JK alikiidangaya kikao cha CC ili kumuokoa Siyoi kwa lengo la kumlinda na tuhuma za rushwa

Zak Malang

JF-Expert Member
Dec 30, 2008
5,404
234
Wadau:


Nawasilisha mada hii na vielelezo ktk kubainisha kuwa Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete aliidanganya Kamati Kuu ya chama chake (CC) iliyokutana juzi chini ya uenyekiti wake kwamba wabunge wawili wa CCM wa mkoa Arusha waliofikishwa mahakamani kwa kosa la kutoa rushwa kwa wajumbe wakati wakigombea nafasi za uongozi katika chama hicho mwaka 2007 waliachiwa na mahakama.

CC iliketi kupitisha jina la mgombea wa CCM kiti cha Ubunge Arumeru Mashariki. Kauli ya JK iko katika gazeti la Mwananchi leo katika stori hapa chini na nimeihighlight kwenye red.

Kauli hiyo ya JK si sahihi. Ukweli ni kwamba Wabunge husika - Michael Lekule Laizer wa Longido na Elisa David Mollel wa Arumeru Magharibi hawakuachiwa na mahakama, bali kilichotokea ni kwamba upande wa mashitaka – yaani TAKUKURU, waliifuta kesi kwa kile kilichodaiwa kutokuwepo ushahidi wa kutosha. Angalia stori chini kabisa iliyotoka katika gazeti la Arusha Times la tarehe 12 – 18 Julai 2008.

Kufuta kesi, au kuiondoa kesi mahakamani siyo kwamba waliachiliwa na mahakama kwa ‘kutopatikana na hatia' au kushinda kesi, bali ni kwa matakwa ya serikali, na mara nyingi hufanya hivyo kwa kuangalia masilahi yake (serikali na chama chake) na si kwamba kulikuwa hakuna jinai iliyotendeka.

Hivyo ni dhahiri JK alidanganya kamati yake (CC) na lengo kuu ni kufumbia macho tuhuma za rushwa katika chama chake ili kumuokoa Siyoi.

Ni vigumu kuupiga vita ufisadi chini ya JK, anaonekana ni kikwazo kikubwa.

Nawasilisha.


_________________________

Rungu la Kikwete lilimwokoa Siyoi



* NAPE, WASSIRA WADAIWA KUSIMAMA KIDETE ATOSWE, JK AKATUMIA 'RUNGU' KUZIMA HOJA,WABUNGE WOTE CHADEMA KUHAMIA ARUMERU

Joseph Zablon, Dar na Moses Mashalla, Arusha

USHINDI wa Siyoi Sumari kupeperusha bendera ya CCM katika uchaguzi mdogo wa Jimbo la Arumeru Mashariki, unadaiwa kuitesa Kamati Kuu (CC) ya chama hicho, baada ya baadhi ya wajumbe kukuna vichwa kuhusu mbinu na mikakati ya kutengua ushindi alioupata katika duru ya pili dhidi ya William Sarakikya.

Katika Mkutano Mkuu wa jimbo hilo uliofanyika, Februari 20 ulimchagua Siyoi ambaye ni mtoto wa aliyekuwa Mbunge wa jimbo hilo, marehemu Jeremiah Sumari kwa kura 361, akifuatiwa na Sarakikya aliyepata kura 259. Hata hivyo, CC ya CCM iliyoketi Februari 27, iliagiza kurejewa kwa upigaji kura kati ya wagombea hao.

Katika duru hilo la pili la uchaguzi uliofanyika Machi Mosi mwaka huu, Siyoi alipata ushindi wa kishindo wa kura 761 na kumtupa mbali mpinzani wake, Sarakikya aliyepata kura 361.


Juzi katika kikao hicho cha CC, ushindi huo wa mara ya pili wa Siyoi uliipasua tena kamati hiyo kuu yenye mamlaka ya juu ya uamuzi ndani ya chama hicho, baada ya baadhi ya wajumbe kudaiwa kutaka atoswe na apitishwe Sarakikya kutokana na tuhuma za matumizi makubwa ya fedha wakati wa kampeni.

Vyanzo vya habari vya kuaminika kutoka katika kikao hicho cha CC, vilifafanua kwamba waliosimama kidete kutaka Siyoi atoswe ni Katibu wa Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Uhusiano na Uratibu), Stephen Wassira.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo, Nape alipinga Siyoi kurejeshwa akizingatia matukio mbalimbali ya tuhuma za matumizi makubwa ya fedha yaliyokuwa yakifanywa na baadhi ya watu ili wamchague mgombea huyo, kitu ambacho hakikupaswa kuvumiliwa.

Hoja hiyo ya Nape iliungwa mkono na Wassira ambaye naye alitaka Siyoi atoswe kutokana na tuhuma hizo za matumizi makubwa ya fedha kutoka kwa baadhi ya wapambe wake waliotaka mgombea huyo achaguliwe.

Lakini inadaiwa kuwa Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete alisema kikao hicho kisingeweza kumkata Sumari kwa sababu tu ya tuhuma hizo za rushwa zilitolewa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), mkoani humo.

Chanzo kingine kilimnukuu mwenyekiti huyo akisema kwamba, Arusha ni mkoa wenye siasa za aina yake hivyo ni muhimu kuwa makini kwani siku za nyuma kuliwahi kuibuka tuhuma za rushwa kwa wabunge wa CCM kukamatwa lakini, mahakama ikawaachia huru.

Chanzo hicho kiliongeza kwamba, Rais Kikwete alisisitiza kuwa hata tuhuma za rushwa zilizotolewa zilikuwa zikigusa wengine kwani iliwahi kupendekezwa kwamba Elishalia Kaaya ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Mikutano cha Kimataifa Arusha (AICC), ndiye apitishwe na wengine wang'olewe.

Katika kikao hicho, Rais Kikwete pia alinukuliwa akihoji kuwa endapo Siyoi angekatwa jina kungekuwa na uhakika wa chama kushinda kwa kumsimamisha Sarakikya? Hakupata jibu kama mgombea huyo wa pili angeweza kushinda kiti hicho.

Hata hivyo, chanzo hicho kilisema baada ya mwenyekiti kutumia rungu kumpitisha Siyoi alimpa angalizo: "Basi na wewe usiende kutamba huko mitaani kwamba umeangusha watu, fanya kampeni, ushinde jimbo tuangalie mambo mengine mbele."

Ilielezwa zaidi kwamba Rais Kikwete aliungwa mkono na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu na Bunge), William Lukuvi, aliyeeleza kuwa haoni sababu ya kumwondoa Siyoi katika kinyang'anyiro hicho kwani ushindi wake ulikuwa mkubwa…………..

Chanzo: Mwananchi

___________________________


Euphoria as MPs are cleared of corruption charges

By Edward Selasini

The two Members of Parliament from Arusha region, Michael Lekule Laizer of Longido constituency and Elisa David Mollel of Arumeru-West have hailed their being set free saying that they were determined to continue serving their people.

The two who were alleged to have offered bribes in last year's CCM leadership elections, along with nine other CCM members, so as to influence voters.


MP Laizer said they had lost a lot of the public precious time in a case that had to be withdrawn by the anti corruption bureau for lack evidence to support their allegations. The withdrawal of the charges, he said, has however cleansed them of the smear and mud-slinging campaign.

MP Mollel said he hadn't been asked a single question at the court throughout the time of his numerous appearances in court.

Others who have been cleared are Daniel Porokwa, CCM Regional Youth Chairman; John Pallangyo and Abraham Zellote Kaaya, Regional and District CCM Representatives.

Others were Emmanuel L. Laizer, Ndewirwa Mbise, Nkoaranga village executive officer (VEO) and CCM national and regional representative; Charles Akyoo, ward executive officer (WEO) for Usa River ward and Abubakar Shakalaghe, CCM ward publicity secretary, Usa River ward.

The Resident Magistrate at Arusha Resident Magistrate's Court George Ndabagoye set them free after the anti corruption bureau had withdrawn the charges.

The announcement saw relatives, friends and supporters explode in euphoria.

Chanzo: Arusha Times (July 12 – 18 2008)
 
Umetoa mada wewe mwenyewe nahukumu ni umetoa wewe mwenyewe sasa unataka sisi tuchangie nini?
 
Sisiem inayumba na itaendelea kuyumba, chama kushikwa na mtu mmoja au wawili ni makosa makubwa ambayo yataipeleka ccm jehanamu!
 
Duh! Kaka huwa haujui kwamba JK ana tabia mbili mbaya katika uongozi wake? Hupenda kunyamaza kimya, lakini ikibidi kusema basi ni uongo tu! Nchi hii iko katika s*** kweli kweli!
 
Umetoa mada wewe mwenyewe nahukumu ni umetoa wewe mwenyewe sasa unataka sisi tuchangie nini?

Wewe magamba vipi? Mtoa mada hakutoa hukumu yeye! Katoa vielelezo kuonyesha uongo wa JK. Hebu niambie mkuu wa nchi anapodanganya kuhusu tukio la ufisadi si nchi imekwisha hii?
 
Kesho Nape atalazimishwa kutoa taarifa ya kukanusha nukuu hiyo ya JK katika Mwananchi. Lakini Nape anafahamu wazi kwamba vikao vya CC na CCM-NEC havina siri tena.

Wajumbe wanaongea ndani na nje watu wanasikiliza yote katika simu zao! Hii ilitokea katika kikao kile cha CCM-NEC kule Dom pale EL alipomnyooshea kidole JK kkuhusu Richmond na Mkapa akaibuka na kumuomba JK asitishe mjadala!

This is how CCM trudges along, na si JK au kiongozi mkuu mwingine yoyote wa CCM anayeonekana kuguswa na uvujaji huu wa mijadala ya vikao!
 
Mh!!!! Mie nafikira tu bado tunaye kwa miaka mingine minne ijayo! The mere thought of that brings nightmares! Sure it does!
 
JK anafikiri Watanzania hawana kumbukumbu. kesi ya wale wabunge haikusikilizwa na mahakama, waliachiwa baada ya serikali ya ccm kuwafutia mashitaka.

Wangelikuwa ni wabunge wa cdm...
 
ni kweli wale wabunge walifutiwa kesi na Takukuru na chanzo cha kesi ni ile ilikuwa njama za EL wakati huo akiwa Waziri Mkuu kuwazuia Lekule aliyekuwa anagombea uenyekiti wa mkoa ili mtu wake Onesmo Nangole (ambaye sasa ni mkiti wa CCM mkoa) ashinde kwa urahisi na pia kumzuia hasimu wake kisiasa Elisa Mollel asiwe mjumbe wa NEC. EL akitumia madaraka yake kama PM aliwaagiza Takukuru wawakamate wazee wale na kuwafungulia kesi na vikao vya juu vya chama chini ya Jk vikawazuia kugombea lakini baada tu ya uchaguzi kupita walifutiwa mashitaka na Takukuru.

Tangu wakati huo watu wengi wanahoji integrity ya taasisi hiyo
 
Back
Top Bottom