Kapyepye Mfyambuzi
JF-Expert Member
- Jun 18, 2020
- 542
- 924
Habari mkuu Mshana Jr naomba nisaidie tena hapa. (Samahani nimetoka nje ya mada)
Kuna website nimesoma inasema kwamba kukaa kwenye chumba cha giza bila kufumba macho (usiku) kila siku kunaamsha hali ya kiroho ya mtu. Wanadai ubongo utazowea na utaanza kubadilisha utoaji wa melatonin na serotonin ambayo huwa inatolewa wakati mtu amelala usingizi na kumfanya mtu huyo aote, ndio inaleta maono na hali ya ufahamu kwa mtu.
Je, Kuna Ukweli wowote kwenye hili hususani kwenye mambo ya spiritual awakening?

kupitia wewe nimekuwa napata elimu adimu na sio mchoyo wa maarifa kama wengine.