Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Sababu za kufichwa kwa kitabu cha Enoch

Biblia ina Vitabu 73 lakini isiwe Mpaka wakusoma hivyo 73 tu, Canon ya Vitabu 73 iliapitishwa mwaka 382 na Baraza la Maaskofu wa Roma kuna Vitabu Vilipitishwa vikiwa Havina Sifa E.g (Waebrania) lakini kuna vitabu havikupitishwa Kuwemo ndani ya Biblia lakini vikiwa na Sifa, mfano Kitabu cha Henoko, Pengine Mababu waliona "Chakuzushi" lakini ukweli ni Kwamba kiliandika Aibu nyingi.

Henoko anayedhaniwa kuwa alikuwa ndio mwandishi wa kitabu hiki ni Yule mtoto wa Yaredi na baba wa Metuselah, ambaye akaja kuwa babu wa Nuhu MWANZO 5:21-23, Ni Moja ya Mtu anayetajwa kuwa na Mwisho wa Ajabu kwani hakufa, bali alitwaliwa mbinguni YOSHUA BIN SIRA 44:16, WAEBRANIA 11:5. Maswala Kama haya hupaswi kujadili na Wale wenye Canon Ya Vitabu 66 kwani watakwambia vitabu hivi havifai "Wanaviita Apokrifa" Wasijue Hata Baadhi ya Sura za Kitabu cha Zaburi ni Apokrifa na katika Biblia yao zimo.

Hiki kitabu cha Henoko Hukataliwa na Kanisa Katoliki la Magharibi (Latin Church) kwa Sababu zake za Msingi Moja ya Sababu ni Kitabu Kukosa Jina la Mwandishi hakika, Lakini kanisa Katoliki la Mashari la Ethiopia (Orthodox) katika Orodha yao wanakitumia kama Kitabu cha Muhimu sana. Ni kama Wayahudi wanavyokitumia kitabu kinachoitwa YASHARI au JASHAR kinachotajwa 2SAMWELI 1:18, Vitabu hivi vina mambo fulani ya kipekee ambayo wataalamu husema ni siri.

Kitabu Cha Henoko Hutajwa kwa hypingwa Vikali kwa sababu Ndio huonyesha Mtu mweupe alipata wapi Ujuzi, Pia huonyesha Chanzo cha Mapepo na Wanefili.

Ukisoma Kitabu cha HENOKO 6:1-8 ni sawa na Ukisoma MWANZO 6:1-8 lakini kuna utofauti wa Stori za malaika zaidi, Inaonekana katika zama za YAREDI babaye na HENOKO kuna malaika kama 200 walikubaliana kushuka duniani na Kujichanganya na wanadamu, hapo ndipo ambapo YUDA alinakili maelezo ya YUDA 1:6 Malaika walipoona kuna mabinti wa wanadamu wanavutia/Wazuri MWANZO 6:2 Ndipo wakashauriana "Mwaonaje Tujitwalie tuwaoe, tuzae nao watoto?" Malaika Kiongozi aliyeitwa SAMYAZA akahofia Labda malaika wenzie wanaweza Kumsaliti katika mpango huu, Akahimiza malaika kuapa, Wakaapa kutekeleza. (Henoko 7:3-6)

Kitabu Cha Henoko kinawataja kabisa kwa Majina Viongozi wa Malaika hao waliokuwa katika Mlima HERMON kwamba ni SEMIAZAZ, ARAKIBA, RAMEEL, KOKABIEL, TAMIEL, RAMIEL, DANEL, EZEQEEL, BARAQIJAL, ASAEL, ARMAROS, BATAREL, ANANEL, ZAQIEL, SAMSAPEEL, SATAREL, TUREL, JOMJAEL, SARIEL.

Ikumbukwe hawa hawakuwa malaika Watiifu kwa Mungu, Ni wazi kuwa walikuwa sehemu Katika wale Walioasi pamoja na shetani, Katika MWANZO 6:2-4 Imewataja kama "WANA WA MUNGU" hili jina lisikuchanganye maana malaika wote huitwa wana wa Mungu ndio maana hata Biblia ya asili ya Kiyunani imewaita malaika "ANGELUS ES DEUS" ikimaanisha malaika wa Mungu No matter Watiifu au Sivyo, Sasa mstari wa 4 katika MWANZO 6 unasema "Basi walikuwepo Wanefili duniani(NEPHILIM THE FALLEN ANGELS) hapo jiulize kwa nini aseme "DUNIANI" ni kwasababu hapakuwa mahali pao pa asili (2Petro 2:4,YUDA 1:6) Ni lazima waliyaacha makao yao...

Kitabu cha HENOKO 7:1-6 tunaona haya yafuatayo, Malaika wale 200 Wakiongoza na SEMJAZA baada ya Kiapo, wanaoa mabinti wanadamu Na Kuwapa Mimba, Hawakuishia hapo, Katika Sura ya 7 Mstari wa 10 tunaona Malaika hawa waliwafundisha binadamu Uchawi "sorcery" Wakafundisha Orodha ya Maneno ya Kufufua wafu "incantations" Wakawafundisha Jinsi ya Kutengeneza Dawa za Kuwatibu kutumia Mitishamba (pharmacology).

Ilipofika kipindi cha wale mabinti kuzaa Katika sura ya 7:11-14 tunaambiwa Walizaliwa Viumbe wakubwa kupita hata Binadamu na Malaika (Giants), Walizaliwa wengi Mpaka Binadamu walichoka Kuwahudumia chakula, Wakaanza kula Wanyama, Ndege na Samaki, Baadae wakaanza kuwala Binadamu, na Mwisho wakalana wao kwa Wao.

Basi katika Sura ya 8 tunaona Malaika AZAZEL anawaonea huruma Binadamu, Anaanza kuwafundisha Kutengeneza Silaha, Mapanga (Swords) , Visu, Ngao na Ngao za Vifuani (BREASTPLATED) hapa ndipo zana za chuma zilipogunduliwa (MWANZO 4:22) TUBALI-KAINI akiwa wa kwanza kuchukua Ujuzi.

Kupitia Malaika Azazel ndipo Binadamu alipojua Kupigana Vita, Malaika hawakuishia hapo, Malaika hawa ndio Walifundisha Dada zetu kuvaa Vikuku na Bangili (BRACELETS) Pia wakafundisha dada zetu kupaka Rangi Kope (BEAUTIFYING OF EYELIDS) na hapa ndipo Dhambi ya Kuzini kwa matamanio ilianza

Malaika waliendelea Kutoa siri nyingi na Kumpa Binadamu uwezo Ulioshindikana, Kila malaika alikuwa na Kitengo chake.

Malaika aliyeitwa SEMJAZA huyu aliwafundisha Binadamu kumiliki Nguvu za Maajabu kufanya Mambo makubwa, Pia Kutumia Mizizi ya Miti kama Tiba, Kemia Kiujumla. Malaika ARMAROS alifundisha jinsi ya Kutatua Tatizo litokanalo na Uchawi wa mtu mwingine. Malaika BARAQIEL huyu aliwafundisha binadamu elimu ya vitu vya Angani "ASTROLOGY" Malaika kwa jina la KOKABEL akawafundisha binadamu elimu ya Anga ihusuyo mipaka ya Nyota na maumbo yake "CONSTELLATION" Malaika EZEQEEL akawafundisha Binadamu Juu ya Mawingu. Malaika ARAQIEL akawafundisha Alama za Kidunia (zodiac elemental rulerships) ambazo tunaziita Libra, Virgo, Capricon nakadhalika. Malaika SHAMSIEL akafundisha alama za Jua Na Malaika SARIEL akawapa Kozi za Elimu ya Mwezini.

Kwahiyo Ujuzi wa Binadamu na Mambo machafu yalianzia Juu ya Hawa malaika Bila Ujio wao Binadamu Angekuwa "Kilaza Mmoja hivi" Basi Baadhi ya Malaika Watiifu walienda Kumuelezea Mungu juu ya Uchafu uliofanywa na malaika duniani, Hata Mungu aliona wameipa Mbingu aibu, na Alishindwa Kuwasamehe na aliwafunga vifungo vya milele chini ya Giza wakingojea hukumu.

Catholic theological reflection.

Wanateolojia wa kanisa husema wazi kuwa inawezekana huu ulikuwa ni mpango wa Shetani kuharibu Mpango wa Mungu wa MWANZO 3:15 kwa Sababu Mungu alisema Mkombozi wa Wanadamu atakuwa binadamu Pure na si Malaika na Atazaliwa Pasipo Dhambi, Na Atazaliwa na Mwanamke, Basi Shetani alipanga kuharibu Vinasaba (Gene) za Binadamu kwa kuzichanganya na za Malaika Basi basi Kuzaliwa Kwa Mkombozi kungeshindikana.

Lakini Mungu anajua Zaidi (An omniscient) Ni zaidi ya Malaika (ISAYA 46:9-10) anajua Mwanzo na Mwisho, Hivyo ndio maana Alifuta Kizazi cha Enzi zakina Nuhu kwa Gharika na Kubakiza Wanadamu 8 tu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Naweka kambi ntarud baadae
 
Ukisoma kitabu cha henoko enock utajua haya;-

1.jua linazunguka Dunia KWA kupitia mageti kumi na Mbili na sivyo tufundishwavyo!

2.Nuhu aliandika magonjwa yote Duniani na tiba zake ZOTE za matunda na mizizi akampa kitabu. Hicho mwanae makubwa shem ambae ni Baba wa wazungu!ni WAKATI akiwa mzee Sana!!

3.wakati huo wa enoch Mbingu au anga lilikuwa KARIBU na Dunia ilipitia majira yake VIZURI KWA mwaka yaani majira yote manne na uzalishaji ulikuwa juu Sana lakini maovu yalipoongezeka tu Mbingu ikapanda juu ZAIDI kama ilivyo leo!!

4.Mgawanyo wa urithi wa nuhu KWA Watoto wake ulikuwa hivi;-

Shemu:-yeye ni mweupe KWA rangi kama mzungu YEYE alipewa maeneo ya baridi hasa barafu huko ulaya HUKO!

jafety;-mwekundu wa Rangi alipewa maeneo ya Kati yaani hakuna joto Wala baridi baba wa waarabu,

Hamu:-ngozi yake iliyoungua KWA maana nyeusi alipewa maeneo ya joto kali!! kwasababu ngozi yake ina mafuta Mengi

Nuhu akawaonya endapo mmojawapo akivamia eneo ambalo Sio lake kutokana na urithi Wake Ndipo kitakuwa na vita Dunia mzima haitoisha !!Hamu uzao wake ukavamia eneo la jafety vita ikaanza Hadi leo machafuko hayaishi!!!
What a load of bs[emoji706]
Kwamba jua linazunguka dunia kwa mageti 7? Mbingu ilikua karibu na dunia? Mbingu ni nn?

Na iko katika hali gani? Iko wapi? Watu wa zaman (kama ulivoandika, "mbingu ilikua karibu na dunia") waliweza kufika huko mbinguni? Kama ndio, tunaweza kufika hata sasa? Kama hatuwezi kufika ni kwann hatuwezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Ukisoma kitabu cha henoko enock utajua haya;-

1.jua linazunguka Dunia KWA kupitia mageti kumi na Mbili na sivyo tufundishwavyo!

2.Nuhu aliandika magonjwa yote Duniani na tiba zake ZOTE za matunda na mizizi akampa kitabu. Hicho mwanae makubwa shem ambae ni Baba wa wazungu!ni WAKATI akiwa mzee Sana!!

3.wakati huo wa enoch Mbingu au anga lilikuwa KARIBU na Dunia ilipitia majira yake VIZURI KWA mwaka yaani majira yote manne na uzalishaji ulikuwa juu Sana lakini maovu yalipoongezeka tu Mbingu ikapanda juu ZAIDI kama ilivyo leo!!

4.Mgawanyo wa urithi wa nuhu KWA Watoto wake ulikuwa hivi;-

Shemu:-yeye ni mweupe KWA rangi kama mzungu YEYE alipewa maeneo ya baridi hasa barafu huko ulaya HUKO!

jafety;-mwekundu wa Rangi alipewa maeneo ya Kati yaani hakuna joto Wala baridi baba wa waarabu,

Hamu:-ngozi yake iliyoungua KWA maana nyeusi alipewa maeneo ya joto kali!! kwasababu ngozi yake ina mafuta Mengi

Nuhu akawaonya endapo mmojawapo akivamia eneo ambalo Sio lake kutokana na urithi Wake Ndipo kitakuwa na vita Dunia mzima haitoisha !!Hamu uzao wake ukavamia eneo la jafety vita ikaanza Hadi leo machafuko hayaishi!!!
Kwamba mtu mwenye mafuta mengi ndio kapewa sehemu yenye joto kali? [emoji23]unajua kazi ya mafuta mwilini lakini?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
What a load of bs[emoji706]
Kwamba jua linazunguka dunia kwa mageti 7? Mbingu ilikua karibu na dunia? Mbingu ni nn? Na iko katika hali gani? Iko wapi? Watu wa zaman (kama ulivoandika, "mbingu ilikua karibu na dunia") waliweza kufika huko mbinguni? Kama ndio, tunaweza kufika hata sasa? Kama hatuwezi kufika ni kwann hatuwezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Mkuu

Kasome mwenyewe!!

Jamaa alitabiri ujio wa yesu Hadi mwisho wa dunia pia Wana wa Israel UTUMWANI Misri!!

Aliandika Kila kitu!!

Hadi wakati enoch anaondoka duniani alipanda farasi baada ya kuwaaga nduguze Sasa wakawa wanamfuata KWA nyuma hadi wakakata TAMAA na wengine waliomfuata wakabadilika na kuwa mawe KWA sababu ya ubishi wao!!

Pia Lindi la malaika likiongozwa na azazel ndio lilifundisha Watoto wa adamu uchawi,uganga,kutengeneza silaha,vioo,ngao,unajimu,na n.k!

Enoch anasema kila kitu tuionacho kuanzia upepo,mvua,radi,matetemeko na mengineyo yanaongozwa na malaika!

Jua huzunguka jua kupitia mageti 12!!!

Nilisoma sana huku kitabu!

Google "the book of Enoch all chapter's"utapata baadhi ya chapter's NYINGI kuna nyingine zimeondolewa nadhani chapters 33 na n.k

Nadhani mengine ni siri hawakutaka tujue!

Endelea kitafakari mambo ya kiroho kimwili,pia jamaa YOTE hayo aliyaandika baada ya kupitiwa na usingizi mzito Sana!Akiamka tu ndio huandika!!

End!
 
Hakuna ushahidi wa hayo mambo kama yalitokea. Kuna namna tunaweza kupata kuona ushahidi wa kwamba jua linazunguka dunia kupitia mageti 12? Mageti ni ya size gani hayo na jua lina ukubwq kiasi gani?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
KWENYE the book of Enoch shemu was white in color,na urithi Wake ni nchi za Baridi ,jafety alikuwa mwekundu na Hamu black,Book of Enoch!
Solomoni/suleiman anasema yeye alikuwa mweusi. Kamsome Jeremiah nae pia anasema ni mweusi.

Ufunuo WA yohana anamuona Yesu anafanana na shaba uliyoungusa sana. Jiongeze hapo.
Plus MISRI ya zamani ya Farao walikuwa weusi so how come Wazungu kama Musa akae kwenye nyumba ya Farao 40years wasimjue.

Kitabu cha Enoch kinamueleza Nuhu kama Albino... WA kwanza duniani... Kutoka kwa mtu mweusi na ndio maana Wazungu walikitoa
 
Halafu mzungu Kaweza kukaa mda mrefu juani baada ya kugundua Yale macream Yao wanapaka bila hivyo kansa ya ngozi sekunde tu anaipata. Ndo akakae utumwani mwenye joto LA MISRI kwa miaka 40[emoji23][emoji24][emoji24][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]

Hakuna mzungu anayeweza Utumwa. Mtu aliyeenda Utumwani ni mmoja tu na ndio anafanana na laana zote zilizoandikwa kwenye kumbukumbu LA torati na huyo kiumbe ni Mtu mweusi tu aka Negroes.
 
Hayo maneno yapo kwenye kitabu Chao Hao mnawaita Waisrael Wazungu..... Wao wenyewe wanajua.... Mzungu ni Japhet.
Screenshot_20221112-125951.jpg
 
Kuna kimoja kinaitwa 'The gospel of Mary' Injili ya Maria, hichi kiliandikwa na Maria Magdalena na kuna shirika la watawa wanakitumia japo hakipo kwenye orodha ya sasa.

Ila biblia ni sawa na mtu tu ukusanye vitabu vya jeografia, kemia, fizikia, historia, hesabu na lugha alafu kila somo hapo uligeuze kuwa sura, then ukiite icho kitabu, kitabu cha maarifa 😂.

Ivyo ndivyo biblia ilivyo.
 
Halafu mzungu Kaweza kukaa mda mrefu juani baada ya kugundua Yale macream Yao wanapaka bila hivyo kansa ya ngozi sekunde tu anaipata. Ndo akakae utumwani mwenye joto LA MISRI kwa miaka 40[emoji23][emoji24][emoji24][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Hakuna mzungu anayeweza Utumwa. Mtu aliyeenda Utumwani ni mmoja tu na ndio anafanana na laana zote zilizoandikwa kwenye kumbukumbu LA torati na huyo kiumbe ni Mtu mweusi tu aka Negroes.
Karibu watu wa aina yote waliwahi kua watumwa. Sio weusi tu

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nimesoma kitabu hicho cha Yuda.

Lakini point yangu itabaki pale pale, ni mafundisho yapi ya Henoko unayoyalilia wewe ukitaka yawekwe kwenye biblia.

Manabii wa zamani walitoa unabii kuwaonya watu wa kipindi kile, si henoko peke yake alifanya hivo, wapo manabii wengi tu.

Lakini swali linakuja wewe uliyesoma kitabu cha henoko unanizidi nini mimi ambae sijakisoma. ?

Na kama waliounganisha vitatu vilivyounda Biblia waliona hakifai Roho mtakatifu aliwaonesha kuwa kimechakachuliwa ? Au si cha muhimu.
Utalazimisha kiwepo kwenye Biblia ?

Kama henoko anamafundisho muhimu sana, tuambie.
Maana mimi najua hata vitabu vya Solomon si vyote vilichukuliwa na kuwekwa kwenye biblia.
Nadhani usiulize yeye aliyekisoma kakuzidi nini, sababu ipo wazi kakuzidi maarifa yeye anakifahamu wewe haukifahamu so amekuzidi Bro.

Pia kwa minajili ya swali hilo, utaulizwa wewe unayeisoma biblia unamzidi nini mtu asiyeisoma pengine hata asiyeijua kabisa iyo biblia?.

Biblia si kitabu kimoja hivyo ni rahisi kubadilika wakati wowote. Mfano kwa sasa biblia inatambua jinsia zote mbili yaani imefanyiwa marekebisho palipotaja Mtu mwanamume pameongezewa na mwanamke, soma biblia za kale na za sasa utagundua ilo swala. Then jiulize kwanini?

Kwanini roho mtakatifu ambaye ni mjuzi wa yote hakuwaonesha mababu umuhimu wa kuzitambua jinsia zote kwenye biblia za kale? Mambo ni mengi hapo.
 
What a load of bs[emoji706]
Kwamba jua linazunguka dunia kwa mageti 7? Mbingu ilikua karibu na dunia? Mbingu ni nn? Na iko katika hali gani? Iko wapi? Watu wa zaman (kama ulivoandika, "mbingu ilikua karibu na dunia") waliweza kufika huko mbinguni? Kama ndio, tunaweza kufika hata sasa? Kama hatuwezi kufika ni kwann hatuwezi?

Sent using Jamii Forums mobile app
Kwa kumsaidia tu, mbingu (Atmosphere and beyond) kuwa karibu Kuna nadharia inaitwa crystalline canopy theory ambapo ukisoma kitabu Cha mwanzo Maji yalitengwa mengine yakabaki ardhini yaani mito,maziwa n.k na mengine yakawekwa juu ya dunia hii ni kwa mujibu wa bible Sasa. Hivyo inadaiwa haya Maji yalisaidia kuotesha sana mazao na kuleta hali ya hewa nzuri n.k so ikawa depicted kwamba mbingu ipo closer kwa ardhi.

NB: kibiblia Mvua ilinyesha kwa mara ya kwanza kipindi Cha Nuhu so ukisikia bible inasema "Maji yalitoka chini na juu ya dunia" ndio wanadai hii canopy ilimwaga mvua isiyokoma kwa siku almost 40.

2. Nadharia ya pili ni Ile fact kwenye Biblia kitabu Cha mwanzo Cha wanadamu kutaka kufika mbinguni (Makao ya Mungu) kwa kujenga mnara mrefu meaning walikua na idea possibly kuwa mbingu ipo "karibu"!!

3. Nadharia ya tatu kwenye book of Enoch ni pale anamuonya Zamuzamim (Malaika aliyetupwa) kuwa asipae sana juu ya anga maana jua limemkosa kosa kumchoma!! Meaning the distance between dunia na space ilikua ndogo biblically.

4. Kuhusu kufika mbinguni (makao ya Mungu) ni ngumu ila hata kwenye book of Enoch walipotaka kufika mbinguni hawakutegemea mnara ndio uwafikishe per se ila walikua wanajaribu kutengeneza warmhole whether kichawi au kisayansi I'm not sure ila kitendo Cha Mungu kuwavuruga means "aliona" Kuna "possibility" ya wao kufika huko.

Kisayansi tunaweza fika kwenye mbingu (atmosphere and beyond) ila sio mbinguni (makao ya Mungu)
 
Heshima kwako mkuu
 
Natumia Muda wangu mwingi kusoma.
Hasa bible study.

From my Knowledge ni kwamba hivo vitabu havina umuhimu wowote.

Kama huto amini Maneno yangu,
Nenda kasome na wewe, make sure umesoma bible yote then fata hivo vitabu vilivyo punguzwa.
Wangeweka vyote sisi ndo tuamue tunasoma kipi na kuacha kipi, kipo kitabu cha yoshua bin sira kama sikosei, kuna mstari unasema "maisha yafaa nini bila pombe"
 
Back
Top Bottom