Sababu ni Nini simu za Tecno kunangwa

Sababu ni Nini simu za Tecno kunangwa

8F6ACB29-1F1D-48EE-984A-54F35F16FEAB.jpeg
 
Salam wakuu. Bila kuwachosha

Kwa miongo kadhaa nimekuwa mtumiaji wa simu za hii kampuni ya Tecno

Binafsi sijaona tatizo lolote kama inavyosemekana

Kipindi flani niliwahi kununua simu ya Samsung baada ya kuona zinasifiwa sana ila kwa baadae nilikuja kuiuza baada ya kuona inakula sana moto

Hata hivyo sikuona Cha ajabu

Sasa Huwa nashangaa sana naposikia mtu anasema kwamba simu za Tecno au Infinix ni simu za wanawake

Nachotaka kujua ni je hizi simu Zina matatizo Gani

Je ni kitu Gani mtu mwenye simu ya Google pixel,Samsung,iphone ya milioni mbili anapata ambacho Mimi mwenye Tecno,Infinix ya laki mbili siwezi kupata

Au ni ulimbukeni wa kupata Hela ukubwani

Kiongozi
Wala usiumize kichwa kwani usafiri ni usafiri. Mkitoka Dodoma kwenda Dar, kuna wanapanda, Basi, wengine Treni, wengine ndege mwisho wa siku wote mnafika Dar
Turudi kwenye simu; Kwa suala la mawasiliano ya kawaida zote zinafanya mawasiliano ILA Kwa wenye kazi nyingi za simu nafikiri ndio simu kama Samsung na Iphone zinawahusu.

Kumbuka tu hizi bidhaa zinatengenezwa ili watumiaji wa uwezo tofauti tofauti waweze kumudu;
ndio sababu hata hizo simu, magari nk yapo ya watu wa uwezo tofauti tofauti kuanzia Passo na kuendelea...ila yote magari ILA ubora na ufanisi ni tofauti. Nunu bidhaa iliyoko kwenye uwezo wako, wala kelele za watu zisikusumbue....
 
Tecno zinadumu na ikiharibika ni rahis kupata vifaa vyake

As an Expert
Swala la uzuri wa simu unachangiwa na matumizi yako

Kuna settings hazipo kwenye simu hii ila unaikuta kwenye simu ingine

Kwa mm nitanunua aina zote kulingana na matumizi yake

Kama unabisha katengeneze simu yako
 
Ukijua utofauti wa V8 na probox basi pia utajua utofauti wa midrange phone na high range phone
 
BMW X 5 Vs PASSO yote kazi yake ni kukutoa point A kwenda point B,lakini kwenye hiyo safari mwenye BMW atasafiri kwa uharaka,kwa kurelax,ataenda u mbali mrefu zaidi bila kupumzika tofauti na Passo!
 
Ndugu mwandishi ungekuwa na akili timamu wewe binafsi ungekubali kutumia tecno?
 
Ndugu mwandishi ungekuwa na akili timamu wewe binafsi ungekubali kutumia tecno?
Naona Unazunguka tu mbuyu ila bado hujajibu swali langu

Nini Cha ziada kilichopo kwenye hizo kampuni mnazosifia

Mpaka Sasa Mimi ni mtumiaji wa Tecno
 
Shida hela mkuu! Ukiwa na hela wala hutajisumbua kuuliza swali la kitoto kama hili. Hela hutofautisha madaraja,wewe upo daraja la chini ndio maana unaona wote mko sawa na mtu mwenye simu ya 2m. Mimi nina tecno camon19 nimeinunua 1.5m unataka kunambia niko sawa na yule wa tecno ya 150k
 
Salam wakuu. Bila kuwachosha

Kwa miongo kadhaa nimekuwa mtumiaji wa simu za hii kampuni ya Tecno

Binafsi sijaona tatizo lolote kama inavyosemekana

Kipindi flani niliwahi kununua simu ya Samsung baada ya kuona zinasifiwa sana ila kwa baadae nilikuja kuiuza baada ya kuona inakula sana moto

Hata hivyo sikuona Cha ajabu

Sasa Huwa nashangaa sana naposikia mtu anasema kwamba simu za Tecno au Infinix ni simu za wanawake

Nachotaka kujua ni je hizi simu Zina matatizo Gani

Je ni kitu Gani mtu mwenye simu ya Google pixel,Samsung,iphone ya milioni mbili anapata ambacho Mimi mwenye Tecno,Infinix ya laki mbili siwezi kupata

Au ni ulimbukeni wa kupata Hela ukubwani
Sababu kuu ni kwamba simu za Tecno zipo chini kiubora kuliko simu za kampuni nyingine. Kwa mfano chukua flagship za Tecno fananinsha na za kamouni nyingine utagundua Tecno zipo nyuma kiteknolojia

Angalia hii video uone Samsung inachoweza kufanya kupitia software pekee

View: https://youtu.be/2R_KBaPeYUg?si=2K-DT9Zp3Nnrvytz

Na hapo hatujaongelea hardware ambapo Tecno iko nyuma sana ukifananisha na makampuni mengine
 
Naona Unazunguka tu mbuyu ila bado hujajibu swali langu

Nini Cha ziada kilichopo kwenye hizo kampuni mnazosifia

Mpaka Sasa Mimi ni mtumiaji wa Tecno
Ni kopo ni sawa na zile simu za copy za wachina wao wanacopy tu simu ya million na point mfano iPhone unakuta inauzwa laki au laki na 50.. ukija kuchunguza vizuri kumbe ni copy/kopo
 
Kaba sijakueleza kwa undani Nenda kwanza kasome utofauti wa display pamoja na processor. Ya tecno na samsung na hapo sijagusia sreen resolution.
Hapo ndo utajua kwanini watu wanaponda sim za tecno infinix na itel
Lakini hizo simu kadri unavyozidi kutumia ubora nao unazidi kushuka mfan kwasababu ya processor yake ukijaza tu vitu au kuwa na file kubwa kuganda ni kawaida na ujumbe wa "unfortunately stoped" hukosi
 
Salam wakuu. Bila kuwachosha

Kwa miongo kadhaa nimekuwa mtumiaji wa simu za hii kampuni ya Tecno

Binafsi sijaona tatizo lolote kama inavyosemekana

Kipindi flani niliwahi kununua simu ya Samsung baada ya kuona zinasifiwa sana ila kwa baadae nilikuja kuiuza baada ya kuona inakula sana moto

Hata hivyo sikuona Cha ajabu

Sasa Huwa nashangaa sana naposikia mtu anasema kwamba simu za Tecno au Infinix ni simu za wanawake

Nachotaka kujua ni je hizi simu Zina matatizo Gani

Je ni kitu Gani mtu mwenye simu ya Google pixel,Samsung,iphone ya milioni mbili anapata ambacho Mimi mwenye Tecno,Infinix ya laki mbili siwezi kupata

Au ni ulimbukeni wa kupata Hela ukubwani
Kaka una uelewa kdg wa mambo ya electronics ? Mfano teknolojia zinazotumika, raw materials na finishing ? Kwamba unaona Samsung na Tecno ni sawa tu hakuna tofauti ? Unadhani bei za Samsung kuwa juu ni utapeli tu wanatuibia ? Hebu waza kwenye areas nyingine kidogo, mfano nguo, viatu, magari nk.. vyote ni sawa kiubora ? Mtu akikwambia amenunua shati karume kwa 10k, na mwingine kkoo kwa 18k na mwingine Posta kwa 100k hayo mashati yatakua sawa tu ? Au kuna haja ya kwenda details kdg kuona manufacturer ni nani na anatumia tech gani na material gani kujitofautisha na wengine, hebu kaulizie Mercedes maybach S class V12 na Crown, zote ni saluni, ushangazwe !
 
Sasa mkuu kama lengo inakuwa kuringishia

Huoni kama kwa mtoto wa kiume kukaa na kuringishia simu inafanya watu tuanze kukufikiria mara mbili mbili
Tecno sio simu ni vile TBS hawapo kazini na pia inaonekana sio mtumiaji wa simu bora ndio maana hauna hoja..Samsung kwenye Electronics wapo mbali sana sana..
 
Back
Top Bottom