Sababu ipi hupelekea wanandoa mke na mme kufungua account ya pamoja?

Zamaulid

JF-Expert Member
May 25, 2009
18,663
13,488
Naomba mnieleweshe...hivi ni sababu ipi hupelekea wana ndoa...mke na mme kufungua account ya pamoja...
1. Kutokuaminiana katika matumizi ya fedha
2. Mahaba yaliyopitiliza... Au kuna sababu ipi nyingine?

Je ni jambo jema kufungua account ya pamoja?
 
Naona si jema
Naona ni vyema kukubaliana namna ya matumizi na
Ni vyema kuandika wosia
 
Kwani haya mambo bado yapo siku hizi...?
Yapo mkuu,nilikuwa bank fulani tena hapa jijini....Dar. jamaa kaja anataka kulipa ada kutoa joint account ya familia...akakataliwa hadi mkewe awepo...hapo jamaa tumesimama naye kwenye foleni kwa masaa kadhaa...akaondoka kinyonge kumfuata mkewe
 
Kwanini unaona sio jema?Kuna hatari gani?
Pesa bana inaonyesha tabia za ajabu za watu vibaya mnoo

Mwanaume asimamie majukumu ya kuhudumia familia
Mke afanye mengine
Joint account vipii

Bora muwe na malengo ya pamoja mchanganye hela mwisho wa mwaka mf kwenda vacay ama kumalizia ujenzi ama kulipia ada etc
 
Pesa bana inaonyesha tabia za ajabu za watu vibaya mnoo

Mwanaume asimamie majukumu ya kuhudumia familia
Mke afanye mengine
Joint account vipii

Bora muwe na malengo ya pamoja mchanganye hela mwisho wa mwaka mf kwenda vacancy ama kumalizia ujenzi ama kulipia ada etc
Joint account haimfanyi mwanaume asisimamie majukumu ya familia.

Issue hapa ni kwamba uaminifu umekosekana kwa kiwango kikubwa sana siku hizi.Magari, viwanja, hati n.k vingi havina majina ya Mr&Mrs bali jina moja kwa kuhofia kutapeliana n.k.

Ila kwa jamii ya sasa hasara/hatari ni kubwa kuliko faida.
 
Naomba mnieleweshe...hivi ni sababu ipi hupelekea wana ndoa...mke na mme kufungua account ya pamoja...
1. Kutokuaminiana katika matumizi ya fedha
2. Mahaba yaliyopitiliza... Au kuna sababu ipi nyingine?

Je ni jambo jema kufungua account ya pamoja?
Ni suala la maamuzi tu, kama watu wamefikia hatua ya kuwa mwili mmoja ambalo ni jambo kubwa zadi hilo la kufungua account moja mbona ni dogo tu.

Wakati wewe unahoji kuhusu wanandoa kumiliki kiji account chao, wapo wanandoa wanawaza kumilki benki yao km mradi na hivi sasa wana microfinance yao.

Wakati wewe unahoji hilo labda na kuona nongwa, wapo wanandoa wamewekeza ktk mradi wa pamoja kama wabia, tena una thamani kubwa tu, sasa kwanini wasifungue account ya pamoja kwaajili ya mradi wao?
 
Joint account haimfanyi mwanaume asisimamie majukumu ya familia.

Issue hapa ni kwamba uaminifu umekosekana kwa kiwango kikubwa sana siku hizi.Magari, viwanja, hati n.k vingi havina majina ya Mr&Mrs bali jina moja kwa kuhofia kutapeliana n.k.

Ila kwa jamii ya sasa hasara/hatari ni kubwa kuliko faida.
Ni kweli kabisa Mkuu
 
Ni suala la maamuzi tu, kama watu wamefikia hatua ya kuwa mwili mmoja ambalo ni jambo kubwa zadi hilo la kufungua account moja mbona ni dogo tu.

Wakati wewe unahoji kuhusu wanandoa kumiliki kiji account chao, wapo wanandoa wanawaza kumilki benki yao km mradi na hivi sasa wana microfinance yao.

Wakati wewe unahoji hilo labda na kuona nongwa, wapo wanandoa wamewekeza ktk mradi wa pamoja kama wabia, tena una thamani kubwa tu, sasa kwanini wasifungue account ya pamoja kwaajili ya mradi wao?
Ni kweli mkuu.

Issue hapa ni kwamba wanandoa wengi sio mwili mmoja.Jamii imebadilika sana.Ndoa zimekosa thamani/maana.Ndoa imekua fasheni, watu wanaoana ilimradi tuu.
 
Back
Top Bottom