Habari JF,
Ukiaachana na nguvu kubwa inatumika kuonesha umma kwa Hayati Magufuli hakufanya kitu huku vitu vinaonekana na tuhuma nzito ambazo hazina ushahidi bado haiwezi ondoa ukweli kwamba hawa viongozi wawili watabaki kuwa bora kuwahi kutokea nchini mwetu.
Kwa kifupi bado tunawahitaji lakini Je, ni rahisi kuwapata ? Jibu hapana na zifuatazo ni sababu kwanini ni Ngumu kuwapata -
1. Demokrasia: Ni mfumo wa kuangalia mawazo ya wengi na kupuuza wachache huu mfumo hautufai Afrika kabisa sababu unatupa viongozi wasiofaa. Pili unapuuza mawazo ya wachache ambayo muda mwingine ni msingi mwisho ni chanzo kikubwa cha migogoro na vita lakini kikubwa zaidi maamuzi mengi sana huwa yanachukua muda mrefu sana sababu inahitajika vikao vingi vya makubaliano. Hivyo AFRIKA INAHITAJI DEMOKSIA INAYOENDANA NA TAMADUNI NA MAZINGIRA YETU.
2. Nguvu ya Mataifa ya nje: Umewahi jiuliza hivi wazungu au mataifa ya nje wanatupenda sana Africa au ni watu wema sana kiasi cha kuacha kusaidia wananchi wao na kutoa misaada na mikopo? La hasha wanafanya hivyo kwa maslahi yao hivyo ni lazima waweke mkono kuhakikisha mtu anapatikina analinda maslahi yao.
3. Ujinga bado mwingi sana: Ujinga ni adui mkubwa sana. Tanzania unaweza fanyika ufisadi mkubwa sana lakini watu wakawa kimya wanaendelea na maisha lakini ukizima data au ukaifungia whatsapp au Twitter basi utawanyima raha sana. Kwa kifupi ni bora uwape uhuru wa kutukanana mitandaoni kuliko maendeleo, sasa watu kama hawa ni ngumu sana kukupa kiongozi bora hasa kwa njia ya demokrasia.
Hivyo tupambane na ujinga.
Je, unadhani kuna siku tutapata watu wazalendo na watakao pigana kwa ajili ya maslahi ya Taifa letu? au tayari tunao tuendelee kuwaamini?