Sabodo afukuzwe uanachama CCM - Mashishanga

Mashishanga mwenyewe haeleweki ndani ya CCM na ndiyo maana kapigwa benchi.

Pia gazeti lililoandika hiyo taarifa sina uhakika nalo maana yake MTANZANIA ni la Habari Corporation ambao linawezekana kabisa kuna gilba ya kibiashara zaidi na kimaslahi dhidi ya mmiliki wake na Sabodo.

Hakuna mtu anafungwa mdomo kuongea.
 
From Wikipedia
"Mustafa Jaffer Sabodo was born in Lindi, Tanzania to parents of Indian descent.
He is an
economist, consultant in international debt-finance, philanthropist and a businessman. He has business interests in India, France, Kenya, Sudan and Zimbabwe.

In 2003, he offered to finance the growing of
pulse for export to the tune of TZS 100 million.

The
Mwalimu Nyerere Foundation National Lottery was the brainchild of Sabodo, who donated TZS 800 million towards a project that established the lottery."

Kwa hiyo CCM wakiamua kutumia TRA kumfilisi itabidi wafanye hivyo Kenya, Ufaransa, India, Sudan na Zimbabwe. Pia huyu mzee ndio supplier wa bidhaa kibao Comoro.
Wajuzi wa mambo wanasema huyu babu aliwekeza kwenye dhamana za serikali miaka hiyooo ambayo watz tulikuwa hatujui treasury bills and bonds ni nini. Anakula interest tu kwa sasa!

CCM wanajua ushindi wao unategemea fedha sasa hofu yao ni kwamba kama huyu babu akiamua kumwaga bilioni zake kwa wapinzani muziki utakuwa mnene...
 
Saiv kuna ma group mengi ndani ya CCM, simshangai Masishanga kwakuwa yeye ni CCM-Chumia Tumbo
 
Naomba Mungu mwenye madaraka ya kumfukuza Sabodo afanye fasta. Cjui anapendelea kunywa bar ipi ili nkimkuta nimtandike John walker green label ili kufacilitate uböngo wake utoe maamuzi ya kumfukuza sabodo mapema kabla hawajaamka waakina,warioba,butiku,na wengine wenye busara wakatibua huu mpango.
 
Katika mshangao mkubwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kada maarufu wa CCM stephen Mashishanga amekitaka chama cha mapinduzi kumfukuza mara moja kada wa chama hicho Mustapha Sabodo kwa kile aklichodai ni usaliti wa waziwazi kwa chama hicho tawala.
Mashishanga amedai maneno aliyotamka alipokuwa na Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ni usaliti mkubwa kwa CCM.Mashishanga hajafurahishwa na kauli ya Sabodo alipomwambia Dr Slaa anatamani CCM ishindwe uchaguzi wa 2015 na akaahidi kumchangia mgombea urais wa Chadema shilingi milioni 500.
SOURCE MTANZANIA.

Embe lililooza haliwezi tena kubaki juu, kinachofuata ni kudondoka tiii..CCM hawawezi kulikwepa hili mwisho wao umefika.
 
Naomba Mungu mwenye madaraka ya kumfukuza Sabodo afanye fasta. Cjui anapendelea kunywa bar ipi ili nkimkuta nimtandike John walker green label ili kufacilitate uböngo wake utoe maamuzi ya kumfukuza sabodo mapema kabla hawajaamka waakina,warioba,butiku,na wengine wenye busara wakatibua huu mpango.

Duh!! Mkuu unamfahamu Mzee Sabodo kweli?
 
nini maana ya kada wa chama jamani? ..... na dhani ma kada ni wle waliopitia mafunzo ya uongozi na siasa za vyama vyao ndio wanaitwa makada, wengine ni wanachama tu!

Dah, Mkuu umeeleza vizuri sana maana hili neno wengi linawapiga chenga.
 
mzee mashishanga na chama chake bado wanatamani watu wenye unafiki waendeleekusapoti ccm. sabodo amechoka hakuna jinsi mnatakiwa kumuheshimu.
mashishanga mzee wetu pumzika kwa amani na pensheni yako
wajinga wanapungua kila kukicha.
siasa za kutawala watu kifikra ziko ukingoni.
 
kumbe kukosolewa ni marufuku ndani ya ccm?
ULIKUWA HUJUI HILO...??? mBONA LIPO TANGU ZAMANI...!!! sIKU ZILE UKITOFAUTIANA NA MWALIMU UNAPOTEZWA AU UNAFUNGIWA KIJIJINI KWENU........... Siku hizi unaweza ukauwawa...... au........... ukaambiwa wewe si raia.............. AU............. CCM NI NDIYO MZEEE NA ZIDUMU FIKRA..........
 
Ndo tatizo la kutokutaka kukosolewa, kinyume chake sio mwenzetu.
 
Kwa msioelewa kiswahili cha CCM: Steven Mashishanga anamtuhumu Mustapha Sabodo kukisaliti chama. Badala ya kufuata utaratibu uliowekwa na CCM (wa kuiba mali za umma na kuwakandamiza maskini) yeye ndio kwanza anafanya kinyume chake (anawachimbia wanavijiji visima vya maji safi) bila kutumia akili kuwa:

-Watu wa mashambani wakinywa maji safi hawataugua ugua hovyo
-kama hawaugui manake watapata fursa ya kwenda shule
-kama wakienda shule wataelimika
-na wakielimika hawatachagua CCM tena

Sasa kweli Mustapha Sabodo anaitakia mema CCM?
 
Tutapata ukombozi siku watanzania watakapo tambua kuwa msingi wa shida zao ni CCM. Nao CCM watajirekebisha siku Watanzania watakapoamua kuwaweka pembeni walau miaka mitano.

Watu makini wote hawapo CCM tena, tuliobaki CCM ni mimi na Nape ambao hatuelewi tunamtumikia nani.
 
Wamewashindwa Chenge na Lowasa wanahamia kwa Sabodo.

Watimueni kwanza kina Chenge na Lowasa. Msijiongezee mzigo ambao hamna uhakika wa kuubeba.

Kwa jeuri ipi waliyonayo?Ndoa CCM iliyoingia na hawa kina Chenge haivunjiki hivi hivi..
 
safi sana CCM wamepata kidume cha kuwakosoa hadharani na kuonyesha mapenzi kwa upinzani, nimeamini kweli "pesa silaha, kisu (greeenguards) mzigo".
 
Back
Top Bottom