Sabodo afukuzwe uanachama CCM - Mashishanga

Katika mshangao mkubwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kada maarufu wa CCM stephen Mashishanga amekitaka chama cha mapinduzi kumfukuza mara moja kada wa chama hicho Mustapha Sabodo kwa kile aklichodai ni usaliti wa waziwazi kwa chama hicho tawala.

Mashishanga amedai maneno aliyotamka alipokuwa na Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ni usaliti mkubwa kwa CCM. Mashishanga hajafurahishwa na kauli ya Sabodo alipomwambia Dr Slaa anatamani CCM ishindwe uchaguzi wa 2015 na akaahidi kumchangia mgombea urais wa Chadema shilingi milioni 500.

SOURCE: MTANZANIA.
Oxymoron.................................
 
Ok, nimekuelewa, nadhani miye ndo sikukusoma vizuri. Mashishanga nashangaa sijui kapewa nini na JK, maana alimtosa mara tu alipoingia madarakani.
mkuu nguvu ya cdm igunga iliilazimu ccm kumuita mashishanga na mangula
 
General Collin Powel alimuunga mkono Barack Obama pamoja na yeye kuwa Republican tena wazi wazi bila kificho hakuwahi hata kuulizwa na chama chake. Hawa magamba kwanini hawajifunzi kwa watu waliopitia mifumo hii ya kidemokrasia kwa muda mrefu, Mzee wangu Mashishanga hebu fikiria upya maana hata wewe ulimuunga mkono Sumaye uliona ni bora zaidi ya Kikwete sasa kosa la mzalendo Sabodo ni nini? After all ccm ndio mnamtegemea zaidi Sabodo kuliko yeye anavyowategemea
 
Saboro lazima afilisiwe. Tunampa mwaka mmoja tu na atakuwa juu ya mawe.
 
Saboro lazima afilisiwe. Tunampa mwaka mmoja tu na atakuwa juu ya mawe.
Ah! Mzee mwenyewe anakaribia kutuaga kama sisi tutaendelea kuwepo! Niliona kwenye gazeti ameshateua na warithi kabisa!
 
Tena afadhali Sabodo analaumu mfumo ndani ya CCM hagusi haiba ya mtu, yeye Mashishanga akiwa mkuu wa mkoa Morogoro alitamka maneno ya kejeli kwa wagombea wengine aliposema hayuko tayari kuongozwa na rais msanii ambaye ana uhakika hata mudu jukumu la kuongoza nchi.

Na tunajua alimlenga nani. Taabu ya watanzania ni kuwa vigeugeu na kukwepa misimamo ambayo ingeweza kuwajengea heshima. Mimi kabla ya hii kauili ungeniuliza ni kiongozi yupi wa ngazi ya juu serikali na CCM aliwahi kuonyesha busara na kutumikia ukweli ningekwambia bila kuuma maneno ni Mashishanga. Kwa nini?

Ni kwa sababu yeye tu aliona mbali na akakataa kufa na maneno yake na kujitokeza mbele kuwaeleza watanzania kilichokuwa moyani mwake and the history has proved him correct on that aspect. Lakini kwa msimamo wake wa leo kuhusu sabodo unafuta umakini aliounyesha mwaka 2005 na kumrudisha katika uonvyo wake wa asili, sijui hata binti yake anamwambia nini amemfuta ukoo kwa kuwa anatofautiana naye kiitikadi?

Kuwa na maoni tofauti katika jicho la kisiasa si uhaini, Mwaka 1995 tukiwa katika uchanga wa vyama vingi Nyerere alisimama imara kuwakosoa wagombea CCM majimbo mawili ya Musoma na badala yake ni kama aliwaombea kura wagombea wa NCCR sijui Mashishanga anamweka baba wa taifa katika kundi lipi?

Hawa wameweza, waendelee kuikosoa CCM kwa nguvu zao zote, Tanzania tuitakayo itakuja lazima. Na sasa tunaona wengi wanazaliwa kila kukicha, Tambueni kuwa uovu katika jamii na siasa si suala ambalo linaweza kudumu milele. Kwa nguvu na maagizo yake baba, nuru ya umilele ilitolewa katika utukufu tu na adui yake mkubwa ni tabia za ushetani. T u t a f i ka l a z i m a
 
Saboro lazima afilisiwe. Tunampa mwaka mmoja tu na atakuwa juu ya mawe.
Anafirisiwa kwa njia ipi? ya hila kwa sababu amewapinga? Na nani atamfilisi kijinga hivyo TRA? kwa hiyo unataka kutuambia vyombo na wakala wa serikali hutumika kwa masilahi ya CCM? afadhali umetujuza tuelewe hivyo, kwa hiyo siku mwingine akiingia madarakani awafilisi wote wanaowapinga sasa?
 
Mzee Mashishanga kishachoka, bora apumzike na mambo ya siasa amwachie mwanae Rachel asaidie wapiganaji wengine kuleta mabadiliko kupitia chadema.
 
Bashe naye amewahi kutamka kuwa anataka CCM ishindwe Igunga ili mheshimiane. Mfukuzeni.
Wee Mashishanga hana jeuri ya kusema hivyo kwa Bashe,Mashishanga ni kati ya wazee wanaozeeka vibaya ,sampuli za akina mzee Makamba,mbona hajamfukuza nyumbani kwake binti yake ambaye ni kiongozi wa CDM,kwanza yeye mashishanga ni nani kwani hilo tu ndio kaliona?kwanza arudi usukumani badala ya kulowea uluguruni hii ni aibu kwa mtu mzima kukataa kwenda kumalizia maisha kwenu
 
Kuna wazee wafuatao wanazeeka vibaya...
  1. Stephen Mashishanga..
  2. Wasira
  3. Msekwa...
  4. Sitta..
  5. Kingunge...
  6. Warioba
endeleza list..................
 
Saboro lazima afilisiwe. Tunampa mwaka mmoja tu na atakuwa juu ya mawe.

Mkuu hapo kwenye red sio "Saboro" ni Sabodo najua utasema ni typing error lakini mimi najua ni kwasababu ya uwezo wako mdogo wa kufanya mambo.Kwa upande wa mada ni kawaida yenu? Mnawaacha wahuni kama RA halafu mtawasumbua wazee wenye akili kama Sabodo....
 
Mzee mashishanga amepotoka hiyo ndiyo demokrasia si afadhali mzee sabodo mashishanga ananufaika na chadema kupitia kwa binti wa kiuno chake ambae ni mbunge wa viti maalum kupitia chadema amfukuze basi na amtenge kutoka katika familia yake
 

Matajiri na Wahindi wakitoa pesa CCM = Hicho chama kimetekwa!

Matajiri na Wahindi wakitoa pesa Chadema = Huo ni uzalendo! Peeepoz Pawa!
 
Back
Top Bottom