Wengi mlioandika mmekuja kwa asira na utashi wa kukosoa,inaweza kuwa kweli kuwa karibu na huyu Tony sio kwema lakini kuna sababu Tony Blair kuwa na hiyo nafasi,na wala si kuwa ni yeye binafs naomba mfuatile 'Tony Blair Institute' alafu jiongezeeni ujuvi.
Pamoja na kuwa Blair kwao anaonekana mwongo sababu ya vita ya Iraq,lakin bado ni 'one of the most influencial figures in uk',na bado ana uhusiano mkubwa na wa karibu na wanasiasa,wafanyabiashara na viongozi wengi serikalini,ivo msimchukulie poa.
Mwaka 2016 mzee mmoja aitwa John Chilcot alifanya assessment ya kitendo cha Tony Blair kuiingiza nchi yake kwenye uvamizi wa Iraq.
Tathmini ile ilimmaliza kabisa Tony Blair pale iliposema kwamba yeye (Blair) na George Bush waliudharau Umoja wa Mataifa na kuamua (wao wenyewe) kuivamia Iraq.
Tony Blair mwenyewe akihojiwa na Fareed Zakaria wa CNN mwaka 2015 aliomba radhi kwa makosa aloyafanya na akakubali kwamba kulikuwa na ukweli kwenye madai uvamizi ule ulisababisha kuibuka kwa kundi la ISIS.
Tukiachana na hayo, Tony Blair ni mwanasheria nguli, msemaji na mzungumzaji mzuri yaani "keynote speaker and Performer" na hualikwa kwa kutoa mihadhara mingi ya faragha kwa pesa ndefu sehemu mbalimbali duniani.
Tony Blair amewahi kuwa mhadhiri wa masuala ya utandawazi na imani katika vyuo vikuu vya Yale na Divinity na baadae akashiriki kuanzisha stashahada katika masuala hayo iitwayo Globalisation Initiative kwenye vyuo hivyo vya Yale, Durham cha UK na national University cha Singapore.
Iliripotiwa kuwa Tony Blair ana kamba zilizounganishwa kwenye kampuni iitwayo UI Energy Corporation na huvuta mpunga wa kutosha kutoka huko.
Hii kampuni inajishughulisha na utafutaji na uchimbaji wa mafuta, madini, uwekezaji wa vituo vya kufulia umeme na pia inajishughulisha na usambazaji wa vifaa vya mahospitalini yaani medical equipment.
Hawa UI Energy ni sehemu ya mtandao mkubwa yaani Consortium wa makampuni mengine mengi tu humo uitwao KNOC Bazian Limited.
Hili la Tony Blair kuwa mshauri wa serikali ya Tanzania si geni, kwani nchi zingine kama Khazakhstan zimemtumia kusafisha taswira ya nchi hiyo ambayo ilikuwa na rekodi chafu kabisa ya ukiukaji haki za binadamu na rekodi hiyo bado ipo palepale.
Kuna mauaji makuwa yalifanywa nchini humo yaloitwa "Zhanaozen Massacre" na Tony Blair akatumiwa na raisi wa nchi hiyo Nazabayev kufanya kitu chaitwa damage-limitation advice.
Tony Blair amewahi kuwa mshauri wa masuala ya biashara kwa serikali ya Misri.
Tony Blair ni mjasiriamali na ana hisa katika makampuni kadha wa kadha na kiasi cha fedha za kutoka katika akiba ya benki.
Juzijuzi mzee huyu ametajwa katika orodha ya watu ambao ni mashuhuri lakini wanaweka fedha nje ya nchi zao, orodha ilopewa jina la Pandora Papers.
Uwezo wake wa fedha na ushawishi wake mkubwa umemfanya kuwa na marafiki au watu wengi ambao hujihusisha nae kwenye masuala ya biashara yaani Associates na alianzisha kitu chaitwa Tony Blair Associates.
Hawa hukusanya fedha na kuzielekeza katika miradi au shughuli mbalimbali barani Afrika na nchi za mabara mengine.
Ndipo akaanzisha taasisi iitwayo Institute for Global Change.
Pamoja na mambo mengine mengi taasisi hii kwa sasa imejikita kwenye janga la COVID-19.
Hivyo hii waita Government Advisory Practice ambapo taasisi hii ina watu kama 200 hivi ambao wamesambazwa katika nchi hizi za Afrika na zingine.
Kwa Afrika kuna nchi 14 kama za Senegal, Rwanda, sasa Tanzania na Zanzibar wamejiingiza humo hivi karibuni.
Vaccine Management for Africa.
Huu ndo mpango wenyewe ambapo Tony Blair kwa kupitia taasisi yake wanashirikiana na Oracle ambao ni wataalam wa kanzidata kuboresha mifumo ya kuweka kumbukumbu za afya katika mpangilio wa kisasa.
Hii Oracle Health Management System itasaidia kurahisisha usambazaji na utoaji wa chanjo na rekodi za watu wote walochanjwa zitahifadhiwa kwenye kanzidata iitwayo Cloud.
Kwa kifupi ni kwamba kama umechanjwa Afrika na wataka kwenda Ulaya au Marekani basi itakuwa rahisi kupata taarifa zako kwa wakati muafaka.
Hivyo hiyo yaweza kuwa ni moja ya masharti kwa serikali ya Tanzania kuondolewa kwenye ile Red List.
Pili hii kanzidata ya OHMS ikiimarishwa itasaidia nchi za Afrika kuweza kuwa na mipango mingine zaidi ya kupambana na si tu COVID-19 bali magonjwa mengine kama polio na surua.
Ikumbukwe kuwa nchi za Afrika kwa kukubali kushiriki katika mpango wa COVAX na mingine kama huu wa OHMS zimepewa miaka 10 kutumia mfumo huo na kupata msaada wa kitaalam na bila malipo.
Hivyo kwangu mimi sioni kama kuna tatizo kwani sisi kama nchi bado tupo nyuma sana kiteknolojia na kufikiri nje ya boksi.
Na ndo maana hata raisi wetu ametangaza kujengwa kwa chuo kikubwa sana cha Tehama Tanzania ambacho kitafundisha vijana masomo ya sayansi na kompyuta ingawa tayari wasomi wa tasnia hizi wapo na wanazurura mitaani.
Hivo tukijadili tuangalie zaidi Context ya mradi ( IFGC) na sio mtu binafsi maana yeye bado aruka na ndege huku na huko duniani kupiga pesa ya maana.