SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

Memento

JF-Expert Member
Jun 13, 2021
4,423
9,962
Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

Screenshot_20211025-221652_1.jpg
 
Wengine tulishaliona hapa na kuandika, hii ni fedheha sana,Blair ni tapeli la kimataifa, yeye ni mtu wa kupiga dili tu hana lolote, ana historia mbaya sana na hizo dili zake na hata Pandora Papers yumo kaficha pesa zake anazopata kwa kula rushwa.

Na hiyo pesa ya msaada kwa ajili ya COVID itaishia kumlipa Blair. Sijui huyu tapeli atamshauri nini raisi wetu ambacho washauri wa raisi wetu wameshindwa kumshauri au hawakijui.
 
Hatari sana kujiweka Rehani.

Awamu ya Sita tunawategemea wazungu kwa kiasi kikubwa.
Kuna tatizo kubwa kama Mkuu wa nchi atakuwa na washauri peke yao walioelimishwa kwa fedha za multilateral institutions au taasisi za magharibi!!! Mlengo wao mara nyingi sio kuwa independent thinkers bali to always lean towards western interests na sio interests za nchi zao!!! Ni vema kama kiongozi akiwa na jopo [ diversity] la washauri hasa kwenye mambo ya uchumi kuliko kumtegemea kiumbe mmoja!!

Kuhusu uteuzi wa Tony Blair, mimi binafsi sina tatizo kutegemeana na nchi inataka nini kutokana na uteuzi huo. Katika miaka hii ya utawala wa Magufuli nchi yetu haikuwa na uhusiano mzuri na mataifa mengi hasa ya Ulaya na Marekani; hivyo ikaonekana kutokana na historia ya huko nyuma enzi za Mkapa, mtu pekee ambae anaifahamu vizuri nchi yetu na angeweza kutusaidia kurudisha uhusianao mzuri na nchi za nje ili kupata misaada hasa wa kupambana na covid 19 ni taasisi ya Tony Blair.

Tukumbuke kuwa huko nyuma akiwa Waziri Mkuu enzi ya Mkapa nchi yetu ilikuwa na ludo la madeni ya nje na ni huyu huyu Tony Blair aliyetusaidia kuwashawishi wadeni wetu kupunguza na hata kuyafuta madeni na nchi ikapata afueni. Ni kufuatana na historia hiyo na matatizo tuliyonayo na covid 19 ndio maana ikaonekana kuwaomba taasisi ya Tony Blair kutusaidia ni jambo la busara. Tukumbuke pia kuwa hizi chanjo za covid19 zinapatikana hasa kwenye nchi zilizoendelea na hasa marekani hivyo tunahitaji mtu anayekubalika na BIDEN iili kupata hizo chanjo!

Tanzania sio nchi pekee ya Africa inayomtumia Tony Blair kwa ushauri. Majirani zenu wa Rwanda wamekuwa wanamtumia kwa muda mrefu sasa na wana matokeo mazuri
 
Back
Top Bottom