Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

But historic wise Kushites wametokea Middle East (Sumeria) ndio maana walipofika Afrika waka settle Misri,Nubia na kuna wakati wakatawala mpaka Yemen/Kuwait za enzi hizo za ma-Pharaoh.

Kush anaongelewa kama mweusi sababu mama yake alikua typical black (Neitam'uk) and of course descendants wa Cush walikua black hata leo. So it can be suggested either alitoka mweusi kma Mama yake ama Naye alioa mweusi typical so dark became darker or rather baada ya kusettle Afrika maybe rangi zao zikawa darker kuliko mwanzo.
Eeh sasa najifunza kitu
 
Book of Enoch
chapter 105
1 And after some days my son Methuselah took a wife for his son Lamech, and she became 2 pregnant by him and bore a son. And his body was white as snow and red as the blooming of a rose, and the hair of his head and his long locks were white as wool, and his eyes beautiful. And when he opened his eyes, he lighted up the whole house like the sun, and the whole house 3 was very bright. And thereupon he arose in the hands of the midwife, opened his mouth, and conversed with the Lord of righteousness. 4 And his father Lamech was afraid of him and 5 fled, and came to his father Methuselah. And he said unto him: ' I have begotten a strange son, diverse from and unlike man, and resembling the sons of the God of heaven; and his nature is different and he is not like us, and his eyes are as the rays of the sun,
Yaani hapa sifa za Nuhu zimempraise sana mzungu jamani
 
Mimi naujua umuhimu wa agano la kale na muhubiri anatakiwa kulitumia vipi agano la kale kufundisha neno la Mungu,
Agano jipya pia.

Sasa kama kuna kitu cha muhimu mwanadamu kukijua na hakipo ndani ya biblia kiseme.

Kwasababu biblia inasema laiti kama biblia ingeandika kila alilolifanya Yesu kipindi chake isinge wezekana ?
Yohana 21:25
[25]Kuna na mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa.
Maji yawe wino, mbingu ziwe karati haziwezi kutosha kuandika sifa zake Yesu
 
Maandiko ya Biblia yanajitosheleza kabisa, na ndio Mungu kataka tusome hayo tu.

Nje na hapo hakuna hekima tena, labda ukajifunze uchawi tu huko nje ya biblia.

Kitabu cha ufunuo kinaeleza kwamba maandiko ya BIBLIA ni sehemu ndogo sana ya mambo yote yaliyopaswa kuandika, yameandikwa kidogo ili tupate kishuhudia. Uwezekano wa kuwapo maandiko upo.

Nawapongeza wenzetu wa Kanisa Katoliki Wana hifadhi kubwa ya masalia ya maandiko na kumbukumbu za kiroho.
 
Nyie wote mmepotoka , mnakubali kuamukiwa vitu vya kusoma,? Mnajifanya mnajua sana maandiko wakati bado ni watumwa tu kwasababu mnaamuliwa mskme nini na njni msisome !

Wapuuzi waafrika rudini kwenye tamaduni zenu Mungu yupo kwenye nature sio hizo dini dini
 
B
Pia Mungu anaweza taka wewe ukakisome hicho kitabu.
Ndio sikatai
Lakini usiseme biblia inamapungufu.
Ilivyo ndivyo Mungu ametaka biblia iwe.
Walioamua ni kitabu gani kiwepo kwenye bibilia na kipi kisiwepo ni watu tuu kama wewe!

Je waliviondoa kwamba havifai kwa mitazamo yao tuu au kwa lengo lipi?

Kwa faida ya nani?

Na kama havikuwekwa kwenye Biblia kwamba havikufaa kwanini hawakuviweka kwenye rejelea ili kama kuna mtu anauhitaji navyo avipate kwa urahisi?
 
Nyie wote mmepotoka , mnakubali kuamukiwa vitu vya kusoma,? Mnajifanya mnajua sana maandiko wakati bado ni watumwa tu kwasababu mnaamuliwa mskme nini na njni msisome ! Wapuuzi waafrika rudini kwenye tamaduni zenu Mungu yupo kwenye nature sio hizo dini dini
Hakika naamini mungu yupo, ila hizi mambo za Bible toleo la 5 la king James 🤣🤣🤭 wananivunja mbavu nakunitoa relini kwamba kuna kikundi cha watu wanakaa wanapanga toleo hili la bibilia kipi tukiondoe na tuongeze kipi (hatujui ni kwa faida au hasara ya nani) ndio wanaowaamulia wakristo wote duniani
 
Ngoja nikupe na huu mstari

Mwanzo 4
23 Lameki akawaambia wake zake,Sikieni sauti yangu, Ada na Sila;Enyi wake za Lameki, sikilizeni usemi wangu;Maana nimemwua mtu kwa kunitia jeraha;Kijana kwa kunichubua;
24 Kama Kaini akilipiwa kisasi mara saba,Hakika Lameki atalipiwa mara sabini na saba

Hapa umeelewa nini?
Huenda Lameki aliua, japo biblia haijatuambia ni nani, wapi na kwa nini ?
 
Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri.

Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

Catholic theological reflection.

Wanateolojia wa kanisa husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (An omniscient) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.



Sent using Jamii Forums mobile app
Hata ule ujuzi wa silaha ksali kali za jamii ya mongolian( China, korea, japani na urusi) sio wakawaida.
 
Hakika naamini mungu yupo, ila hizi mambo za Bible toleo la 5 la king James 🤣🤣🤭 wananivunja mbavu nakunitoa relini kwamba kuna kikundi cha watu wanakaa wanapanga toleo hili la bibilia kipi tukiondoe na tuongeze kipi (hatujui ni kwa faida au hasara ya nani) ndio wanaowaamulia wakristo wote duniani
Hizo ni translation tu sio "Version" mfano kuna maneno ya kiingereza Cha Karne ya 16 kwa sasa huwezi elewa ndio kinatafsiriwa upya.

However ukiona mstari umeachwa ujue text walizotumia kutafisira say Codex Sinaiticus n.k hazina huo mstari maana hautafsiri kutokea Biblia ya kiingereza hiyo hiyo Bali unatafsiri upya kutumia ancient texts ambazo ni original na credible in Hebrew and Greek.
 
Huenda Lameki aliua, japo biblia haijatuambia ni nani, wapi na kwa nini ?
Book of Enoch inadai Lamech ndio alimuua Cain kwa mkuki na pia akamuua mwanaye yaani Tubal-Cain by accident. So ile laana ikahamia kwa Lamech so kisasi kikawa doubled!!!

However bible haisemi Cain alikufaje so imeacha gap kama hiki kisa ni kweli ama lah
 
Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani,

Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, W
Kwani uasi ulitokea huko mbinguni baada ya mwanadamu kuwa ameshaumbwa ?
 
Hiko kitabu kinatumika na Ethiopian Orthodox ambalo ndio kanisa la Kwanza Afrika hata kabla RC haijafikiriwa kuanza.

Je unaona nani yupo sahihi hapo? Au inakua halali pale tu mzungu akikiweka kwenye biblia?

Mfano Wimbo ulio bora una changamoto zote kma book of Enoch ila hakijatolewa and more so hta makanisani hakifundishwi regularly!! But kingekua nje ya Biblia kama naona jinsi mngekikejeli.
Mkuu unakumbuka hii habari kwenye kitabu cha mwanzo...

Mwanzo 6:14 " Nao wanefili walikuwako duniani siku zile; tena baada ya hayo, Wana wa Mungu walipoingia kwa binti za wanadamu, wakazaa nao wana; hao ndio waliokuwa watu hodari zamani,watu wenye sifa".

Mkuu hawana wanefili mahali pao ni wapi ? Maana kama walikuwepo huku duniani,ina maana hapakuwa kwao...halafu baada ya gharika wote walikufa na Nuhu alianza upya.

Halafu soma tena

Hesabu 13:33 " kisha huko tuliwaona wanefili, Wana wa Anaki, waliotoka kwa hao wanefili; tukajiona nafsi zetu kuwa mapanzi; nao ndivyo walivyotuona sisi"

Hii ilikuwa ni ripoti ya wale wapelelezi waliotumwa na Musa kuipeleleza Kanani, walisema waliwaona wanefili, na Wana wa wanefili (Wana wa Anaki ),

je ina maana wakati wa ile gharika hawa wanefili hawakuangamia wote ndio maana wakawepo wengine mpaka wakati Waisrael wametoka utumwani wakakuta bado masalia yao yapo tena mpaka wamezaa kizazi chao (Wana wa Anaki ) ?
 
Mam

sio kweli! Mambo gani aliyofanya yesu na hayaandikwa? Mbona Yesu kaandkwa na wahubiri wanne (matayo, marco, luka na yohana) lakin wote wanaeleza yale yale tu.. apo si ndo kila mmoja angeandika ambayo mwenzie hajaandika... kama wameandika hadi alivokwenda kwa zakayo sasa wameacha jambo gan la muhimu?
Akikujibu niite
 
Back
Top Bottom