Saa inatakiwa kuvaliwa mkono gani?

Saa inatakiwa kuvaliwa mkono gani?

Binafsi huwa napenda kuvaa SAA, mkono Wa kulia. Najisikia kuwa huru.hata nikiwa naandika ili kujua muda inaniwia rahisi.

Nikivaa mkono Wa kushoto, sijisikii poa
 
Mkono wa kushoto...... Sijua why ila ni mkono wa kushoto
 
kwa sababu natumia sana mkono wa kulia hadi saa napendelea kuvaa mkono wa kulia ndo rahisi kwangu kuangalia muda
 
SAA inavaliwa KUSHOTO.,,na inatakiwa,ivaliwe juu ya MKONO,,itazame juu,, sio chini ya mkono
 
Inategemea na thamani ya Saa
Sie wa zile za Manzese na kariakoo za Buku tatu au mbili jero kama ya Kenyata tunavaa kushoto,maana hata ukikaa kwenye gari unamuachia kibaka mkono wa kuiba kisha kesho unatoa buku tatu unanunua nyingine.

Wale wenye ma Platinumz watch wao wanavaa kulia,we madini umeona wapi yakavaliwa kushoto mazeee
Safi
 
Tunavalia saa mkono wa kushoto (logic) kwa sababu kwanza iwe rahisi kuona mda wakati unaandika na pia mkono wa kushoto hauna movements nyingi kama mkono wa kulia. Hivyo kuifanya saa idumu miaka mingi and that's the fact
asante, big up
 
Haina kanuni ila mkono ambao sio active sana unavalishwa saa . Ukisema kanuni ni kushoto huwatendei mashoto haki
 
saa inavaliwa mkono wa tofauti na unaotumia kwa matumizi ya kila siku:ukiwa ni mashoto unavaa saa mkono wa kulia na zipo saa za kuvaliwa na watu wa mashoto ambazo hata "knob" ya kurekebisha majira inawekwa upande wa kushoto tofauti na saa nyingi tunazovaa watu wa tunaotumia mkono wa kulia na kuvaa saa upande wa kushoto ambapo "knob" ya kurekebisha majira ipo upande wa kulia wa saa.
Kama unauwezo wa kutumia mikono yote unaweza vaa mkono wowote tu kama afanyavyo obama
 
Navaaga mkono ninaojisikia kwa wakati huo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom