Sababu zinazopelekea viongozi kukingiana vifua pale wanapotakiwa kuwajibishwa kisheria, madhara yake katika maendeleo ya Taifa

DeMostAdmired

JF-Expert Member
Oct 7, 2017
1,180
2,943
-Kwa zaidi ya asilimia 90% viongozi wetu wanapatikana kupitia michakato ya kisiasa. Either kwa kuteuliwa na kiongozi wa kisiasa au kuchaguliwa na wananchi na wadau kupitia chaguzi zilizowekwa na zinazotambulika kisheria.

-Chama cha kisiasa hasa hapa kwetu nchini ni kama familia ambayo ina mshikamano, ina maagano, viapo vya siri, njama na mipango ya kijasusi.

-Yes ni familia lakini ni Ile familia ambayo ni sawa na camp ya catfish (kambale) yani mkubwa ndevu mtoto ndevu.

-Inapotokea nchi kwa asilimia kubwa inaongozwa na viongozi kutoka chama kimoja eg wabunge, ma DC, RC na wengineo, hii kitu huwa ni mwiba kwa puto la maendeleo ya Taifa.

-Nimefananisha vyama vya siasa hasa chama tawala kama camp ya catfish kwasababu....
1. Kiongozi mkubwa anamtegemea kiongozi wa chini yake na hata wa chini kabisa ili aweze kuendelea survive katika kiti chake.
2. Huyu kiongozi wa chini kabisa anamtegemea kiongozi wa juu ili aendelee ku-survive katika kiti au nafasi au fursa anazozipata kupitia system.

ATHARI ZAKE KATIKA MAENDELEO YA NCHI.

1. Viongozi wenye mamlaka kushindwa kuwawajibisha viongozi wanafamilia wenzao pale wanapopatikana kufanya makosa kisheria kupitia vyombo vilivyowekwa kisheria na vinavyoendeshwa kisheria.

2. Viongozi wakubwa kupungukiwa na nguvu ya kufanya maamuzi sahihi pale ambapo maamuzi yao yataonakana kugusa maslahi binafsi ya wanafamilia wenzao katika namna hasi.

3. Kushindwa kuwajibishwa kikamilifu kwa viongozi na wasimamizi mbalimbali katika nafasi mbalimbali za kiuongozi na kiusimamizi ni chanzo cha rushwa na ukiukwaji wa haki na upotevu wa stahili na stahiki za wananchi.

4. Rushwa, ukiukwaji wa haki, stahili na stahiki kwa wananchi ni chanzo cha ushukaji wa kimaendeleo almost katika kila nyanja kufuatia wananchi kama mashine za kuleta maendeleo kupungukiwa na ari katika shughuli na uzalendo kwa Taifa lao. Mfano mimi niliyeandika Uzi huu, ninaweza kuthibitisha ya kwamba kuna wastaafu flani wapo mkoa wa tabora walistaafu miaka kadhaa nyuma lakini mpka sasa hawajapata stahiki zao. Huwa wanajazishwa fomu zisizoisha na hakuna kinachoendelea Sasa hii ni athari ya upungufu wa nguvu na mamlaka miongoni mwa viongozi wenye dhamana na mamlaka ya kuwawajibisha wasimamizi na viongozi wanaoratibu mchakato wa mafao na stahiki za wastaafu.

5. Uibukaji wa watu wanaojiita CHAWA. Hawa watu huongea mambo ambayo yanawalinda viongozi no matter what iwe wanakosea au wapo sahihi wao wanachojua ni kusifia tu. This is the source of IRRESPONSIBILITY AND UNACCOUNTABILITY.

6. Upewaji wa teuzi kwa watu wasiokidhi vigezo kukaa katika viti husika ndio maana unaweza kuona viongozi wanaishia kuwa waropokaji ili angalau wawafurahishe wakubwa zao na waendelee kusalia katia vito vyao
Unaweza pata kuona jinsi viongozi wanaongea vitu vyakushangaza, vyakuchekesha na kusikitisha. Hii ni dhahiri kwamba viongozi wenye dhamana hawana uwezo wa kutoa mchango wenye tija kwa maendeleo kwasababu hawana uwezo wa kufanya hivo either kwakukosa elimu, maarifa au akili ya kufikiria kitaalam zaidi na mwisho wa siku wanajikuta katika uchawa.

ALL IN ALL - ROME WAS NOT BUILT IN A DAY.

Thanks.......
 
Back
Top Bottom