Rungu la Kikwete lamwokoa Siyoi Sumari Kamati kuu. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Rungu la Kikwete lamwokoa Siyoi Sumari Kamati kuu.

Discussion in 'Chaguzi Ndogo' started by Molemo, Mar 5, 2012.

 1. M

  Molemo JF-Expert Member

  #1
  Mar 5, 2012
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 13,287
  Likes Received: 580
  Trophy Points: 280
  USHINDI wa Siyoi Sumari kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, unadaiwa kuitesa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, baada ya baadhi ya wajumbe kukuna vichwa kuhusu mbinu na mikakati ya kutengua ushindi alioupata katika duru ya pili dhidi ya William Sarakikya.

  Katika Mkutano Mkuu wa jimbo hilo uliofanyika, Februari 20 ulimchagua Siyoi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361, akifuatiwa na Sarakikya aliyepata kura 259. Hata hivyo, CC ya CCM iliyoketi Februari 27, iliagiza kurejewa kwa upigaji kura kati ya wagombea hao.
  Katika duru hilo la pili la uchaguzi uliofanyika Machi Mosi mwaka huu, Siyoi alipata ushindi wa kishindo wa kura 761 na kumtupa mbali mpinzani wake, Sarakikya aliyepata kura 361.

  Juzi katika kikao hicho cha CC, ushindi huo wa mara ya pili wa Siyoi uliipasua tena kamati hiyo kuu yenye mamlaka ya juu ya uamuzi ndani ya chama hicho, baada ya baadhi ya wajumbe kudaiwa kutaka atoswe na apitishwe Sarakikya kutokana na tuhuma za matumizi makubwa ya fedha wakati wa kampeni.

  Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka katika kikao hicho cha CC, vilifafanua kwamba waliosimama kidete kutaka Siyoi atoswe ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira.

  Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Nape alipinga Siyoi kurejeshwa akizingatia matukio mbalimbali ya tuhuma za matumizi makubwa ya fedha yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya watu ili wamchague mgombea huyo, kitu ambacho hakikupaswa kuvumiliwa.

  Hoja hiyo ya Nape iliungwa mkono na Wassira ambaye naye alitaka Siyoi atoswe kutokana na tuhuma hizo za matumizi makubwa ya fedha kutoka kwa baadhi ya wapambe wake waliotaka mgombea huyo achaguliwe.

  Lakini inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kikao hicho kisingeweza kumkata Sumari kwa sababu tu ya tuhuma hizo za rushwa zilitolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani humo.

  Chanzo kingine kilimnukuu mwenyekiti huyo akisema kwamba, Arusha ni mkoa wenye siasa za aina yake hivyo ni muhimu kuwa makini kwani siku za nyuma kuliwahi kuibuka tuhuma za rushwa kwa wabunge wa CCM kukamatwa lakini, mahakama ikawaachia huru.

  Chanzo hicho kiliongeza kwamba, Rais Kikwete alisisitiza kuwa hata tuhuma za rushwa zilizotolewa zilikuwa zikigusa wengine kwani iliwahi kupendekezwa kwamba Elishalia Kaaya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), ndiye apitishwe na wengine wang'olewe.

  Katika kikao hicho, Rais Kikwete pia alinukuliwa akihoji kuwa endapo Siyoi angekatwa jina kungekuwa na uhakika wa chama kushinda kwa kumsimamisha Sarakikya? Hakupata jibu kama mgombea huyo wa pili angeweza kushinda kiti hicho.

  Hata hivyo, chanzo hicho kilisema baada ya mwenyekiti kutumia rungu kumpitisha Siyoi alimpa angalizo: "Basi na wewe usiende kutamba huko mitaani kwamba umeangusha watu, fanya kampeni, ushinde jimbo tuangalie mambo mengine mbele."

  Ilielezwa zaidi kwamba Rais Kikwete aliungwa mkono na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, aliyeeleza kuwa haoni sababu ya kumwondoa Siyoi katika kinyang'anyiro hicho kwani ushindi wake ulikuwa mkubwa.

  SOURCE:MWANANCHI
   
 2. Mag3

  Mag3 JF-Expert Member

  #2
  Mar 5, 2012
  Joined: May 31, 2008
  Messages: 9,094
  Likes Received: 6,188
  Trophy Points: 280
  Kikwete na Lowassa hawakukutana barabarani!
   
 3. Emmani

  Emmani JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 27, 2012
  Messages: 525
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hii inadhihirisha kwamba ndani ya CCM kutoa rushwa si haram!
   
 4. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Rais na Mwenyekiti wa Chama anapotetea na kushinikiza mtoa rushwa apitishwe kugombea ubunge tutazamie nini katika serikali yake? Jibu amehalalisha rushwa katika serkali yake.
   
 5. Feedback

  Feedback JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Mar 14, 2011
  Messages: 7,944
  Likes Received: 358
  Trophy Points: 180
  Mzee si kwamba Kikwete amependa iwe hivyo ila amelazimika.
   
 6. RICH OIL SHEIKH

  RICH OIL SHEIKH JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Jan 2, 2012
  Messages: 882
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  JK - makini kabisa
   
 7. Kiona

  Kiona JF-Expert Member

  #7
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 3, 2012
  Messages: 936
  Likes Received: 9
  Trophy Points: 35
  Na bado watatapatapa sana.

  Chadem anaibuka kidedea.
   
 8. S

  Shembago JF-Expert Member

  #8
  Mar 5, 2012
  Joined: Aug 20, 2011
  Messages: 332
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Unatazamia nini kwa magamba jamani? Huwa nivituko na miuzauza!
   
 9. Komeo

  Komeo JF-Expert Member

  #9
  Mar 5, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 2,393
  Likes Received: 423
  Trophy Points: 180
  Du! Siri za CC zimevuja tena! Kazi kweli kweli.
   
 10. p

  punainen-red JF-Expert Member

  #10
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 18, 2010
  Messages: 1,735
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 0
  Hakuna siku nguruwe-pori ataacha kuchimba kwenye matope akakae juu ya mwamba mkavu na msafi. Nguruwe-pori na uchafu ni sawasawa na ccm na uchafu wa kila aina.Anayetegemea uadilifu kutoka ccm awahi akapimwe akili.
   
 11. Wambandwa

  Wambandwa JF-Expert Member

  #11
  Mar 5, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 2,240
  Likes Received: 337
  Trophy Points: 180
  Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama cha magamba ana roho ngumu kuliko ya paka shume. Kila kukicha anagonga mwamba kwenye chama chake.
  Kashindwa (kaangukia pua) vita ya kuwavua gaadi.mba mafisadi, na sasa bado anapigana vita anayoshindwa, si aondoke huko akafufue CCJ yake? Huko atakuwa huru kurusha madongo ya kuwapiga mafis
   
 12. DOUGLAS SALLU

  DOUGLAS SALLU JF-Expert Member

  #12
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 11,584
  Likes Received: 4,692
  Trophy Points: 280
  CCM na rushwa ni kama mkono wa kushoto na masaburi.
   
 13. TUJITEGEMEE

  TUJITEGEMEE JF-Expert Member

  #13
  Mar 5, 2012
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 10,776
  Likes Received: 2,676
  Trophy Points: 280
  Takrima imerudishwa Kimya kimya, mkuu.
   
 14. Mtumishi Wetu

  Mtumishi Wetu JF-Expert Member

  #14
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 4,984
  Likes Received: 425
  Trophy Points: 180
  nasikia eti huyo dogo sioi katoboa sikio, waliye karibu naye tujuze?????????kama ni kweli tanzania tuko elekea sio kuzuri!!!!!!

   
Loading...