Sababu za wameru kumkataa Siyoi Sumari

wote uliowataja hawaishi meru.kwa wameru hili ni jambo kubwa.lakini ni lazima tujue meru ni jimbo lenye wamasai na wameru kwa wingi hata hivyo sikumbuki ni lini mmasai aliwahi kushika jimbo hili!

Mgombea Sioi, Baba ni Mmeru na Mama ni Mmasai(Ilboru). Ila sijui kwa nini mkuu unaangalia sana kabila wakati wazazi wa Sioi hawakuusisitiza ndiyo maana mdau mmoja anadai Sioi hajui 'kilugha'.

Jimbo la Arumeru linahitaji mbunge makini kama mgombea wa CHADEMA Bw. Nassari kutokana na sera makini za chama cha CHADEMA kutaka kuleta mabadiliko jimboni na nchini kwa ujumla, na siyo kwa vigezo la 'kabila','kilugha','urithi', rushwa na ufisadi.
 
Maadam ccm wameamua kumsimamisha sioy kuwa mwakilishi wao, basi hao wasiopenda kuona uongozi wa kisultani waonyeshe kwa mfano katika sanduku la kura.

Wasijekuwa wanaongea kwakuwa walikosa chochote kitu katika mgao wa milioni 700 zinazotajwa kumwagawa huko meru kumuwezesha sioy kushinda kwa kishindo.
 
Usipungukiwe umakini hivyo mkuu!
Kwa mfano, Lipumba aliposhinda kuwa mgombea urais ndani ya CUF, ni wapiga kura wa Tanzania waliompitisha kwa kishindo???
Tofautisha chama na taifa!
 
leo nimepata fursa ya kuongea na baadhi ya wananchi wa arumeru mashariki,wengi wanaonekana kuchukizwa na kitendo cha ccm kumsimamisha ndugu siyoi sumari kama mgombea wake.
Sababu kubwa zinazotajwa ni pamoja na:
siyoi sio mkazi wa arumeru
siyoi hajui kimeru(hata salamu)
siyoi amekosa utu,kwani ni wiki chache baada ya mzee wake kututoka mtoto anaingia kwenye kinyang'anyiro cha uchaguzi.
Pia hawapendezi kuendelea kuongozwa kisultani.
Fedha nyingi(karibu milioni mia saba) zimetumika kumpitisha.
Wameru wamesema wao ndio wenye uamuzi wa mwisho na hawategemei fedha kushinda nguvu ya umma.

Sijui hasira za wananchi hawa zitaamua nini lakini huu ndio msimamo wao.
yaani we umetumwa na zoezi lako limefail kabisa hayo uliyosema ni kinyume sababu siyoi ni mkaazi halali wa arumeru
siyoi anajua limeru kama uji na mgonjwa mahututi
siyoi ana utut sana na ndio mana waanchi wamemsima,isha kuwatoa nishai magamba
kazi kwenu sasa magambaaa
 
Naomba mwenye cv zao aziweke hapa ili tujue uwezo wao wa elimu .
 
Mapenzi mabaya sana Aisee! Sasa mie kujenga hoja kupingana na maneno ya muanzisha hii thread unaniambia na ropoka..

Jamaa yako anasema Siyoi sio mkazi wa Arumeru.

Siyoi hajui Kimeru.

Siyoi amekosa utu.

Siyoi katumia milioni 700..

Sasa hapa sijui nani karopoka au haya maneno maneno unayapenda sababu yanakuliwaza.

Mkuu ushauri wako huu umejaa chuki badalika.
ritz usinichukie mimi haya ni maneno ya wameru.nenda kwenye kampeni ujionee mambo yalivyo!
 
Back
Top Bottom