Sababu za vegetarians kutokula nyama


afadhali hata hao kuliko wanaojifia kwa magonjwa ndugu yangu, unakuta lundo la nyama buku 3 tuu hapo kuna walakini
 
Buddhist monks wanavaa mashuka ya njano/orange (inasemekana bila kufuri?). Sijaahi kuona wakivaa viatu, sana sana malapa na mara nyingi huwa wanatembea pekupeku!

kuna baadhi wanakula na kuna baadhi hawali na sio hizo tu bali hata products kama mikanda, nguo, viatu na chochote kile ambacho kimetokana na kupotea kwa uhai wa kiumbe fulani
 
Mbona vitabu vitakatifu vinasema watu walikuwa wakimtolea mungu sadaka zakuteketeza( mostly wanyama) lkn mungu aliridhika nazo, pia mbona watu walikula nyama tangu enzi za uyahudi?

pia kumbuka hvyo vitabu ni kwa imani yako unaviamini, wengine wana imani tofauti na hawaamini hayo, tunatofautiana sana ktk suala la imani
 

na wewe ni monk?
 
afadhali hata hao kuliko wanaojifia kwa magonjwa ndugu yangu, unakuta lundo la nyama buku 3 tuu hapo kuna walakini

kikweli kama ni mizoga tunalishwa sana, mfano hawa wauza kuku, ikatokea bahati mbaya kuku wawili wakamfia kabla hajawachinja,sidhani kama atawatupa
 
Bahati mbaya imani zilizotangulia kuja Africa zimejenga "concervertism"miongoni mwa wanaozifuata kiasi cha kuogopa kujifunza nje ya box. Kimsingi Vegetarianism inasaidia body and soul ila imani zilizotangulia zime base kwenye soul zaidi.

Asante sana. Hayo maneno yapo too deep.

Halafu nadhani tatizo ni westerners. Ukiangalia monk wa kwanza kutoka western walianza miaka ya 1950's. Walikuja kujua umuhimu wa imani za kale very late maana walikuwa wanaona Asians uncivilized kama walivyotuona sisi waafrika. Na dhana zao na views zao mpaka leo zimeacha mizizi kwetu Afrika na kutufanya tusitoke nje ya BOX kujifunza mengi.

Ila zipo jamii Afrika walizoona meditation, beards, vyakula, n.k vina uhusiano katika kuishi kiimani.
 
Mbona vitabu vitakatifu vinasema watu walikuwa wakimtolea mungu sadaka zakuteketeza( mostly wanyama) lkn mungu aliridhika nazo, pia mbona watu walikula nyama tangu enzi za uyahudi?

tunajadili kwa imani nyingine, na si kuyakosoa maandiko matakatifu, na tunajua ni kwanini baada ya kifo cha Kristo Yesu sadaka za kuchinja wanyama zilikoma
 

Mkuu nataka kufanya hiyo nisaidie hatua zake....
 

Mkuu nimeshindwa kujaribu kukuelekeza juu ya baadhi ya Maisha ya Monks uliyoamini ndio monks wanaishi. Zipo video mbalimbali YouTube au tembelea BuddhaNet utapata vitabu na mafunzo mbalimbali.


Na kuhusu suala la Buddhist monks lazima wakate nywele nilijua lazima ungenibishia kuwa kukata nywele ni sheria, lakink sio wote hufanya hivyo na sio sheria. Inategemea na sect. Kama hujawahi kuona real Buddhist monks wenye nywele kawatafute monks wa Tibet wanaitwa Ngakpa. Ni monks asili yao ni Tibet. Hawakati nywele wala kuzichana kuashiria kuachana na image za kidunia kuwa lazima uwe na nywele zilizochanwa au nywele katika fashion fulani badala yake wanaacha nature ifanyike mpaka kichwani kwani nywele ni part ya mwili kama part nyingine. Buddhism haijasema nywele ni unlawful. Buddha alikata nywele zake kwa upanga na kuanza zikue upya kuashiria safari mpya ya kuwa Buddha baada ya enlightenment. Monks wengine hukata ili kuwa free kichwani hasa katika meditation na kuondoa self attachments. Na waweza ondoa au kijitenga na tamaa za attachments hata kwa kuziacha bila kuzichana. Kila mtu ana purpose yake.
 

Attachments

  • 1400410760840.jpg
    29.4 KB · Views: 104
  • 1400410781278.jpg
    55.5 KB · Views: 105
Mkuu nataka kufanya hiyo nisaidie hatua zake....

Natamani sana ningekusaidia ndugu Yangu. Sema sijawahi kumfundisha mtu nilijifunza mwenyewe kwa kusoma vitabu na baadaye nikawa naona videos YouTube, nikatafuta audios za instructions juu ya meditation. Mwanzo nilianza kujifunza kwa dakika 2, then 5 mpaka 20 na kuendelea. Zipo documents nyingi sana. Mwanzo wa kujifunza kuunganisha Mind yako na wewe inakuwa shida lakini taaratibu utaona mabadiliko.
 
Buddhist monks wanavaa mashuka ya njano/orange (inasemekana bila kufuri?). Sijaahi kuona wakivaa viatu, sana sana malapa na mara nyingi huwa wanatembea pekupeku!

kuna sect kuu 3 za buddhism ambazo ni Theravada,Mahayana na Vajrana. Theravada Wako ukanda wote wa Thailand, India, Mongolia hawa wanavaa mashuka ya njano na fundo lao liko kulia, hawavai viatu wala kufuli wananyoa kipara 2. Mahayana wao wako zaidi China, Taiwan Singapore Malaysia Indonesia sehemu mbalimbali ulimwenguni, hawa wanavaa sandal simple na nguo kama za shaolin temple ya china wananyoa vipara na kuna ordination ceremony ya kuunguzwa na mshumaa kichwani kila ukimaliza state fulani mashuka yao yanatofautiana rangi kutokana na rank, hawali nyama kabisa 3.Vajriyana wao wako linient kidogo wamechukua huku na kule wakachanganya pamoja, hawa hawana masharti magumu sana wanapractice middleway
 
Buddha alikata nywele?! Alikuwa na nywele kama za hawa wafuasi wake walizonazo leo hii?
Angalia "statue" zake zinanywele za aina gani! Endelea ku-Google ujue asili ya Buddha, japo wenyewe wanaoamini hiyo dini wanakataa....kwakuwa "hakuna kizuri kinachotoka Afrika"....

 
Nahisi utakuwa unazungumzia chuoni ufilipino!
Hata kama wanafundishwa kilimo lakini ni mwiko kwao kulima! Wao kazi yao ni kutoa huduma kwenye "temples" n.k

 
Nahisi utakuwa unazungumzia chuoni ufilipino!
Hata kama wanafundishwa kilimo lakini ni mwiko kwao kulima! Wao kazi yao ni kutoa huduma kwenye "temples" n.k

hapana mi nimekaa temple za Bronkhorspruit, Durban Souh Africa, Fo Kuang Shan Taipei Taiwan, Ipoh na Surabaya Malaysia ni hivi ukiwa monestry lazima ujifunze skills zote ila unapofikia hatua ya kuwa mtawa kamili ndio unahudumiwa na disciples hapa ndipo ambapo labda hatukuelewana
 
Hapa tumeelewana sasa. Asante sana. Wewe ni mwalimu mzuri.
Nikweli Monks (si wote) huwa wanafundisha jamii jinsi ya kuishi n.k. Kuna Monks mmoja ni kichwa wa IT!

 

Mhh. Ngoja turudi nyuma kidogo...

Mkuu Ukisema Buddha na Gautamaa ni mtu mmoja lakini state mbili tofauti. Gautama ni jina la Buddha, ambaye alikuwa ni prince Wa kingdom tajiri na baba yake alibahatika kuwa na mtoto mmoja tu, akampa kila kitu na raha zote. Jina lake lilikuwa ni Guatama. Lakini wazee wa kale wenye wisdom walimwambia kuwa Huyo mtoto atakuwa Buddha. Baba yake akabisha kwani hakupenda mtoto wake awe monk bali alitaka awe prince tajiri na kumpa raha zote za dunia ili asitamani kuwa monk. Baada ya Buddha kujifunza kuwa duniani kuna magonjwa, vifo na sufferings roho yake ikamfanya atamani kujua nini chanzo cha shida za dunia hii (mpaka hapa Buddha alikuwa na kijana mwenye nywele ndefu za fashion za kawaida).

Akaacha raha zote, akaondoka kwa baba yake bila kitu chochote kuanza safari ya kuutafuta ukweli wa maisha. Baada ya meditation na mafundisho aliyojifunza katika maisha akawa enlightened.

Nywele unazomuona nazo kwenye picha, na statues zake ni baada ya kuzikata nywele zake kwa upanga kuashiria new journey ya kuutafuta ukweli wa maisha.

Na unaposema wanaokataa hiyo dini sijajua unamaanisha nini. Fahamu kuwa Buddha alizaliwa katika kingdom iliyoaminika ni Asili ya Ethiopia. Kingine Buddhists hawana ubaguzi wa rangi juu ya waafrika. Please naomba usiwe mmbishi bali jaribu kuelewa.

N.B Buddha ni tittle au sifa na sio Gautama tu ndio Buddha. Buddha means the enlightened. Hata wewe waweza kuwa Buddha.

Mimi sio Buddhist, ni Rastafarian in beliefs lakini katika safari Yangu ya kujifunza mambo Buddha ni moja kati ya walimu wazuri ambao Hata Rastafarians wengu humsoma. Na sio Buddhists tu bali hata Hinduism, Judaism n.k tunasoma kuelewa vitu. Sitabisha nikiwa nimekosea. Wote tunajitahidi kuutafuta hivyo nami napenda kujifunza kwako kwani naamini sijui vyote. Let's listen to understand and not to question. Na tuache kuangalia maisha ya movies kujua vitu, visome na kaa na wenye imani hizo kujua kiundani.
 
Hapa tumeelewana sasa. Asante sana. Wewe ni mwalimu mzuri.
Nikweli Monks (si wote) huwa wanafundisha jamii jinsi ya kuishi n.k. Kuna Monks mmoja ni kichwa wa IT!

Asante tunaelimisha wote, unajua huu mjadala kuna kipindi tunajisahau tunachanganya maisha aishiyo layman/disciple anayeamini katika Buddha na mwanafunzi mtawa wa Buddhism
 

Safi sana.
 
Nimekuuliza yale mabutu/kipilipili kwenye "statue" zake zimewekwa kimakosa?
Usijeukasema mbele za wafuasi wa Buddha/Buddhism kwamba asili yake ni Ethiopia! Utapigwa mawe! Ndiyo maana niliandika ...."nothing good comes out of Africa"...

Hawa watu wanakataa ukweli lakini nenda kwenye statue za huyu mheshimiwa utakuwa karibu zote "pua" imegongwa! Ni bahati mbaya? Kwanini wamezigonga pua?

....kwahiyo Buddhism imetoka wapi?

 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…