SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

SABC washangaa Rais Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake

Hoja ya Tonny Blair haiishii hapo tu. Blair ndio alituuzia rada kwa Bei kubwa hadi waingereza wenzake wakaingilia kati
Tony Blair anauzaje radar? BAE ndiye muuzaji wa Radar kwa Tanzania, nionyeshe uhusika wa PM wa UK kwenye hilo!!
 
Alikuwa mhuni miaka ya nyuma. Usikariri tukio moja la zamani ukalihusisha na jingine la miaka ya sasa. Kila mtu anao ujanja wa kuongea na mtu mwingine, anao ushawishi wake usiofanana na wa mwingine.
Kwa.hiyo.unakiri Tony alikua mhuni mhuni enzi hizo na hata Pandora news ya juzi ilimtoa kuwa alimfaidisha Mkewe kibiashara kuficha mkwanja akiwa ofisini kwenye u PM?

Sent from my SM-G9350 using JamiiForums mobile app
 
Shirika la habari la South Africa walikuwa na mjadala kuhusu Mama Samia kumteua Tony Blair kuwa mshauri wake.

Hoja ya wachambuzi haikuwa kwa nini Tony Blair Bali ilikuwa credibility ya Tony Blair.

Wanasema Tony Blair hana credibility, hivyo kumteua kuwa mshauri ni kosa na wanashangaa imekuwaje Tanzania nchi iliyopigania ukombozi kufanya kitu kama hicho.

Mimi binafsi kwenye hili sijui hata nisimamie wapi maana sijui pa kuanzia, ngoja tuendelee kusubiri wajuvi wakilichambua kwa hoja.

View attachment 1987100
Ndio maana tunasema mama samia is either naïve au ni msaliti. Kwanza tujiulize kwa nini mkora wa kisiasa kama tonny blair aje kimyakimya tunashitukia ana maongezi na samia ikulu. Taifa hatujaambiwa rasmi ila samia ajue tonny blair si mtu wa kumuamini.
 
SA sidhani kama wanakitu chochote cha kuifundisha Tanzania..
Zuma ana kesi mahakamani huko. Na ninyi mna la kujifunza hapo. Au ninyi marais wenu wako juu ya sheria.?
Kwani yeye Mh. Tony Blair alitulazimisha kununua hiyo rada?
cc: Bulesi
Nini maana ya kumsaidia mtu fedha, kisha unamtumia wahuni kwenda kumkaba na kumpora fedha zenyewe!?
 
SA chama kipya kinaandaa Xenophobia ya kuaa na kupokonya mali za wageni weusi mwezi ujao Nov njaa ikiwabana wanaamini katika kupora hiyo SABC hutawaona wakiwata watu kuhoji huo ujinga ndio watufundishe sisi..
Ninyi rais wenu yuko juu ya sheria. Wenzenu rais anafukuzwa kazi , kama Mbeki au Zuma walivyofukuzwa.
 
Wengi mlioandika mmekuja kwa asira na utashi wa kukosoa,inaweza kuwa kweli kuwa karibu na huyu Tony sio kwema lakini kuna sababu Tony Blair kuwa na hiyo nafasi,na wala si kuwa ni yeye binafs naomba mfuatile 'Tony Blair Institute' alafu jiongezeeni ujuvi.
Pamoja na kuwa Blair kwao anaonekana mwongo sababu ya vita ya Iraq,lakin bado ni 'one of the most influencial figures in uk',na bado ana uhusiano mkubwa na wa karibu na wanasiasa,wafanyabiashara na viongozi wengi serikalini,ivo msimchukulie poa.
 
Hii ni aibu ya Karne Kwa Taifa, Tanzanians wahahitaji hiyo institute ya Blair , Tanzanians wanahitaji ajira, maji,viwanda, kilimo na haduma bora , hivi vitu anavyo fanya Samia ni utoto wa Hali ya juu, kwani katika awamu iliyopita Tanzania haikuwahi kufungia na mataifa ya nje, kama misaada ilikuja tena Dr. Mpango alimwakilisha Rais kwenda nje na kuongea na mashirika ya fedha duniani bila shida, Kuna wasomi wazuri tu hapa nchini wanatosha kuitangaza nchi.
 
Kwa hiyo unaona uwezo wa Blair kupiga simu ikulu ya Washington ndio kigezo hasa cha mama kumteua kuwa mshauri wake?

Kuweza kupiga Simu Ikulu ya Washington maana yake ana heshimika kiasi cha simu yake kuweza kupokelewa na kuzungumza, hicho ni kigezo kikubwa sana vinginevyo chanjo zitapatikanaje bila wakuu kutoa ruksa? Sio kila Simu inaweza kupokekelewa White House!!!

Wengine Wanasema eti mbona Mpango alikuwa anamuwakilisha Jiwe na misaada ilikuwa inakuja!! Mpango alikuwa anakutana na watu wa world Bank na IMF kupata mikopo ya miradi; sidhani hata kama aliwahi kukutana na Secretary of state licha ya Waziri wa fedha wa Marekani!!! Chanjo ziko chini ya Serikali ya marekani na bila shaka Balozi Mulamula ndiye aliyeshauri kumtumia Blair Kwani anajua na anauzoefu wa mbinu za kufanikisha kupata chanjo kwa wakati pale zinapohitajika.
 
Zuma ana kesi mahakamani huko. Na ninyi mna la kujifunza hapo. Au ninyi marais wenu wako juu ya sheria.?

Kikwete alinusa yaliyomfika rafiki yake Zuma, akaona isiwe shida akaiweka RASIMU YA KATIBA ILIYOPENDEKEZWA KWAPANI!!!!
 
Kumbuka nchi za kiafrika nyingi zilianza kupata msaada toka WHO wakati nyinyi na Jiwe wenu mlikuwa mnajifukiza NYUNGU!! Sasa mmezinduka baada ya JIWE kutwaliwa ni lazima mkimbie ili muweze kunusulika na kuchelewa kwenu na ndio maana akili kubwa ikatafuta mtu anaeweza kumuingia BIDEN na kufanikisha hilo!!! Rwanda wanamtumia Blair, unaona Mafanikio yao wewe bwege unaeniita mimi mtoto wa nursery?
Yale mamitambo ya nyungu yapo wapi maana siyaoni tena (ujinga kitu mbaya sana)
 
-watu wote tujifukidhe na mixture iliyobuniwa na wataalamu wetu hapahapa Tanzania.

clip_now_20211009_102139.png
 
Back
Top Bottom