Sabodo afukuzwe uanachama CCM - Mashishanga

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Katika mshangao mkubwa aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wa Morogoro na kada maarufu wa CCM stephen Mashishanga amekitaka chama cha mapinduzi kumfukuza mara moja kada wa chama hicho Mustapha Sabodo kwa kile aklichodai ni usaliti wa waziwazi kwa chama hicho tawala.

Mashishanga amedai maneno aliyotamka alipokuwa na Katibu mkuu wa Chadema Dr Wilbroad Slaa ni usaliti mkubwa kwa CCM. Mashishanga hajafurahishwa na kauli ya Sabodo alipomwambia Dr Slaa anatamani CCM ishindwe uchaguzi wa 2015 na akaahidi kumchangia mgombea urais wa Chadema shilingi milioni 500.

SOURCE: MTANZANIA.
 
Kumfukuza uanachama ndo watamkomoa? Labda kwa hila zao, wawaagize TRA kuingilia biashara zake, la sivyo ndo kwanza watakuwa wameongeza mafuta kwenye utambi. Wataisha tu.

Wanachotakiwa kujihoji, kwa nini hata makada wao wa siku nyingi wamewachoka na kuonesha waziwazi?
 
tatizo la magamba wanajiangalia wao tu mwenzao akijitokeza kutetea wananchi wanasema msaliti hawa watu hawafai kabisa.
 
Mwendelezo wa siasa za chuki!mashishanga mwenyewe alisema anamuunga mkono sumaye kwenye kura za maon za urais(2005) jk akamtosa.Lakin pia mashishanga mwanae wa damu ni CHADEMA atangaze basi kua yule c mwanae!nadhan SABODO hafurahshwi na mambo ya chama chake
 
nini maana ya kada wa chama jamani? ..... na dhani ma kada ni wle waliopitia mafunzo ya uongozi na siasa za vyama vyao ndio wanaitwa makada, wengine ni wanachama tu!
 
Mashishanga angekua baba yangu ningemkana kabisa,kati ya watu wanaochanganyikiwa vibaya ni huyo mzee lofa mkubwa,ujue hakumbuki ccm ya jk ilivyo mpiga ban kali na baadae hali ya Igunga ilivyo kuwa mbaya wakamtumia,sasa kameamua kajikombe zaidi kwa kutoa matamko ya kijinga,njaa mbaya
 
Enzi zetu makada wa chama walikuwa ni wale tu waliokuwa wamepitia mafunzo maalum angalau kwa miezi 9 kwenye vyuo vya CCM kama Kivukoni, Hombolo, Murutunguru,....Mashishanga si mmoja wao.
 
Ni njaa na kujikomba kwa Mashishanga hana lolote jipya na kumfukuza hawawezi wameshindwa magamba sasa wanatapatapa
 
Sabodo ni mtu jasiri sana yule mzee, bora wamuache tu, wakimkorofisha watamkoma, atadhamini kila mpambano wa Chadema, operesheni sangara itafanywa kwa kutumia helikopta hata tatu, yule mzee jeuri hii anayo. Lets wait
 
Back
Top Bottom