Sababu za kuzuiliwa Mikutano ya hadhara.

Ulimbo

JF-Expert Member
Aug 14, 2009
3,767
4,035
Salaamu wana JF.
Nimekuwa na maswali mangi ya kwa nini kuna mikutanoinazuiliwa kufanyika bila kupata majibu ya kutosha.

Kumekuwepo na tabia ya viongozi hasa wa ccm wakishitikiana na jeshi la polisi kuzuia mikutano na makungamano bila kutoa sababu za kutosha.
Kwa uchache tu:

1:Kuna kipindi hapa nyuma, bawacha walitata kufanya maobi kwenye uwanja fulani huko Arusha, cha ajabu viongozi wa ccm walileta tracta wakaulima ule uwanja kwa madai kuwa kuna mfadhili kajitokeza kuwaboreshea huo uwanja.

2: Kuna muhubiri aliomba kufanya mkutano katika uwanja wa ngarenaro, walipata vibali toka mamlaka husika, wakafanya maandalizi, wakaweka matangazo na pia kutangaza kwa kutumia magari ya matangazo.
Cha ajabu sikuya mkutano, walizuiliwa kufanya huo mkutano kwa kisingizio kuwa Arusha kuna kipindupindu.

Pamoja na kuzuiliwa huko, Huyo muhubiri toka nchi jirani alitoa msaada wa shilingi 10,000,000/= kukarabati shule ya ngarenaro.
Cha ajabu kuna diwani wa eneo hilo alijigamba akisema wametupa pesa, lakini tumewazuia kufanya mkutano. Je ni nani kafaidi?

Kabla ya majuma kama mawili kwisha, ccm (Katibu mkuu wa ccm) walifanya mkutano kwenye uwanja wa mpira Stadium, katika jiji ambalo wengine walizuiliwa kwa kisingizio cha kipndupindu.
Najiuliza je ni kweli Arusha kuna kipindupindu? Kama kipo wanaofanya mikutano ya ccm hawaleti madhara bali wanaohubiri ndo wanaoleta kipindupindu?
 
Back
Top Bottom