Buddhist haifungi mtu suala la ulazima wa kula nyama. Ila kutokula nyama ni part ya Karma cleaning. Kuwa mfuatiliaji mzuri na msomaji mzuri. Other things Google can tell you. Buddha na monks wengi hawali nyama. Nyama tangu traditions inakuaminiwa ni karma mbaya na haikupi enlightment. Sio kila kitu Google. Nipe email kama unataka nikupe PDF ya Maisha na safari za Buddhists.
ni kweli lakini kumbuka ndani ya buddhism kuna seck nyingi na zinatofautiana kwenye mengi kuanziaa meditation, mavazi chakula na chanting kwa mfano buddhist wengi wa Japan wanakula nyama lakini kwa kiwango fulani, kwasababu maalum na si kama walavyo wengine kwa ulafi na hamu ya matamanio ya mwili
ni kweli lakini kumbuka ndani ya buddhism kuna seck nyingi na zinatofautiana kwenye mengi kuanziaa meditation, mavazi chakula na chanting kwa mfano buddhist wengi wa Japan wanakula nyama lakini kwa kiwango fulani, kwasababu maalum na si kama walavyo wengine kwa ulafi na hamu ya matamanio ya mwili
Hapa nazungumzia wale ambao hawali nyama kiimani na si wale ambao hawali kwasababu za kiafya tofauti na ukristo na uislam, dini kama buddhism, krishna nk wanaamini sana katika karma ya kila kiumbe na uwepo wake katika uso wa dunia, kwamba bata, mbuzi, samaki, punda na chochote chenye uhai kuna sababu maalum ya kuwa hivyo kilivyo.
Kwahiyo huwezi kutoa uhai wake kwa ajili ya shibe yako, utakuwa unajitengenezea karma mbaya, yani leo ukimuu mnyama ukala nyama yake next reincarnation yeye atazaliwa binadamu na wewe mnyama halafu atatenda kama wewe ulivyotenda imani hii imezama mno mioyoni mwao kiasi kwamba ni ngumu mno kuwakuta wanakula nyama. Kuna mazingira ambayo yanaweza kuwafanya wale nyama nayo ni
1.hawakushuhudia mnyama akichinjwa/akiuliwa
2. Hakuchinjwa kwa ajili yao
3. Isiwe ni nyama kwa ajili ya biashara, hapo anaweza kula na karma isimdhuru kila imani ina uchizi wake, kuna mavegetarian ambao kwa compassion kwa viumbe hufagia kabla ya kukanyaga ili wasiwadhuru viumbe
Sijakataa kuwa Buddhist hawali nyama.Rejea maneno niliyoweka "bold"....
Ukilinganisha na idadi ya "Buddhists", "Monks" ni wachache sana na wanakula nyama ya "kitimoto" n.k bila tatizo lolote. Wanafundishwa wasiombe kupewa chakula kizuri wanachopenda wao wenyewe bali wapokee chochote wanachopewa!!
Asubuhi na mapema "Monks" huwa wanajipanga kwenye makazi ya watu na wanapewa chakula...na ninakuhakikishia wanakula nyama, tena sana!
Vegetarians wanaweza wakala nyama, mayai na maziwa.
Vegans hawali wala kutumia kitu chochote ambacho ni product ya mnyama yoyote (hata samaki).
mh vegetarian wanaweza kula nyama, kivipi wanaweza kula nyama, kwani nilivoelewa vegetarian ni wasiokula nyama
Binafsi, tangu nilipokuwa mdogo nilikuwa sipendi sana kula nyama! Baadae likaja suala la dini. Nilikuja kuacha kabisa kula nyama ya aina yeyote ile kipindi fulani hivi wauza nyama walikuwa na tabia ya kuuza nyamafu!
Nimeipenda sana hii mada, inagusa vitu vingi na ufahamu mkubwa.
Heshima kwenu wote mnaokula nyama na msiokula nyama. Its our choice so big up to all.
nyamafu ndio nini mkuu,
Sijakataa kuwa Buddhist hawali nyama.
Na Sio monks wote huzunguka na kuomba vyakula kwa watu. Wapo ambao wanapanda mbogamboga na kujitegemea. Sijajua unazungumzia monks wa sects gani. Sawa na kusema monks wote hunyoa kipara wakati sio wote.
Kuwa monk mojawapo ya maisha yake ni kuachana na attachment za kidunia mfano kuchagua chakula, hilo ndilo fundisho kuu, sio kwamba una njaa halafu ukapewa nyama ya mtu aliyeuawa ukala kwa kusema uridhike na ulichonacho.
According to tradition vegetarian ndio msingi mkuu wa Circe of Rebirth.
Na monks wanaotafuta enlightment hawali nyama. Sio kwa Google bali kwa vitabu vya teachings za Buddha.
Kumbuka Buddha hakulazimisha watu kuishi kwa kutoua mnyama au kufuata maandiko yake, hivyo utofauti wa views haumaanishi ni kutokana na utofauti wa walimu. Mwalim mmoja views nyingi. Kila mtu ana choice yake.
Hivi vegeterian hao wanakula products za wanyama kama maziwa na mayai??
nyama mfu, kibudu au mzoga, kiumbe kilichokufa bila kufuata taratibu husika za uchinjaji
Hapo kwenye "bold" hakuna kitu kama hicho!!!
Monks halimi! Monks hapiki!
Kuna watu maalumu wanawapikia!
Monks wote huwa hawatoki kwenda kuomba chakula bali wanaenda nje sehemu maalumu wanasimama na jamii inaenda pale kuwapa chakula. Ni wajibu wa jamii japo si lazima. Jamii inaamini kuwapa chakula wanapata thawabu!!!
Sijawahi kuona "Monks" mwenye nywele!
Usisahau kwamba huwa kuna watu wanatumikia dini yao kwa muda wa miezi mitatu. Huwa ni mtu pengine ameoa, anakazi yake n.k ila anaenda kuishi maisha ya kimonki kwa muda huo mfupi tu! Usichanganye mkuu!