Sabaya asema alimiliki silaha kwa sababu alikuwa anatishiwa kuuawa

Waandishi wanatuangusha jumla. Mwananchi huko nyuma ilikuwa na waandishi wazuri, sijui kwanini sasa wako hivyo
 
pole shoga angu,tafuta bwana mwingine,Sabaya anafungwa
Mbona unachekesha sana! 1. Mimi ni mwanaume (najua unalijua hili ila umeamua kunitukana) 2. Sabaya simpendi kabisa kabisa na hata ningesikia amehukumiwa kunyongwa ningeandaa sherehe (hili hulijui na ulidhani kwenye post yangu nilikuwa namtetea)
 
Nilikuwepo Mahakamani leo, ninachoweza kusema ni kwamba huyu dogo HACHOMOKI kwenye hii Kesi iwe Jua iwe Mvua,Ushahidi wake ni wa magumashimagumashi sana mpaka Mawakili wake wanatingisha vichwa kama kutopendezwa na majibu yake,huyu Mvua zinamhusu
Nasikia wale wasaidizi wake kawakana hawajui?..
 
Huyu jamaa hakuwa wa kupeleka mahakamani, huyu jamaa kama jamii inauhakika kweli aliyetenda maasi kwa raia wema bila sababu basi alipaswa aabakizwe mtaani ili aadhibiwe kama yule Marehemu Ditopile Mzuzuli.......huku atachomoka tuu nadhani
Ditopile aliadhibiwa kivipi?..
 
mi bado namung'unya popcorn yangu taratibu huku nikiangalia picha linavoenda ...🧏‍♂️
 
Back
Top Bottom