Sababu za walimu kukosa zoezi la sensa hizi hapa

huo ni uhuni wa serikali wala hakuna kusema kunawimbi la form VI au graduate wengi mitaani. serikali dhaifu huzaa maamuzi dhaifu wasubiri 2015 kama watawaweka hao graduate waone nini kitatokea maana hawa hawanunuliki au hawahongeki

Kwahiyo mkuu unatakutuambia huwa walimu ununuliwa wakati wa UCHAGUZI?
 
Naona tatizo kwa huku,ni undugunaizesheni.Watu wamebebana kipuuzi puuzi,mpaka ninapoandika hapa kuna Cashier mmoja yupo cello,kisa,amepata los baada ya makarani kuwazidishia ela.BADALA YA LAKI 2 AMEWAPPA LAKI 4.
 
hili ni somo muhimu sana kwa walimu.hasa ukizingatia kwa miaka kadhaa wamekuwa wakikwamisha juhudi za watanzania kujikomboa.naona uswahiba wa walimu na ccm umeanza kufikia kikomo

Hebu fafanua vizuri na kwa ufasaha kabisa ni jinsi gani walimu kwa miaka kadhaa wamekuwa wakikwamisha juhudi za watanzania kujikomboa?

Kuwepo au kutokuwepo kwa uswahiba wa walimu na CCM umetokana na utashi wa walimu wenyewe.Huwezi kulazimisha urafiki.Lakini kumbuka rafiki katika shida ndiye rafiki wa kweli.Tabia binafsi kama kulipiza kisasi hazitakiwi kufanywa na viongozi katika jamii. Tunao viongozi wenye tabia hizo na wanafahamika.Walimu wasikatishwe tamaa kwa kufutwa majina yao, wawe na umoja katika kutafuta haki yao. PEACE AND LOVE.
 
Juzi nimekutana na karani mmoja wa sensa nikawa namchukua maelezo kuhusu uelewa wake kuhusu zoezi zima la sensa,aiseee nilichoka inaonesha yuko kimasilahi zaidi,eti bora liende,labda ni kweli bora walimu wangepewa priority ya kwanza!
 
Kumekua na tetesi kuwa walimu wengi wamekosa kushirikishwa zoezi la sensa kama ilivyozoeleka kisa ni kujihusisha na mgomo.
Ukweli niliopata kutoka kwa afisa mipango wa wilaya moja ni kwamba kuna ongezeko kubwa la graduates kutoka vyuo mbalimbali na form six leavers kutoka shule mbalimbali ambao wamechukua nafasi za walimu. Wengi wa haya makundi niliyotaja hawana ajira hivyo serikali imeamua kuwapa dili ili wajikimu kimaisha japo kwa muda mfupi.


Labda ile slogan ya "Ari mpya, Kasi mpya na Nguvu mpya", ndiyo kidogo imeanza kufanya kazi! Tusisahau tulipewa ahadi ya maisha bora (nchi ya asali na maziwa) kwa kila Mtanzania.Sisi watanzania ni watu wa ajabu sana! Mara nyingi tumekuwa tukipewa ahadi hewa na kuridhika bila kutekelezewa.Sasa leo tunapakwa mafuta kwa mgongo wa chupa kwa kupewa ajira za muda tunafurahi kwa kuwacheka walimu waliofutwa katika orodha ya makarani wa sensa! Kumbuka mwenzio akinyolewa wewe unatakiwa kutia maji kichwa chako.Maswala ya sensa,vitambulisho vya uria na mambo mengine nyeti yanahitaji umakini mkubwa sana.

Serikali itafute dawa ya matatizo ya ajira/waajiriwa na sio kutoa ajira za muda ili kufunika kombe,mwanaharamu apite. Kama kweli waliotakiwa kufanya kazi za sensa ambao wengi wao walikuwa ni walimu waliotahiniwa na baadaye kupewa semina elekezi juu ya taratibu zote za sensa na kufutwa,hawa wapya hawa waliowekwa wamepewa lini semina elekezi juu ya sensa? Kuna umakini kweli hapa? MAMA YANGU TANZANIA.
 
hili ni somo muhimu sana kwa walimu.hasa ukizingatia kwa miaka kadhaa wamekuwa wakikwamisha juhudi za watanzania kujikomboa.naona uswahiba wa walimu na ccm umeanza kufikia kikomo

mkuu walimu hawahusiki na hilo, usiwapake matope!
 
Kumekua na tetesi kuwa walimu wengi wamekosa kushirikishwa zoezi la sensa kama ilivyozoeleka kisa ni kujihusisha na mgomo.
Ukweli niliopata kutoka kwa afisa mipango wa wilaya moja ni kwamba kuna ongezeko kubwa la graduates kutoka vyuo mbalimbali na form six leavers kutoka shule mbalimbali ambao wamechukua nafasi za walimu. Wengi wa haya makundi niliyotaja hawana ajira hivyo serikali imeamua kuwapa dili ili wajikimu kimaisha japo kwa muda mfupi.

Labda ile slogan ya "Ari mpya,nguvu mpya na Kasi mpya" kidogo ndiyo imeanza kufanya kazi.Kumbuka tulipewa ahadi ya maisha bora(nchi ya ahadi yenye maziwa na asali) kwa watanzania wote.Sisi Watanzania ni watu wa ajabu sana! Tumekuwa ni watu wa kupewa ahadi zisizotekelezwa na ghafla tunasahau yaliyopita na kuibuliwa mengine(ahadi) mapya kabisa!

Leo tunawacheka walimu kwa kupokwa kazi waliyoahidiwa,wakatahiniwa na kupewa semina elekezi kuhusu sensa. Japo kila mtu/watu mwenye sifa na si mwalimu/walimu peke yake/yao mwenye haki ya kuwa karani/makarani wa sensa,je ni hasara au gharama(kodi ya watanzania) kiasi gani itakuwa imepotea baada ya kutumika katika mafunzo ya namna ya kufanya na kusimamia zoezi la sensa na kisha kuwafuta waliopewa elimu hiyo? Walimu waimeshanyolewa na sisi wengine akina yakhe tunatakiwa kutia maji vichwa vyetu.Hawa wengine hawa wanaosemekana kuchukua nafasi za walimu katika kufanya kazi wakati wa sensa wamepewa semina elekezi lini hawa? Jamii yetu inatakiwa kuwa na watu/viongozi walio na uchungu na nchi yao kwa kutatua shida mbalimbali kwa kusikilizana na kwa upendo wa dhati. Umakini mkubwa sana unatakiwa katika zoezi lote la uandikishaji sensa na vitambulisho vya uraia. MUNGU IBARIKI TANZANIA. :A S cry:
 
Nawashukuru wachangiaji wenzangu waliopita.kwa mtazamo wangu, serikali ya CCM ndo ipo kwenye utekelezaji wa ilani ya chama ya kutengeneza ajila million moja ambazo iliahidi wakati wa kampeni 2010 hivyo basi hao magradute na six leavers ndo wameshapata ajila wasitegemee tena ajila nyingine hadi miaka kumi ijayo kutakapo kuwa na sensa nyingine kama serikali sikivu itakuwa madarakani.
 
Nawashukuru wachangiaji wenzangu waliopita.kwa mtazamo wangu, serikali ya CCM ndo ipo kwenye utekelezaji wa ilani ya chama ya kutengeneza ajila million moja ambazo iliahidi wakati wa kampeni 2010 hivyo basi hao magradute na six leavers ndo wameshapata ajila wasitegemee tena ajila nyingine hadi miaka kumi ijayo kutakapo kuwa na sensa nyingine kama serikali sikivu itakuwa madarakani.
 
Hivi walimu wana hati miliki ya shughuri hizi (sensa usimamizi wa uchaguzi nk.) Naipongeza serikali kuwapa kazi hi vijana wetu wanao shinda juani bila kazi wakati wamesoma. Kwanza walimu wanadai wnafanya kazi kubwa afu wanalipwa kidogo sasa serikali imesikia kilio chao ikawapunguzia mzigo wanalalamika eti wamekosa sensa. Sasa hamuoni kuwa serikali ni sikivu????????????
 
Kwani ni lazima wapewe walimu???? pengine huko nyuma kuliwa na ulazima huo lakini kwa sasa wasomi wa level tofauti wako nchi nzima na suala la kudodosa sensa haviko complicated.
 
Tuliopata sensa huku tanga wengi wanajua lilikuwa dili kuwaacha walimu mana kuna siri ilivuja ikabidi msimamizi wa sensa aseme iliandikwa kwa ajili ya walimu tu,kwa hyo kata hapo,na kwa hasira zaid darasa la saba watasimamia walimu wa sekondar mwakahuu kisa chanzo cha mgomo walimu wa msingi.
 
Ni kweli mkuu dawa yao nikuongeza idadi ya zero tu kwenye kila matokeo vii f4 f6

Kweli suala la Elimu hapa nchini duuhhhhh!!!!!!!!!!! .................. tunakomoana kuanzia sirikali mpaka na wewe???? Ama kweli kama elimu ni mkombozi basi sisi bado ni watumwa hivyo tujiandae kutawaliwa tuuuuuuuuuuu!!!
 
2 Reactions
Reply
Back
Top Bottom