Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 7,235
- 12,748
Mara nyingi wanajeshi husema kuwa wanapindua nchi sababu ya uongozi mbaya, kwa ajili ya wananchi blah blah. Ukweli hizo si sababu kabisa zinazofanya wafanye hivyo.
Mara nyingi wanajeshi hupindua nchi baada ya kuona mtawala hana maslahi tena kwao au hawezi kuendelea kulinda maslahi yao. Mfano, kama kiongozi ni mgonjwa sana, kuna uwezekano mkubwa wa kupinduliwa. Sababu wanajeshi wanakuwa na mashaka na mustakabali wao.
Hili lilifanyika sana kwa masultani wa Milki ya Ottoman. Unakuta Sultani ana watoto wengi kwa mama mbalimbali. Siku akishikwa na ugonjwa na watu/watoto wakawa hawana uhakika na future yao, huwahi kumpindua mapema ili kuwawahi watoto wengine kushika madaraka.
Mobutu alitawala miaka kibao lakini alikuja kugeukwa baadaye, inadaiwa kuwa alipatwa na ugonjwa wa kansa ya kibofu. Majenerali wake wakaona hapa nguzo inaenda kuanguka, ni kuchukua chako mapema.
Hata Bongo wa Gabon kuna uwezekano mkubwa kapinduliwa sababu ya afya yake mgogoro.
Sababu nyingine ni uzee. Watu wakishaona unakuwa mzee wanaanza kuulizana nani atarithi. Maneno hayo yanapamba moto na kusababisha watu kuwahi chao mapema. Ni kama kilichotokea kwa Mugabe.
Mapinduzi yote ni watu wanaangalia maslahi yao kwanza. Ndiyo maana ukipindua kitu cha kwanza ni kushika hazina ya nchi ili uweze kuwalipa machawa wako.
Kitu cha kwanza ambacho wa Ottoman walifanya baada ya kufanya mapinduzi ilikuwa ni kushika hazina. Ukishindwa kufanya hivyo unapinduliwa tena. Na ukipindua na kujidai kuleta utawala bora na kubana mafisadi, hao chawa wako watakupindua. Kama kilichomkuta Sankara.
Pamoja na yote hayo, utawala wa madikteta wa kijeshi ni bora kuliko wa kidemokrasia, sababu hasa ni kuwa kwenye demokrasia kuna chawa wengi sana wa kuwalisha.