Mikono yako katika roho

Mikono yako katika roho

a sinner saved by Christ

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2017
Posts
2,457
Reaction score
2,658
MIKONO YAKO .
Mit 3:16 SUV

Ana wingi wa siku katika mkono wake wa kuume, Utajiri na heshima katika mkono wake wa kushoto.

Mkono wa kulia-Umebeba wingi wa siku zako za kuishi.

Mkono wa kushoto-umebeba mafanikio yako

UKIOTA NDOTO
umeumia mkono wa kulia ,labda umekatika mkono,au mnyama amekuuma mkono wa kulia umeumia unavuja damu...maana yake washirikina mawakala wa nguvu za giza wanataka wakumalize kabisa ufe.,wachukue uhai wako.

mkono wa kushoto ..wanalenga kushambulia mafanikio yako heshima utajiri.

Ukiona KIGANJA cha mkono wa kushoto unakuwasha kusiko kwa kawaida ghafla tu bila ugonjwa bila sababu zinazotokana na ugonjwa.

Maana yake --Hiyo ni alama ya kufuatilia uchumi wako,mafanikio yako...wengi huwa wanafikiri kiganja cha mkono wa kushoto kikiwasha watapokea PESA ,ila ni kwamba hiyo alama ya kufuatilia mafanikio yako kiroho ina maanisha KUZUIA mafanikio yako,kuzuia usipate fursa,na hata ukipata pesa zitumike hovyo ziishe
unakuta kiganja kinawasha hata siku tatu mfululizo maana yake unapigwa vita ya upoteze uchumi wako,ugali wako,usipate fedha,usipate kazi,au hata ukipata fedha zipotee kwa haraka.

USIFURAHIE ukiona kiganja cha mkono wako kinawasha,ukafikiri inakaribia kupata pesa/mafanikio.

ni kinyume chake badala ya kupata/kupokea UNAKWENDA KUPOTEZA hata ukizipata zitapotea kama moshi upesi kwenye matatizo au zitazuiliwa zisikufie.

Maana ya pili ya ishara ya kuwashwa kiganja cha mkono wa kushoto,ni kuashiria mizimu ya ukoo wenu nayo maagano na nguvu za giza inataka utolee sadaka,unakuta mababu zako waliweka maagano na madhabahu za mizimu,waganga wa kienyeji,kuhusu uchumi/fedha saaa inadai mgao uwagawie pesa kidogo...hivyo zitapotea zitaisha kama upepo.

ukipata pesa matatizo ya matumizi yatatokea mpaka hiyo hela yote itumike iishe.

maana nyingine ya kuwashwa kiganja cha mkono ni kukuibia baraka zako za fedha kuzihamisha kwa mtu mwingine kwa kutumia nguvu za giza,hapa viganja vya mikono yotr miwili vinaweza kuwasha cha kipokea(kushoto)na cha kutoa(kiganja cha mkono wa kulia).

KUTOFAUTISHA KUWASHA KIGANJA kwa kawaida na kinakosababishwa na mashambulizi ya nguvu za giza.
Kuna kosababisha na nguvu za giza kunakuwa kwa ghafla,halafu kunawasha sana na muda maalumu ule ule,na kunatokea pale ukikaribia kupata pesa au matatizo yanayoleta matumizi ya pesa yanapotokea

itakuletea hali ya wasiwasi na kukosa amani au nafsi kuwa uzito

muwasho unaendelea hata ukikuna hauishi tofauti na muwasho wa kukauka ngozi.

Kama matatizo ya kuongezeka matumizi ya pesa yanatokea baada ya kiganja kuwasha

HATUA YA KUCHUKUA
OMBA SALI Mungu BABA kama hukunkuwashwa kwa kiganja cha mkono kunatokana na maroho ya nguvu za giza zinazofuatilia uchumi wangu,nakukataa kwa jina la Yesu,nampinga shetani naye anikimbie,kila silaha yeyote itakayofanyika ,zifukuze ziondoke ziache kukufuatilia kwa jina la Yesu.

Vunja maagano yote ya ukoo,ya mizimu ,roho za ukoo zinazofuatilia maisha yako na uchumi wako,vunja hiyo mikataba ya mababu,wazee wa ukoo,waganga wa kienyeji,inayodai sadaka uchumi wako kwa jina la Yesu.

Nafunika baraka zangu za kiuchumi,fedha ,roho yangu,nafsi yangu,mwili,wangu ,kwa DAMU YA YESU.


Takasa mikono yako,viganja vyako mikono kwa kwa Damu ya Yesu.

KUMPA MKONO MTU.
kuna mtu ukimpa mkono ghafla una anza kukuwasha au kukuuma

au kuna nyumba ukiingia baadae viganja vya mikono vinaanza kukuwasha.

Kuna watu ukiwapa mkono tu unaanza kuumwa mkono.

Hosea 4:6
Watu wangu wanaangamizwa kwa kukosa maarifa
;
 
SWALI
Kaka naumia na hizo njozi za mapolice ni njozi inayojirudiarudia,
Police maana yake nini katika ulimwengu wa roho.

JIBU
Jeshi la mapolisi katika ndoto maana yake ni wachawi(washirikina,walozi,wanga)

bundiki na silaha zao ..ni makombora yao ya kichawi..

ukiota wamebeba bunduki bunduki au mabomu au mikuki ....ndio makombora yao kichawi...wanakurushia....mana yake wanakushambulia katika ulimwengu wa roho..
Zab 27:3
Jeshi lijapojipanga kupigana nami, Moyo wangu hautaogopa. Vita vijaponitokea, Hata hapo nitatumaini.
CHA KUFANYA SASA..

Sali omba Mungu ,tumia damu ya Yesu..silaha yetu na nguvu zetu ni jina la Yesu na damu ya Yesu,na jeshi la malaika

ufunuo 12:11
Nao wakamshinda kwa damu ya Mwana-kondoo

isaya 54:17
zaburi 91:10-15
zaburi 35.
zaburi 18 na zaburi 19

jeshi la malaika walioko upande wetu ni wengi kuliko hao
wao watataja farasi ,wao watataja farasi lakini sisi tunakuja kwa kulitaja jina la Yesu.

Isa 41:10-13
usiogope, kwa maana mimi ni pamoja nawe; usifadhaike, kwa maana mimi ni Mungu wako; nitakutia nguvu, naam, nitakusaidia, naam, nitakushika kwa mkono wa kuume wa haki yangu.

USIOGOPE KABISA.
2 Kor 10:4
maana silaha za vita vyetu si za mwili, bali zina uwezo katika Mungu hata kuangusha ngome;

Usiogope kabisa ukiogopa tu unakosea unawafungulia mlango,vaa silaha za imani,tumia upanga wa neno...neno la Mungu ni silaha ,upanga mkali sana...fuatilia masomo na mafundisho yote niliyokutumia...

wachawi wanatakiwa wakuogope wewe na sio wewe uwaogope wachawi... kwa sababu wewe unamtumainia YESU BWANA WA MAJESHI...mfalme wa utukufu mwenye nguvu na utukufu..wewe ni mshundi tayari kupitia Yesu,wewe ni mwana wa Mungu mfalme ,sasa unaogopaje mapepo na wachawi,badala wao ndio waungue na kukukimbia si utumie silaha unazo ..OMBA tumia damu ya Yesu,jina la Yesu,kemea,tumia NENO ambaye huyo neno ndio Yesu

Ebr 4:12
Maana Neno la Mungu li hai, tena lina nguvu, tena lina ukali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili, tena lachoma hata kuzigawanya nafsi na roho, na viungo na mafuta yaliyomo ndani yake; tena li jepesi kuyatambua mawazo na makusudi ya moyo.


OMBA wewe mwenyewe kwa mdomo wako na kwa moyo wako..muombe Yesu kwa imani kwa kumaanisha kwa ujasiri.

hauhutaji kuombewa wala kutumia mafuta ya upako,wala kwenda popote hapo hapo ulipo Yesu yupo upo naye yupo karibu yako anakuona anakujua na anakusikia,ila ni lazima UOMBE.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom