Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Usijipe limit soma
Natumia Muda wangu mwingi kusoma.
Hasa bible study.

From my Knowledge ni kwamba hivo vitabu havina umuhimu wowote.

Kama huto amini Maneno yangu,
Nenda kasome na wewe, make sure umesoma bible yote then fata hivo vitabu vilivyo punguzwa.
 
Sasa lengo la kutuficha ni nini???yani ili iweje ??mbona watu wa zamani walikuwa vilaza hii story ina ukweli ndani yake yani Methodius kilaini hajuo kuhusu hili??
 
je ina maana wakati wa ile gharika hawa wanefili hawakuangamia wote ndio maana wakawepo wengine mpaka wakati Waisrael wametoka utumwani wakakuta bado masalia yao yapo tena mpaka wamezaa kizazi chao (Wana wa Anaki ) ?
Nadhani tumewahi kuwa na mjadala huko nyuma kupitia hizi threads. Kuna hypothesis ya Mfalme Ogu inaweza kuleta mwanga kwenye swali lako.


 
Hizo stori/hadithi kuziweka ndani ya bible ni nonsense kwa sababu Biblia sio kitabu Cha historia, hizo zinatakiwa ziandikwe kwenye vitabu vya civics na history then zifundishwe darasani,, Biblia Ina malengo tofauti kabisa na set ya ufahamu wako
 
Kingine Cha kukusaidia majini/mashetani hawakuhukumiwa kwa makosa ya kusex na binadamu pia kosa lililoseal fate Yao halikufanyika hao viumbe wakiwa hapa duniani maana kosa lao walilifanya wakiwa mbinguni na walikuwa malaika watiifu kwa Mungu lakini malaika mmoja kwa jina la lucifa alipanga njama ya kumpindua Mungu (coup) na akawashawishi malaika wale kuhusu njama yake na wakakubali kuwa washirika wa mpango.

Sasa katika kutekeleza azma Yao walifeli wakakamatwa wakahukumiwa kwa kosa la TREASON na wakatupwa Huku duniani na walipoonekana kuzidi kuchafua wakawekwa sehemu tengwa kuzuia interaction Yao na binadamu.

NB fate Yao ilishakuwa sealed forever na hakuna msamaha kamwe zidi Yao wao ni kama rotten rubbish kwenye dustbin
 
Hapa umeelewa nini?
Uelewe Ni subjective sio objective.kila mtu Yuko biased na kuelewa kitu so ni Kama unatishia ama unababaishia watu labda you're so special to to have objective understanding.

How much are you sure kuwa wewe ndiye ulielewa kilichodhamiriwa na mwandishi.

Hata hapa hutonielewa Bali utaishia kuleta your personal bias
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri.

Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

Catholic theological reflection.

Wanateolojia wa kanisa husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (An omniscient) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Mashahidi wa yehova wameligusia hili kidogo
 
Pia Mungu anaweza taka wewe ukakisome hicho kitabu.
Ndio sikatai
Lakini usiseme biblia inamapungufu.
Ilivyo ndivyo Mungu ametaka biblia iwe.
Una uthibitisho na maneno yako haya "Mungu ametaka biblia iwe ilivyo na isisemwe kama ina mapungufu"...Wewe una "Udini" ndani yako unataka kuona imani, dini, na maandiko yako (Biblia) ni bora sana kuliko andiko lingine lolote lile kwa vile tu Huna zaidi ya unachojua nje ya maandiko yako...Usifosi na kulazimisha Imani yako na dini yako ionekane bora kwa kila mtu maana kuna mambo huyajui na wewe.

Mungu hana Biblia wala Quran wala andiko lolote lile linalojitosheleza kusema ni andiko la Mungu...Vitabu vyote vya Kidini Biblia, Quran vyote vina MAPUNGUFU MAKUBWA SANA....na hakuna andiko lolote lililo kamili kumuelezea Mungu.

Mungu hana dini wala Andiko lolote la Kidini la kumuelezea yeye ni nani...Vyote ni mawazo na imani za wanadamu tu..
 
Back
Top Bottom