Sababu za serikali kuhamia Dodoma zabainika

tpaul

Platinum Member
Joined
Feb 3, 2008
Posts
27,205
Reaction score
27,841
Watu wengi watakuwa wanajiuliza itawezekanaje serikali hii kuhamia Dodoma ndani ya muda mfupi wakati serikali zote zilizopita, ikiwamo serikali ya muasisi wa makao makuu hayo, Mwalimu Julius Burito, zilishindwa kufanya hivyo. Aidha, kuna baadhi wanadhani huenda serikali inahamia Dodoma kama njia ya kumuenzi baba wa Taifa. La hasha! Imebainika sababu KUU ya serikali kuikimbia Dar es Salaam ni kuepuka aibu ya kuwa chini ya himaya ya UKAWA, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru wake mwaka 1960.

Kama mnavofahamu, serikali ya UKAWA ndiyo inayotawala jijini Dar es Salaam, baada ya kufanikiwa kunyakua umeya wa jiji na halmashauri mbili kati ya tatu za jiji. Dar es Salaam imekuwa ikiongozwa na CCM miaka nenda miaka rudi lakini katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo Waziri Mkuu mstaafu, Dr Edward Ngoyai Lowassa alikuwa mgombea kupitia UKAWA, CCM waliangukia pua. Hili jambo halikuwafurahisha viongozi wa CCM hata kidogo. Baada ya kutupa kete zao zote kulazimisha watawale jiji hili kukwama, sasa wamebakiwa na kete MOJA tu….kulikimbia jiji! Sasa mtu unaweza ukajiuliza: hivi siku UKAWA wakifanikiwa kutawala jiji la Dodoma, serikali itakimbilia wapi tena? Mbona serikali hii inakuwa na uoga wa kike kiasi hiki? Ni suala la kusubiri na kuona itakuwaje.
 
"...... Uoga wa kike kiasi hiki? " [emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23].
Mkuu kwan hujawah kuskia kale ka msemo "usiempenda kaja" lazima watafutane tu
 
huu ni ukweli mtupu

angalia walivyoikimbia arusha na sasa wanaikimbia Dar..

na tutawafuta 2020 tunawakimbiza dodoma
 
Watu wengi watakuwa wanajiuliza itawezekanaje serikali hii kuhamia Dodoma ndani ya muda mfupi wakati serikali zote zilizopita, ikiwamo serikali ya muasisi wa makao makuu hayo, Mwalimu Julius Burito, zilishindwa kufanya hivyo. Aidha, kuna baadhi wanadhani huenda serikali inahamia Dodoma kama njia ya kumuenzi baba wa Taifa. La hasha! Imebainika sababu KUU ya serikali kuikimbia Dar es Salaam ni kuepuka aibu ya kuwa chini ya himaya ya UKAWA, jambo ambalo halijawahi kutokea tangu nchi ipate uhuru wake mwaka 1960.

Kama mnavofahamu, serikali ya UKAWA ndiyo inayotawala jijini Dar es Salaam, baada ya kufanikiwa kunyakua umeya wa jiji na halmashauri mbili kati ya tatu za jiji. Dar es Salaam imekuwa ikiongozwa na CCM miaka nenda miaka rudi lakini katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana, ambapo Waziri Mkuu mstaafu, Dr Edward Ngoyai Lowassa alikuwa mgombea kupitia UKAWA, CCM waliangukia pua. Hili jambo halikuwafurahisha viongozi wa CCM hata kidogo. Baada ya kutupa kete zao zote kulazimisha watawale jiji hili kukwama, sasa wamebakiwa na kete MOJA tu….kulikimbia jiji! Sasa mtu unaweza ukajiuliza: hivi siku UKAWA wakifanikiwa kutawala jiji la Dodoma, serikali itakimbilia wapi tena? Mbona serikali hii inakuwa na uoga wa kike kiasi hiki? Ni suala la kusubiri na kuona itakuwaje.
Nilivyofungua hii thread nilitegemea facts kumbe ni upuuzi mtupu wa kupoteza mda wa watu
 
huu ni ukweli mtupu

angalia walivyoikimbia arusha na sasa wanaikimbia Dar..

na tutawafuta 2020 tunawakimbiza dodoma
Wameamua kuua biashara ya utalii arusha na kilimanjaro kwa kuweka kodi kibao.....tutawafuata huko huko dodoma
 
Nyerere enzi zake nae alitaka kuhamisha serikali kuipeleka dodoma na wakati huo ilikua chama kimoja tu, unatuambiaje na hapo pia?
 
Kwahiyo UKAWA ikichukua dodoma 2020 makao makuu yatahamia wapi? Sababu dhaifu hii
 
Back
Top Bottom