Uchaguzi 2020 Sababu ni kwanini Rais Magufuli atashindwa sana uchaguzi huu

Prof Koboko

JF-Expert Member
Aug 15, 2020
350
2,549
Hili tumekua tukilisema sana humu mara nyingi.

Sababu kubwa Rais Magufuli kushindwa na Wapinzani tena kwa kura nyingi sana ni Ugumu wa maisha aliousababisha yeye na serikali yake. Watu wote nchi nzima wanalia na maisha magumu mzee hasikii kabisa.

Mzee amekimbilia kuanzisha miradi mikubwa ambayo unatafunwa pesa nyingi sana kupelekea kupungua kwa mzunguko wa pesa kwenye biashara mitaani. Hii hakushariwa vyema lakini ndio itamuondosha mapema sana. Ugumu wa maisha unaumiza mtu mmoja mmoja ndio hawa watapiga kura.

UNAMPIGIA KURA MAGUFULI ILI IWEJE?
Hivi unaweza ukawa na sababu ya msingi kumshawishi huyu Mtanzania wa kawaida ambaye sasa anakula mlo mmoja kwa siku?
Utmwambia nini yule mama ambaye anapanga Nyanya zake barabarani kutwa nzima hata nusu ya misingi wa biashara yake hairudi?
Utamshawishi vipi Mfanyakazi huyu ampigie kura Magufuli ambaye hajamuongezea mshahara miaka yote 5? Ampende Magu kwa lipi hasa?

MAGUFULI AMEMPA LISSU USHINDI WA MAPEMA SANA
Kwanza Lissu utamshinda kwa halali, akikushinda huwezi kumpora haki yake. Labda akiwa Kitandani hoi ndio utampora haki yake kama walivyompora Ubunge wake akiwa kitandani Ubeligiji. Magu ana deni kubwa sana kwa Lissu kwa kutomuonyeshaau kutowapata waliomshambulia maana yeye ndiye Amiri jeshi mkuu. Hili deni kutampa shida na ndiyo moja ya sababu ya kushindwa vibaya uchaguzi huu.

LISSU ANA USHAWISHI NA MVUTO WA KISIASA ZAIDI KULIKO MAGUFULI
Hii ni sababu nyingine kubwa ndiyo maana mikutano yake inakaa sana bila kutumia wasanii wala vyombo vya habari, hapa ni kumshauri mzee ajiandae tu kisaikolojia.
 
Huyo Mtanzania anayekula mlo mmoja kwa siku kafurahi sana kwakuwa matajiri sasa wanakiona cha moto, so wote tutarudi kuwa level za chini.

Kula ya NDIO tena kwake.
Ndugu Kiboko,tusubiri kura zipigwe ,ndio tuseme nani anashinda.Prediction zako ni za kishabiki sana.Lissu awezi kushinda uchaguzi huu.
 
Ndugu Kiboko,tusubiri kura zipigwe ,ndio tuseme nani anashinda.Prediction zako ni za kishabiki sana.Lissu awezi kushinda uchaguzi huu.
Umesema nn.....Na wewe nafanya nn
 
Ndani ya miaka mitano ametengeneza maadui wengi kuliko marafiki. Baadhi ya maadui ambao hawatampa kura ni hawa hapa

1 Watumishi wote ambao hawajapanda madaraja yao ...
2. Wahanga wote wa vyeti feki..
3. Wahanga wote wa kuvunjiwa nyumba na Matetemeko ya ardhi..
4. Watumishi wote aliowatumbua hadharani
5. Familia za wote waliopotea ama kutekwa....
6. Wana CCM wote walioshinda kura za maoni ila lakini majina yao kukatwa
7. Wafanyabiasha wote waliofirisiwa na mamlaka ya kikodi
8. Wafia chama wote ambao huhangaikia ushindi wa chama lakini kwenye teuzi zii.
 
Samahani mkuu,
Wewe ndo katibu mkuu Chadema?

Kama ni wewe, unalipwa posho za bule kabisa, yaani unasema anayeshindwa vibaya kuliko chaguzi zote ndiye unayesema atashinda ili Tu uendelee kulinda ugali siyo?

Bora ungeombaga tu ubunge kilaza wewe!!
 
Hili tumekua tukilisema sana humu mara nyingi.

Sababu kubwa Rais Magufuli kushindwa na Wapinzani tena kwa kura nyingi sana ni Ugumu wa maisha aliousababisha yeye na serikali yake. Watu wote nchi nzima wanalia na maisha magumu mzee hasikii kabisa...
Ni ushauri mzuri sana, tatizo muhusika na wapambe wake watakuelewa??
 
Nasubiri ifike wakati huo msikimbie hili jukwaa jamani!
 
Kumpa kura yako tena ni kubariki muendelezo wa mateso tuliyopitia ktk miaka hii mitano, BIG NO.
Miaka mitano ya maisha ya kishetani kwa:
√ Wanasiasa uchwara;
√ Wanasiasa wenye uchu wa madaraka;
√ Mangimeza;
√ Wapiga dili;
√ Misheni Tauni;
√ Mafisadi;
√ Watumishi wenye vyeti feki; nk.

Miaka mitano itajayo ni KUFYEKELEA MBALI masalia yao.
 
Ndani ya miaka mitano ametengeneza maadui wengi kuliko marafiki. Baadhi ya maadui ambao hawatampa kura ni hawa hapa

1 Watumishi wote ambao hawajapanda madaraja yao ...
2. Wahanga wote wa vyeti feki..
3. Wahanga wote wa kuvunjiwa nyumba na Matetemeko ya ardhi..
4. Watumishi wote aliowatumbua hadharani
5. Familia za wote waliopotea ama kutekwa....
6. Wana CCM wote walioshinda kura za maoni ila lakini majina yao kukatwa
7. Wafanyabiasha wote waliofirisiwa na mamlaka ya kikodi
8. Wafia chama wote ambao huhangaikia ushindi wa chama lakini kwenye teuzi zii.
#Machinga & mama ntilie
#wahitimu wa vyuo waliokosa ajira
 
Ndugu Kiboko,tusubiri kura zipigwe ,ndio tuseme nani anashinda.Prediction zako ni za kishabiki sana.Lissu awezi kushinda uchaguzi huu.
Umerudia kosa unalolipinga, kweli wewe mwana CCM wa kweli.
 
Back
Top Bottom