduma za kijamii bila kujali itikadi ya vyma. Hata Mwl. Nyerere aliwahi kusema kuwa CCM si mama yake, Mashishanga anaweza kuendelea kubaki na CCM yake lakini hawezi kulazimisha watu kuendelea kukumbatia chama kilichokosa visheni.
 
Big up Sabodo kwa kuwa muwazi inagwa najua wengi wana hamu ya kutamka hayo maneno ila wanaogopa chakula yao ya kila siku itakatwa
Mashishanga mbona wa kuwatimua CCM wanajulikana
 
Ok, nimekuelewa, nadhani miye ndo sikukusoma vizuri. Mashishanga nashangaa sijui kapewa nini na JK, maana alimtosa mara tu alipoingia madarakani.

Alimtosa vipi? Wanaotoswa ni watu ambao wanakuwa wamefanya vitu fulani muhimu. Ukisema kama Mangula alitoswa hapo nitakuelewa. Huyu mashishanga aliachwa tu hakutoswa.

Wanaotoswa ni wale wanakuwa wameonyesha na wamefanya mambo fulani ya kuheshimika kwenye jamii. Mashishanga ni kama kina kapuya tu. Asipchaguliwa wengi hawashangai wala kujiuliza kwa nini kaachwa
 
Back
Top Bottom