Sababu za walimu kukosa zoezi la sensa hizi hapa

meningitis

JF-Expert Member
Nov 17, 2010
8,349
4,674
Kumekua na tetesi kuwa walimu wengi wamekosa kushirikishwa zoezi la sensa kama ilivyozoeleka kisa ni kujihusisha na mgomo.
Ukweli niliopata kutoka kwa afisa mipango wa wilaya moja ni kwamba kuna ongezeko kubwa la graduates kutoka vyuo mbalimbali na form six leavers kutoka shule mbalimbali ambao wamechukua nafasi za walimu. Wengi wa haya makundi niliyotaja hawana ajira hivyo serikali imeamua kuwapa dili ili wajikimu kimaisha japo kwa muda mfupi.
 
kama kuna ukweli ni sawa ingawa inaonekana kwamba kulikuwa na beef flani kwa siri-kali dhidi ya walimu baada ya mgomo ikabidi wawatemeshe hilo dili
 
Hilo linafahamika, lakini sio sababu tosha, hiyo ni sababu ya kiofisi, tulioko huku twajua zaidi ya hizo story za mtaani
 
kama kuna ukweli ni sawa ingawa inaonekana kwamba kulikuwa na beef flani kwa siri-kali dhidi ya walimu baada ya mgomo ikabidi wawatemeshe hilo dili

hakuna beef lolote.it was planned!
 
Serikali hiyo hiyo ilijua kwamba kuna wimbi la graduates na waliomaliza kidato cha sita ambao hawana kazi lakini ikaamua kufunga shule mapema kuwawezesha walimu kushiriki katika zoezi zima la sensa.
Kweli walimu waliorozeshwa na majina ya waliokubaliwa yakawekwa kwenye mbao za matangazo,sehemu nyingine wakawa wameanza semina kuhusiana na swala la sensa.
Ajabu walimu walioenguliwa ni wale walioshiriki mgomo hicho ni kitu kilichopangwa kwa minajiri ya kukomoana kuonyeshana ubabe na kulipiza visasi na kushikishana adabu kwa serikali 'sikivu' dhidi ya walimu.
 
Walimu hawakuenguliwa kwa bahati mbaya ilikuwa ni mpango hasa mara baada ya mgomo kutokea. Mpango wa kufunga shule ni kwa sababu ilikuwa planned kwamba walimu ndio watahusika kwenye zoezi hivyo wanafunzi wasingepata muda wa kukaa mashuleni na walimu wao kwa ajili ya masomo.

Naamini kama ungekuwa ndio mpango wa serikali tangu awali kutokuwashirikisha walimu wasinge thubutu kupanga kuwanyima watoto haki yao ya kufundishwa. Wangetangaza mapema kuwa walimu hawata husika kwa kuwa kuna graduates na form six leavers mtaani ambao ndio watahusika kwa 100%.

Naamini kwa utaratibu huu mpya wa kuanza kuwa ignore walimu utaendelea mpaka kwenye kusahihisha na kutunga mitihani. Serikali ifanye kama ilovyofanya kwenye mitihani ya kidato cha pili, nne, sita na darasa la saba.
 
huo ni uhuni wa serikali wala hakuna kusema kunawimbi la form VI au graduate wengi mitaani. serikali dhaifu huzaa maamuzi dhaifu wasubiri 2015 kama watawaweka hao graduate waone nini kitatokea maana hawa hawanunuliki au hawahongeki
 
Sisi tupo walimu 35 hakuna aliyechaguliwa sensa, sasa je kulikuwa na lazima gani kufunga shule? Kweli nchi hii ni ya mfalme juha.
 
Unalosema inaweza kuwa moja ya sababu. Ila mbona serikali imebadili muda wa kufungua mashule sababu ya sensa? Pia si kweli kuwa Magraduate wapo accessible na wametawanyika vizuri nchi nzima kama walimu. Hapo sababu kubwa itabaki kuonekana ni KISASI tu, tusubiri 2015 utashangaa mengine.
 
WAACHE MASIKHARA KUNA STD 7 UMEWAACHA KWENYE HILO KUNDI NA ZAIDI UNDUGU NA UBINAFSI NDIO ULIO JAA KWENYE UTEUZI WA MAKARANI:flypig:
 
Hili hata huitaji kujiuliza maswali mengi,zaidi ya kisasi kwa walimu sababu ya mgomo
 
Binafsi siungi mkono hiyo hoja,lkn nawashauri walimu kuachana na mambo yanayorudisha nyuma mshikamano. Huu ulikuwa wakati mzuri wa kuanza kuachana na shughuli ambazo zitafanywa na hao wengine km uchaguzi, kampeni mbalimbali nk.

Naamini km malipo ya sensa yangekuwa elfu kumi kwa siku walimu wangetumika lkn kwa kuwa malipo ni tofauti ndio maana wapo maafisa wamesafirisha ndugu zao mikoa mbalimbali kwenye hili zoezi. Pia inasemekana wapo baadhi ya washiriki wanasubiri walipwe pesa waishie zao kwani zoezi ni gumu.

All in all tunawatakia mafanikio mema ili zoezi likamilikel
 
Binafsi siungi mkono hiyo hoja,lkn nawashauri walimu kuachana na mambo yanayorudisha nyuma mshikamano. Huu ulikuwa wakati mzuri wa kuanza kuachana na shughuli ambazo zitafanywa na hao wengine km uchaguzi,kampeni mbalimbali nk. Naamini km malipo ya sensa yangekuwa elfu kumi kwa siku walimu wangetumika lkn kwa kuwa malipo ni tofauti ndio maana wapo maafisa wamesafirisha ndugu zao mikoa mbalimbali kwenye hili zoezi. Pia inasemekana wapo baadhi ya washiriki wanasubiri walipwe pesa waishie zao kwani zoezi ni gumu. All in all tunawatakia mafanikio mema ili zoezi likamilikel

hili ni somo muhimu sana kwa walimu.hasa ukizingatia kwa miaka kadhaa wamekuwa wakikwamisha juhudi za watanzania kujikomboa.naona uswahiba wa walimu na ccm umeanza kufikia kikomo
 
na wategemee matokeo mabovu ya sensa..hii kazi ya kushed c mchezo..na kundi pekee ambalo lingeweza kuifanya kwa ufanisi ni walimu..tuliopo huku tunajionea vituko juu ya vituko..watu vichwani hamna kitu mnawapa kazi ya kwenda kuhoji idadi ya watu. I do believe zoezi hili bila ya watu makini litakuwa na madoa mengi
 
hamna ukweli wowote hapo! kwanza kwa sasa wle tuliotoka vyuo wengi tumekimbia zoezi zima la sensa baada ya watu mbalimbali kupata tempo na ajira sehemu mbalimbali.
 
hamna ukweli wowote hapo! kwanza kwa sasa wle tuliotoka vyuo wengi tumekimbia zoezi zima la sensa baada ya watu mbalimbali kupata tempo na ajira sehemu mbalimbali.

sensa ni mojawapo ya tempo ndugu yangu.
 
na wategemee matokeo mabovu ya sensa..hii kazi ya kushed c mchezo..na kundi pekee ambalo lingeweza kuifanya kwa ufanisi ni walimu..tuliopo huku tunajionea vituko juu ya vituko..watu vichwani hamna kitu mnawapa kazi ya kwenda kuhoji idadi ya watu. I do believe zoezi hili bila ya watu makini litakuwa na madoa mengi

karibu sana JF.najua walimu wengi mmeumizwa na uamuzi huu lakini ni lazima mkubali matokeo kuwa ccm imeshawatupa na muache kujipendekeza
 
Walimu hawakuenguliwa kwa bahati mbaya ilikuwa ni mpango hasa mara baada ya mgomo kutokea. Mpango wa kufunga shule ni kwa sababu ilikuwa planned kwamba walimu ndio watahusika kwenye zoezi hivyo wanafunzi wasingepata muda wa kukaa mashuleni na walimu wao kwa ajili ya masomo.

Naamini kama ungekuwa ndio mpango wa serikali tangu awali kutokuwashirikisha walimu wasinge thubutu kupanga kuwanyima watoto haki yao ya kufundishwa. Wangetangaza mapema kuwa walimu hawata husika kwa kuwa kuna graduates na form six leavers mtaani ambao ndio watahusika kwa 100%.

Naamini kwa utaratibu huu mpya wa kuanza kuwa ignore walimu utaendelea mpaka kwenye kusahihisha na kutunga mitihani. Serikali ifanye kama ilovyofanya kwenye mitihani ya kidato cha pili, nne, sita na darasa la saba.

waalimu wameuwa ignored kvipi? na ni wangapi ambao wamepigwa chini kama walioomba? jamani sensa wanalipwa sh 30 kwa siku za semina ambayo ni sawa na 360000/= kwa 12 . siku ya sensa yenyewe wanalipwa kama sh 200000/= na kitu so ukisum up ni kama 600000/= hazizid hapa. sasa nauliza kweli hizi laki 6 ndo zitutoe nyongo waalim hadi tuonekane kama tumekuwa ignored?

istoshe waalim wengi walioomba wamechukuliwa ila tu kumewekwa uwiano kati ya shule na shule manake kuna shule wamechukua waalim kama 20 hivi hawajazidi hapo sasa sijui kwanini ionekane kama ni ishu ya kujadiliwa hadi tusemwe tumedharauliwa ama mitihan watatunga wao nk. nijuavyo mmi mtihani anayetunga ni qualified person na sisi waali huwa tunatuma maaswali tu wataalam wa mitihani kutoka kila somo ndio huwa wanacompile na kuyafanyia moderation na kutengeneza table of specification sasa sjui haya ni yepi ambayo yametokea kwa mitihan. marking lazima waende waalim wa masomo ambao wako competent.
 
huo ni uhuni wa serikali wala hakuna kusema kunawimbi la form VI au graduate wengi mitaani. serikali dhaifu huzaa maamuzi dhaifu wasubiri 2015 kama watawaweka hao graduate waone nini kitatokea maana hawa hawanunuliki au hawahongeki

Ni kweli mkuu dawa yao nikuongeza idadi ya zero tu kwenye kila matokeo vii f4 f6
 
Back
Top Bottom