Sabaya: Sikumbuki kushtakiwa kwa kujifanya Usalama wa Taifa

mshale21

JF-Expert Member
Apr 8, 2021
2,049
4,904
Arusha. Lengai Ole Sabaya, aliyekuwa mkuu wa Wilaya ya Hai, amedai hakumbuki kushtakiwa kwa kujifanya ofisa Usalama wa Taifa wala kuhojiwa na Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi Odira Amworo, katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha jana, Sabaya alitoa madai hayo akiwa anahojiwa na mawakili wa Serikali, Tumaini Kweka, Felix Kwetukia na Baraka Mgaya kwa tofauti tofauti, kuhusu utetezi aliotoa mahakamani hapo.

Akihojiwa na Mgaya, Sabaya alieleza mahakama kumtambua mshtakiwa wa pili katika kesi hiyo, Sylvester Nyegu na kudai kuwa hakuwa msaidizi wake, bali alipata kazi na mkurugenzi wa halmashauri ya Hai.

Sehemu ya mahojiano ilikuwa hivi:

Wakili: Shahid hakukusikia wakati unatoa ushahidi wako kuwa mamlaka ya utumiaji wa sheria zetu sijui akaja Dk Bashiru na kesi iliyokuwa inakukabili mahakamani iliondolewa na DPP?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Ni sahihi ulifikishwa mahakamani kwa kosa la kujitambulisha wewe ni usalama wa Taifa 'undercover'.

Shahidi: Sikumbuki.

Wakili: Shahidi ni sahihi kesi hiyo ya jinai ndiyo ilipeleka ukatenguliwa nafasi yako ya uenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha

Shahidi: Siyo kweli

Wakili: Shahidi wa sita wa jamhuri (Bakari Msangi) alieleza mahakama alikuwa mjumbe, wewe umiliki mwenyekiti na moja ya sababu za kuuawa ni kesi hiyo na tumeundwa na mako makuu?

Shahidi: Sikumbuki Bakari alisema nini kuhusu kutenguliwa, lakini hakueleza hayo.

Wakili: Kuanzia Julai 2018 hadi Mei 2021 ukiwa katika Wilaya ya Hai, ulikuwa ukifahamika kama mkuu wa wilaya?

Shahidi: Kila mtu alikuwa na namna yake ya kunitambua

Wakili: Hapa mahakamani kwa mara ya kwanza Julai 16, 2021 ulisomewa mashtaka matatu yanayokukabili?

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Uliulizwa majukumu yako ya DC ni yapi?

Shahidi: Nilieleza majukumu ya DC shughuli za shughuli zote za maendeleo, usalama wa usalama na kutekeleza majukumu mengine ambayo hutumika na mamlaka iliyomteua

Wakili: Kwa hiyo utakubaliana pamoja na Katiba, sheria iliyokuwa inaongoza majukumu yako ni sheria inayosimamia Tawala za Mikoa?

Shahidi: Ni moja ya sheria hizo.

Wakili: Kwa mujibu wa sheria hiyo, ulikuwa unawajibika chini ya mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

Shahidi: Sijaisoma hiyo sheria

Wakili: Kwa hiyo ulikuwa hujui unatekeleza majukumu yako chini ya nini?

Shahidi: Sijui.

Wakili: Uliapishwa tarehe ngapi kuwa mkuu wa wilaya?

Shahidi: Tarehe 1 / 8/2018

Wakili: Uliapishwa wapi na nani alikusimamia kula kiapo?

Shahidi: Nilikula kiapo mbele ya mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Wakili: Nani aliyekupa kiapo?

Shahidi: Simfahamu.

Wakili: Baada ya kuapa ulimfahamu alikuwa ni nani?

Shahidi: Dk Anna Elisha Mghwira

Wakili: Unaieleza mahakama ulikuwa humjui mkuu wa mkoa ambao anakuapisha ni nani.

Shahidi: Kwa wakati nimeshika biblia naapa, sikuwa namfahamu ila nilimfahamu baada ya kuapa.

Wakili: Mamlaka yako ya uteuzi kuwa DC ni nani wakati huo?

Shahidi: Rais wa Jamhuri ya Muungano Tanzania.

Wakili: Kama mamlaka iliyokuteua ni Rais kwa nini ulienda kuapa kwa mkuu wa mkoa?

Shahidi: Aliniapisha kwa niaba ya Rais.

Wakili: Kwa hiyo moja ya msingi hiyo uliapa mbele ya mkuu wa mkoa, hiyo majukumu yako ulitakiwa utekeleze kupitia yeye.

Shahidi: Yeye pamoja na wengine.

Kuanza utumishi wa umma

Wakili: Lengai ulianza lini kuwa mtumishi wa umma?

Shahidi: Siwezi kulieleza hilo bwana bwana.

Wakili: Tarehe 9/2/2021 baada ya kumaliza kikao ulieleza kuwa utapata simu kutoka kwa mamlaka iliyokuteua

Shahidi: Ndiyo.

Wakili: Na ukapokea wageni uongezane nao Arusha.

Shahidi: Nilieleza.

Wakili: Na ukawaongoza kuja Arusha kama nani?

Shahidi: Siwezi kueleza, anayeweza kujibu ni aliyenipa kazi hiyo.

Wakili: Lengai amesema miongoni mwa majukumu yako ni mwenyekiti wa kamati za ulinzi na usalama.

Shahidi: Ni sahihi.

Wakili: Utakubaliana na mimi majukumu hayo ambayo ni ya kiwango cha juu na kile kitu kimeundwa na nguvu.

Shahidi: Nakubaliana na wewe

Wakili: Katika muktadha huo utakubaliana na muundo wangu na kazi ya kamati ya ulinzi na usalama, siri?

Shahidi: Siyo.

Wakili: Na kazi za hizo kamati zimehifadhiwa hivyo hivyo sio siri.

Shahidi: Ni siri.

Wakati fulani, wakili alimuuliza kuhusu baba yake na kuhojiwa kwake na Tume ya Haki za Binadamu:

Wakili: Baba yako yupo?

Shahidi: Siwezi kueleza masuala ya kifamilia. Sitajibu hilo swali

Wakili: Una uhusiano gani na Mzee Thomas Ole Sabaya

Shahidi: Siwezi kueleza uhusiano wetu

Wakili: Nikikwambia ni baba yako utakataa?

Shahidi: Siwezi kueleza hilo

Wakili: Lengai kati ya masuala uliyoulizwa na Tume ya Haki za Binadamu, ni kwanini una vijana zaidi ya wale unaokuwa nao ofisini na ofisi ya ofisi na si waajiriwa wa utumishi wa umma?

Shahidi: Sikumbuki kuwahi kuulizwa swali hilo

Wakili: Jana wakati unajitetea wakili alikuuliza ukataja operesheni nyingi na ukaeleleza watu wengi wanatumia nje ya maeneo ya kazi, wakati alitekeleza kutoka kwa Hai alikuwa na cheo gani?

Shahidi: Nilikuwa Mkuu wa Wilaya

Wakili: Mkuu wa Wilaya ni kazi ya kiutendaji au kisiasa?

Shahidi: Mtumishi wa umma (mtumishi wa umma)


Chanzo: Mwananchi
 
Akili zake zipo nusu kaputi au ? 😁👇
10c.png
 
Sawa bwana general tumekusikia, Ila daaah kwa nchi za wenzetu ujiite General cheo ambacho watu wanaloga asubuhi na jioni hawakifikii Leo sabaya ni General looh😢😢😢😢😢
 
Jamaa alikuwa mpuuzi sana. Sijui ilikuaje akawa DC. yaani hajui tu ile kutoka nje ya wilaya yake tayar siyo DC tena?????
Ati anasema ametumwa na mamlaka za uteuzi???? Kwahiyo zingemtuma akamuue babake angekwenda????
 
Sawa bwana general tumekusikia, Ila daaah kwa nchi za wenzetu ujiite General cheo ambacho watu wanaloga asubuhi na jioni hawakifikii Leo sabaya ni General looh😢😢😢😢😢
Yule diwani mwenye hio kesi kule dukani kwa Mwarabu alimsalimia Sabaya habari za mchana mh. Sabaya,jamaa halikujibu likamwambia Mlinzi wake hanijui jina langu huyu mshughulikie.

Diwani alikula makofi ya masikio mpk akakumbuka jina la mkuu,akasalimia tena Habari za mchana GENERAL MO POWER ndipo Sabaya akamjibu.
 
Jamaa alikuwa mpuuzi sana. Sijui ilikuaje akawa DC. yaani hajui tu ile kutoka nje ya wilaya yake tayar siyo DC tena?????
Ati anasema ametumwa na mamlaka za uteuzi???? Kwahiyo zingemtuma akamuue babake angekwenda????
Ndipo unaweza ukajua IQ ya mteuaji wake ilikua Ni ya level gani mkuu.
 
Hayo maswali ni leading questions. Yaani unaulizwa swali ukilijibu tu unapigwa lingine kwisha habari ndio maana Sabaya anayapangua kwa njia hiyo

Akijichanganya kujibu kama anavyotaka wakili inakula kwake asubuhi na mapema.

Kwa mfano pale alipolengeshwa kuhusu baba yake amejibu kitaalam sana vinginevyo angeingizwa King kweupe
 
Back
Top Bottom