Sababu 10 za kuikana (DISOWNED) Tume ya Katiba ya Warioba...

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Mwenyekiti wa Tume ya marekebisho ya katiba; Joseph Sinde Warioba, hivi karibuni amekuwa akitoa matamshi yanayoonyesha dhahiri kutunyanyapaa wananchi ambao tumekuwa mstari wa mbele kutoa maoni yetu kwenye tume tajwa!

Pamoja na kauli zake tata, Warioba amedai maoni yetu yamefanana kupindukia na ni kwa sababu tunayatoa maoni hayo kwa mashinikizo ya NGOs, vyama vya kisiasa na taasisi za kidini!
(La ajabu, hakuzitaja!)

Kauli hizi zinatia mashaka makubwa katika maeneo yafuatayo kwa tume tajwa kututendea haki:-

1) Tuhuma za Warioba dhidi yetu hajazipa ushahidi wowote hata basi kuwataja kwa majina taasisi husika ikiashiria kuwa haheshimu utawala bora ambao unamsukuma ahakikishe ya kuwa tuhuma zinaandamana na ushahidi ili ziweze kupatiwa majibu fasaha........na watuhumiwa.

2) Ni dhahiri kwa vile tunaishi nchi moja na kukabiliana na changa moto zinazofanana ni wazi maoni ya majibu ya kero zetu pia yatashabihiana.......................sasa sijui kwanini Warioba atushangae kwa hilo?

3) Tusisahau wajumbe wote wanaounda tume ni matunda ya mfumo mbovu tulionao wa kiutawala hivyo tunapowaona wameanza kupembua uhalali wa maoni yetu hata kabla ya wao kuikamilisha kazi ya kuyakusanya maoni tajwa wasiwasi wetu ni kuwa huenda kwenye mikoba yao wana katiba wanayoitaka kuishinikiza tuipigie kura ya maoni na ushirikishwaji wetu ni "danganya toto" tu!

4) Kitendo cha tume kuhoji uhalali wa maoni yetu lakini bado wanaendelea kuyakusanya ili kuhalalisha malipo makubwa ya posho wanazojilipa inatuthibitishia ya kuwa lengo siyo kuutafuta ukweli bali kuupotosha ukweli kwa malipo lukuki kwenye vibindo vyao!

5) Wajumbe wote hawana wasifu wa kuupigania na kuutetea mfumo wa utawala bora na hata kuhatarisha mkate wao. Wengi wao wamebandikwa huko kwa sababu ya kuutetea udhalimu na hivyo si rahisi siye kuwaamini kama watatutendea haki na kuwakilisha kile ambacho tumewaambia na baadhi ya mifano ya taswira zao ni kama ifuatavyo:-

i) Bw. Warioba kupanda kwake kwenye chati ya uongozi hapa nchini kwa kiasi kikubwa alinufaika na kivuno cha
"ukabila" wakati wa utawala wa Nyerere. Sidhani kama Raisi kama asingelikuwa anatoka Musoma angeliweza kuteua Mwanasheria Mkuu kwa kiwango cha duni cha uzoefu alichokuwa nacho Warioba wakati alipoteuliwa. Mwaka 1990, Mwinyi aliunda tume ya kumchunguza Warioba njia alizozitumia kuukwaa ubunge wa Bunda na tume ilithibitisha ya kuwa alitumia vibaya madaraka yake ya dhamana ya Uwaziri Mkuu na Makamu wa kwanza wa Uraisi na kushauri aenguliwe.

Aidha tume feki ya kuthibiti mianya ya ufisadi ambayo aliisimamia wakati wa Mkapa ilitutupia changa la machoni pale msisitizo wake ulipokuwa kuwakomoa baadhi ya watendaji serikalini badala ya kuona mfumo mzima wa kiutawala ulikuwa ni tatizo kubwa la uchocheaji wa ufisadi serikalini. Mapendekezo yake yalijaa visasi na akina Bw. Nalaila Kiula na wenzie baadaye walikuja kusafishwa na mahakama na hadi leo Warioba au serikali haijawahi kuwaomba msamaha waathirika hawa au hata kuwafidia!

Pengine baya kuliko yote Warioba amehusishwa moja kwa moja na ufisadi wa EPA na hadi leo hajarudisha hata sumuni au hata kufikishwa kwenye vyombo vya dola kuchunguzwa kama kweli njia alizozitumia kujichotea mabilioni BOT zilizingatia sheria zilizopo.

Katika wasifu wa Warioba kama ulivyo wasifu wa wajumbe karibuni wote wa tume ni kuwa nafasi zote walizowahi kuzishika za kiutendaji serikalini hawajawahi kuziomba au hata kushindana na mtu yoyote na hivyo kuwatarajia wapendekeze nafasi zote serikalini kupatikana kwenye mazingira ya uwazi na ushindani kuwa ni njozi za ajuza.

ii) Makamu wao wa tume, Jaji Mkuu mstaafu - Augustine Ramadhani- alijivika joho la kuishinikiza mahakama ya Rufaa ambayo alikuwa akiisimamia kuzuia mgombea binafsi akidai siyo kazi ya mahakama kuliingilia bunge wakati katiba kama ilivyo sheria nyingine mahakama ndicho chombo pekee iliyopewa mamlaka ya kuzitafsiri sheria zote zikiwemo za kikatiba kuona kama zinalinda utawala bora. Jaji Ramadhani kwa kasi ya mithili ya mwewe, aliteua tume ya majaji wenzie saba badala kuanzia majaji watatu ili kuzika haki yetu hiyo ya kimsingi kabisa. Hivi leo jaji Ramadhani kweli atakuwa kabadilika na huku yeye mwenyewe alikiri kuwa ule uamuzi aliutoa kwa mashinikizo ya kisiasa? Ni vigumu kwetu kumkubali kuwa anaweza kututendea haki pale ambapo Ikulu ileile ya JK iliyomteua kuwa jaji Mkuu kwenye mazingira yasiyoeleweka na aliiogopa kwenye suala la mgombea binafsi leo ageuka kuwa ngangari! Labda atueleze ile khofu aliyokuwa nayo kama jaji Mkuu sasa imezimwa na na nini...........................???????

iii) Dr. Senkondo Mvungi ni kinara wa kuzuia utawala bora ndani ya NCCR Mageuzi na mfano ni pale aliposhangilia kufukuzwa uanachama kwa mbunge wao wa Kigoma kwa kosa la kuwania kugombea nafasi ya uenyekiti wa chama chao. Hivi kama kugombea nafasi ambayo ni haki ya kikatiba ni nongwa je inapokuja masuala ambayo watawala hawayataki kwa sababu yanahatarisha mkate wao huyu ni mwakilishi wa kutumainiwa au ni sehemu ya uwakilishi haramu?

iv) Uwakilishi wa cdm pia una sura kama hiyo ambapo madiwani wanatimuliwa na hivyo kudhoofisha maana halisi ya
"people's power" ambayo wamekuwa wakituzuga nayo.................................kama walaji wawili, watatu kule Dar-CDM ambao hawakushiriki kwenye chaguzi za kuchagua madiwani wana nguvu ya kufutilia mbali "people's power" ya wapigakura kweli unawategema watusaidie katiba ambayo italinda misingi ya utu ndani ya katiba tarajiwa kama siyo ubabaishaji mtupu?

v) Wajumbe wote wa tume hawana wasifu wa kutetea utawala bora zaidi ya kutetea mkate wao unapokuwa hatarani kuangukiwa na vumbi tu............

6) Kwa vile wajumbe wa tume hawajajitokeza hadharani na kumpinga Warioba na kauli zake za kubeza demokrasia na ambazo zimo nje ya hadidu za rejea alizopewa ni sahihi kwetu kuchukulia tume nzima iliukubali msimamo tajwa na hivyo haina uhalali tena wa kuendelea na ukusanyaji wa maoni tajwa bali kufungasha virago na kurudia kazi zao zenye kipato cha mwendo wa kinyonga..............

7) Tume wakati ikijitungia hadidu ya rejea ya kutupasha madhaifu yetu kazi ambayo siyo yao, wamesahahu kujipanga na kuja na mkakati wa jinsi gani sheria mpya ziundwe kabla ya uchaguzi wa 2015 ambazo bila ya sheria hizo katiba mpya hata iwe imeboreshwa vipi kamwe hatutaweza kuitekeleza. Wao wamejipanga kumaliza zoezi hili mwaka mmoja kabla ya uchaguzi mkuu wakati sheria nyingi za kuuongoza uchaguzi huo zinadai miaka angalau 3 kama uzoefu wa majirani zetu wa kenya unatoa busara zozote hapa..................

8) Kutojenga njia pana na kuwagharimia taasisi huria katika kuhakiki jinsi tume inavyofanya kazi ni dhahiri tume utendaji wake haiwajibiki kwa yeyote yule jambo ambalo linatia dosari zoezi zima. Tulipaswa tuwe na vyombo vingi huria ambavyo navyo vitahakiki utendaji wa kazi wa tume badala ya sisi kusubiria ghiliba za tambo za Warioba kama sehemu ya hakiki tajwa........................

9) Sheria inayoanzisha tume tajwa haijaipa tume mamlaka ya kuyawakilisha maoni ya wananchi kwa bunge badala yake wanayapeleka kwa Raisi ambaye ana kila shauku ya kuchakachua maoni tajwa. Kumbuka JK ni sehemu ya serikali ya Mkapa ambayo ilikuja na "white paper" ambayo ni misimamo ya serikali ya katiba ya watawala na waliipitisha kwa mabavu nyakati hizo. Hivi leo unapoona JK anapokataa kulimilikisha bunge zoezi hilo na kulichakachua kwa kulichanganya na la wakilishi visiwani wakati kuna Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na marekebisho haya yanafanyika nje ya katiba yetu...........................sasa tutarajie nini?..........mimi naendelea kushangaa tunaruhusu watu wale pesa zetu kwa utapeli wa kutuandikia katiba mpya kwa mfumo wa utaratibu ambao hautambuliki ndani ya katiba ya jamhuri ya Muungano wa Tanzania ila sheria inatumika kutengua mantiki zote zilizomo ndani ya katiba!!!!!!!!!!........Uandikaji wa katiba mpya lazima unahitaji marekebisho ya kikatiba ili zoezi hilo liweze kuwa na meno ya kisheriana wala siyo vinginevyo.

10) Uteuzi wa tume haukuwa wazi, shirikishi na wenye ushindani lakini bado tunaitegemea tume ije na mapendekezo ambayo ni shirikishi, wazi na yenye ushindani katika kutupatia watendaji serikalini. Hii ni sawasawa kabisa na kumwomba chui mwenye njaa kali akulindie sungura...........
 
Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
35,874
37,116
Warioba alitakiwa apumzike ale penshen yake,
akili imeshachoka hata mwili pia umechoka.

Kwani vijana mnasoma ili mfanye kazi gani kama nchi yetu
inazidi kuwakumbatia wazee ambao hawataki kuchanganya akili zao na za wengine.

Kwa katiba wengine hatujui hata hayo maoni unayasemea wapi, huwa tunasikia tu kwenye vyombo vya habari mwisho.
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Warioba alitakiwa apumzike ale penshen yake,
akili imeshachoka hata mwili pia umechoka.

Kwani vijana mnasoma ili mfanye kazi gani kama nchi yetu
inazidi kuwakumbatia wazee ambao hawataki kuchanganya akili zao na za wengine.

Mamndenyi La ajabu Warioba amekuwa akitamba kuwa hakuna tume iliyofanyakazi kama yao ya kuwafikia wananchi....wengi mithili wa sisimizi....tatizo anapiwa na nani? Anajipima mwenyewe............na si tunajua mwamba ngoma huvutia kwake?

Kwa katiba wengine hatujui hata hayo maoni unayasemea wapi, huwa tunasikia tu kwenye vyombo vya habari mwisho.
 
Last edited by a moderator:

Bobuk

JF-Expert Member
Oct 8, 2010
5,870
3,262
M/Kiti tume Judge Warioba ni MUUMINI WA SERIKALI MBILI hivyo hawezi kutenda haki kwenye suala la MUUNDO WA MUUNGANO.

Makamu/kiti Jugde Augustine Ramadhani ni MUUMINI wa wagombea wa nafasi za kisiasa eg udiwani, ubunge na Rais LAZIMA watokane na vyama vya SIASA, hivyo hawezi kutenda haki kwenye suala la MGOMBEA BINAFSI
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
M/Kiti tume Judge Warioba ni MUUMINI WA SERIKALI MBILI hivyo hawezi kutenda haki kwenye suala la MUUNDO WA MUUNGANO.

Makamu/kiti Jugde Augustine Ramadhani ni MUUMINI wa wagombea wa nafasi za kisiasa eg udiwani, ubunge na Rais LAZIMA watokane na vyama vya SIASA, hivyo hawezi kutenda haki kwenye suala la MGOMBEA BINAFSI

Bobuk Kwa mazingira haya, si wanatupotezea muda na mipesa bureeeeeeeeeeee
 
Last edited by a moderator:

Mamndenyi

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
35,874
37,116
Rutashubanyuma hivi huko vijijini itakuwaje kama hata town centre imekuwa hivyo,
kweli suala la katiba tz ni issue,

Mamndenyi La ajabu Warioba amekuwa akitamba kuwa hakuna tume iliyofanyakazi kama yao ya kuwafikia wananchi....wengi mithili wa sisimizi....tatizo anapiwa na nani? Anajipima mwenyewe............na si tunajua mwamba ngoma huvutia kwake?

Kwa katiba wengine hatujui hata hayo maoni unayasemea wapi, huwa tunasikia tu kwenye vyombo vya habari mwisho.
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Rutashubanyuma hivi huko vijijini itakuwaje kama hata town centre imekuwa hivyo,
kweli suala la katiba tz ni issue,

Vijijini waandike maumivu makali sana..................maana hakuna hata mjumbe mmoja anayeishi vijijini aliomo kwenye hiyo tume...................sasa wategemee nini?
 
Mr Rocky

JF-Expert Member
Oct 10, 2007
15,181
14,319
Mkuu Rutashubanyuma yaani tume ishachoka hata kabla haijaanza kazi yake maana inajipa mpaka majukumu ya kusema ni nani na nani wanaruhusiwa kutoa maoni na nani haruhusiwi
Kutupa katiba mpya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi na sheria nyingine zote zikabakia kama zilivyo ni kama umeweka mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani maana bado tutakuw ana tume ile ile ya uchaguzi na sheria zile zile za uchaguzi ambapo kama walikuwa na nia kweli tungepata katiba na wakajipa muda wa kubadilisha sheria nyingine zote ambazo mpaka sasa zinalalamikiwa
 
Last edited by a moderator:

Dingswayo

JF-Expert Member
May 26, 2009
4,019
2,911
Ungetuwekea wengine maneno yake halisi ambayo aliyatamka ili tuweze kuyachambua na kulinganisha na hoja zako na kuweza kufikia uamuzi.
 
Mvaa Tai

JF-Expert Member
Aug 11, 2009
6,161
4,434
Imeniuma sana wasiojua wanaweza wakayachukulia kirahisi rahisi matamshi ya Warioba, kwa ufupi warioba ameamua kututukana Watanzania kwamba hatuwezi kutoa maoni mpaka tuambiwe na NGOs, Wanasiasa, misikiti au makanisa. Nijuavyo mimi ni kwamba Warioba amekasirika kwani maoni yanayotolewa na Watanzania hayafanani kabisa na katiba wanayoitaka waliomteua kufanya hiyo kazi
 
Alakara Armamasitai

JF-Expert Member
Feb 4, 2011
481
132
mimi nasikia watu wanasema kuwa usijisfu mwenyewe kaa usifiwe sasa warioba yeye na tume yake ndio wanakusanya maoni kwanini sasa ajitokeze yeye mwenyewe na kujipima kuwa wamewafikia watu wengi angesubiri watu ndio wapime kuwa wamefanya kazi nzuri sio kukurupuka na kuanza kujipongeza kuwa eti amewafikia watu wengi zaidi pia tukumbuke rais ndiye aliyeunda tume kama ulivyosema kwa hiyo inaweza wao wanayokatiba ambayo wakubwa wanahitaji sasa wanachokifanya ni kutuzuga na kujilipa maposho kibao sisizokuwa na msingi.
 
ndetichia

JF-Expert Member
Mar 18, 2011
27,774
6,527
huyu mzee anataka kulazimisha kila kitu anachofikiria yeye upande wake kuwa ni sawa basi kila mtu afuate ndio anaona sawa..

R I P tanzania sijui lini tutakutana..:A S angry:
 
Haika

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,338
539
he wewe Kaka Rutashubanyuma, mbona unazidi kutukatisha tamaa??
Wenzio hapa tunalazimishia kuwa na imani ya hii tume!!!

Please let the little trust and hope we have on the tume, keep us going.
Ila kiukweli mimi sioni ni jinsi gani tutapata katiba ambayo inapendwa na wengi yani majority.

Tutapigia kura options kwa vipengele vya katiba au katiba nzima kama Kenya? manake?
 
Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Mkuu Rutashubanyuma yaani tume ishachoka hata kabla haijaanza kazi yake maana inajipa mpaka majukumu ya kusema ni nani na nani wanaruhusiwa kutoa maoni na nani haruhusiwi
Kutupa katiba mpya mwaka mmoja kabla ya uchaguzi na sheria nyingine zote zikabakia kama zilivyo ni kama umeweka mvinyo mpya kwenye chupa ya zamani maana bado tutakuw ana tume ile ile ya uchaguzi na sheria zile zile za uchaguzi ambapo kama walikuwa na nia kweli tungepata katiba na wakajipa muda wa kubadilisha sheria nyingine zote ambazo mpaka sasa zinalalamikiwa

Mr Rocky naona lengo ni kwenda uchaguzi wa 2015 na kivuli cha katiba mpya lakini sheria za mambo ya kale........
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
he wewe Kaka Rutashubanyuma, mbona unazidi kutukatisha tamaa??
Wenzio hapa tunalazimishia kuwa na imani ya hii tume!!!

Please let the little trust and hope we have on the tume, keep us going.
Ila kiukweli mimi sioni ni jinsi gani tutapata katiba ambayo inapendwa na wengi yani majority.

Tutapigia kura options kwa vipengele vya katiba au katiba nzima kama Kenya? manake?

Haika kura ya maoni ni ya ndiyo au hapana hakuna kuinyambulisha......unasema ndiyo unachokitaka na usichokitaka.......tuma kama ni bomu lazima tukiri kwanza ili itakapotukwaza tuweze kujua kulikoni..........
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Ungetuwekea wengine maneno yake halisi ambayo aliyatamka ili tuweze kuyachambua na kulinganisha na hoja zako na kuweza kufikia uamuzi.

Dingswayo kuna uhaja wa kufika mbali huko? Waswahili husema samaki mmoja akioza wote wamefanya nini?
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
huyu mzee anataka kulazimisha kila kitu anachofikiria yeye upande wake kuwa ni sawa basi kila mtu afuate ndio anaona sawa..

R I P tanzania sijui lini tutakutana..
A%20S%20angry.gif

ndetichia who said life was easier?
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
mimi nasikia watu wanasema kuwa usijisfu mwenyewe kaa usifiwe sasa warioba yeye na tume yake ndio wanakusanya maoni kwanini sasa ajitokeze yeye mwenyewe na kujipima kuwa wamewafikia watu wengi angesubiri watu ndio wapime kuwa wamefanya kazi nzuri sio kukurupuka na kuanza kujipongeza kuwa eti amewafikia watu wengi zaidi pia tukumbuke rais ndiye aliyeunda tume kama ulivyosema kwa hiyo inaweza wao wanayokatiba ambayo wakubwa wanahitaji sasa wanachokifanya ni kutuzuga na kujilipa maposho kibao sisizokuwa na msingi.

LULUNGEN Uliloongea ni neno la Mwenyezi Mungu..........soma Proverbs 27:2 "Let another man praise you, and not your own mouth, a stranger, and not your own lips."
 
Last edited by a moderator:

Rutashubanyuma

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
217,027
728,455
Imeniuma sana wasiojua wanaweza wakayachukulia kirahisi rahisi matamshi ya Warioba, kwa ufupi warioba ameamua kututukana Watanzania kwamba hatuwezi kutoa maoni mpaka tuambiwe na NGOs, Wanasiasa, misikiti au makanisa. Nijuavyo mimi ni kwamba Warioba amekasirika kwani maoni yanayotolewa na Watanzania hayafanani kabisa na katiba wanayoitaka waliomteua kufanya hiyo kazi

Mvaa Tai unachosema ndicho sahihi kabisa. tangia tupate uhuru katiba yetu ni ya kuwanufaisha viongozi na ndiyo maana hupanga safu za watu wao kwenye tume ya katiba ili wayafyatue yale ambayo yatakidhi hulka zao za kutawala milele...............
 
Last edited by a moderator:

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

15 Reactions
Reply
Top Bottom