Rwanda yamkataa Balozi wa Tanzania

Rwanda yamkataa Balozi wa Tanzania

nadhani jambo la muhimu ni serikali kufunga tu ubalozi wetu hapo Kigali....
 
Rwanda imemkataa Balozi mteule wa Tanzania, Mussa Siwa, ambaye alitakia na serikali kwenda kufanya kazi kwenye ubalozi wa Tanzania nchini humo.Taarifa kutoka Rwanda na duru za ndani ya serikali ya Tanzania zimeeleza serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi huyo kwasababu mbalimbali zikiwemo za kiusalama.

Habari kutoka ndani ya Ikulu ya Rwanda zinaeleza kuwa serikali ya nchi hiyo imemkataa balozi Siwa, baada ya kumshuku kuwa ni jasusi. Siwa kabla ya kuteuliwa kushika wadhifa huo, alikuwa ofisa katika ubalozi wa Tanzania nchini Ujerumani.

Tazania kwa sasa haina balozi nchini Rwanda tangu Dr.Marwa Matiko amalize muda wake wa kufanya kazi hiyo. Nafasi hiya kwa sasa inakaimiwa na Francis Mwaipaja,ambaye kabla ya kupelekwa Rwanda alikuwa msaidizi wa katibu mkuu kiongozi, Ombeni Sefue.

Ofisa mmoja mwandamizi wa Ikulu ya Rwanda aliliambia MTANZANIA kuwa viongozi wa nchi hiyo wanachukuwa tahadhari dhidi ya wanadiplomasia wa Tanzania wanaofanya kazi nchini Rwanda , tangu nchi hizi mbili ziingie katika vita ya maneno mwaka jana.


‘’Viongozi hapa wamekuwa na hofu kubwa na Tanzania na kufanya wawe macho na watanzania wanaoishi hapa na hasa maofisa ubalozi na ndio maana wamemkataa balozi huyo mteule’’. Alisema mtoa taarifa wetu.

Wafuatiliaji wa maswala ya kidiplomasia wametafsiri kitendo hicho kuwa ni mwendelezo wa kutofautiana kati ya serikali za nchi hizi mbili.

Rwanda iliingia katika mgogoro na Tanzania baada ya kuchukizwa na ushauri uliotolewa na Raisi Jakaya Kikwete wa kuitaka serikali ya nchi hiyo kufanya mazungumzo na kundi la waasi la FDLR, ambalo limejichimbia ndani ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo.

Rais kikwete alitoa ushauri huo mbele ya katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Kin-Moon na Raisi wa Umoja wa Afrika, Nkosazana Dlamini-Zuma, wakati wa mkutano wa viongozi wa ukanda wa maziwa makuu ya afrika uliofanyika mjini Addis Abab, Ethiopia, Mei, mwaka jana.

Ushauri huo ulipokelewa vibaya na Rais Kagame na waziri wa mambo ya nchi za nje wa nchi hiyo, Louise, Mushikiwabo, ambao walitoa kauli za kumdhalilisha Rais Kikwete.


Mkataba wa Vienna

Hata hivyo, Rwanda ina uhuru wa kisheria wa kumkataa balozi mteule wa kigeni kama inaona hafai kwenda kuishi nchini humo. Kifungu cha nne cha mkataba wa kimataifa wa Vienna wa mwaka 1961 unaozungumzia masuala ya kidiplomasia baina ya mataifa,kinatoa uhuru wa nchi kumkubali balozi mteule wa kigeni. Mathalani Tanzania , mwaka jana ilimkataa balozi mteule wa Ujerumani, Margit Hellwig – Boette, ambaye alitakiwa kuja kuwa balozi hapa nchini mara baada ya kumaliza muda wake nchini Kenya.

Sefue asema hana taarifa

Akizungumzia suala hilo, Sefue alisema taarifa hizo hajazipata na kwamba wizara ya mambo ya nje ndiyo inayoweza kufahamu vizuri suala hilo. ‘’Mimi sifahamu chochote kwakweli, nadhani watu wa wizara ya mambo ya nje ndiyo wanajua process (taratibu) hizi ndiyo maana hata jina la huyo balozi aliyekataliwa silijui’’ alisema.

Wizara ya mambo ya nje washangaa

Nae mkuu wa kitengo cha mawasiliano cha wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa, Mkumbwa Ally, alishangaa na kuhoji kuwa hizo taarifa tumezipata wapi kwani ni habari za ndani.

‘’Hizo taarifa mmezipata wapi, ni taarifa za ndani, chanzo chako cha habari ni nani’’,alihoji ally. Hata hivyo, alipoombwa kuzungumzia swali la msingi alisema suala hilo lipo nje ya uwezo wa wizara yake kwani Rais Kikwete ndiye mwenye mamlaka ya kuteuwa na kutangaza jina la mteule huyo.

“Kiujumla sijapata taarifa za uhakika kuhusu suala hilo kwa sababu uteuzi wa balozi yeyote ni ‘process’ utaratibu’’ , hivyo hatuwezi kujua jina lake mpaka uteuzi wake ukamilike ndipo tutangaziwe na mwenye mamlaka hayo ni Rais, hivyo siwezi sema chochote ‘’
alisema.

MTANZANIA lilifanya jitihada za kumtafuta Siwa bila mafanikio kuzungumzia suala hilo.

Katika siku za hivi karibuni uhusiano baina ya Tanzania na Rwanda umeonekana kusuasua na hata viongozi wa nchi hizi mbili wamekuwa wakidaiwa kukwepana katika hafla mbalimbali zinazohusu nchi zao pamoja na zile za jumuiya ya Africa mashariki(EAC).

Wiki mbili zilizopita, Rais kagame alikacha kuhudhuria sherehe za maadhimisho ya miaka 50 ya muungano wa Tanganyika na zanzibar zilizofanyika jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na marais wote wanachama wa ( EAC).

Mbali na Kagame kutokuhudhuria maadhimisho hayo, pia aliukacha mkutano wa wakuu wa nchi za EAC uliofanyika jijini Arusha, lakini alikwenda nchini Kenyana kuhudhuria kikao cha viongozi wa nchi za Afrika Mashariki wanaounganishwa na mradi unaoitwa ‘ Northern Corridor Infrastructure Project’. Waziri Mkuu Pinda aliiwakilisha Tanzania katika mkutano huo.


Source: Gurudumu la Habari

Ha ha haaaaaa....hii afrika bhaana ila ajue kabla hujampiga adui yako mjue kwanza rafiki yake.
 
Zile siraha zote kwa sasa hakuna kiwanda hata kimoja kinacho unda, Uganda wana Ndege bora kabisa kutuzidi


uganda wana hii SU-30 kutoka Urusi,
duh hayo makombora mawili yaliyopo chini hapo yakitua si htari tupu
 
Halafu bado mnashauri kuharakishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki inayojumuisha Rwanda. Ningekuwa Rais wa TZ ningefunga ubalozi wa TZ kule Rwanda.
ili iweje sasa!! Siasa haiko ivo wewe!! we lini umeona Marekani wakifunga ubalozi wao Russia pamoja na kwamba mara nyingi huzozana juu a mambo mbalimbali? tumia akili basi.
 
Tanzania tuna mashushushu wengi. Si ateuliwe mwengine tu kimyakimya aende akalinde maslahi yetu?
 
nadhani jambo la muhimu ni serikali kufunga tu ubalozi wetu hapo Kigali....
hapana mkuu, tulikubali ni la kawaida, ni mwaka jana tu Tanzania imemkataa balozi wa Ujerumani aliye teuliwa kuja bongo ambaye awali alikuwa anafanya kazi kwenye ubalozi wa ujerumani nchini kenya, ingawa sababu za kumkataa hazikuwekwa wazi!.
 
nakumbuka kagame hakuwepo kwenye sherehe za muungano, alituma mwakilishi, naamini mwakilishi hakumpa boss wake mrejesho wa alichokiona pale uwanjani...i mean maonyesho ya silaha zetu

Vita Siyo Silaha tu Peke Yake na Uwezo Wa Mbinu, Mikakati na Mipango Pia. Iran Ina Jeshi Imara Sana Na Lenye Vifaa Kuu Kuu Vya Kijeshi Tena Kuliko Hata Vya Tanzania Lakini Kila Kukicha Anasumbuliwa Na Israel tena Yenye Ukubwa Kama Wilaya Nzima Ya Magu. Ningewaona Wa Maana Badala Ya Kupiga Mkwara Humu Mngeishambulia tu Rwanda Kisha Muone Kilichomtoa Nyoka Pangoni. Huna Jeshi Imara La Kupigana Na RPF na Nakupa Kazi Ya Kufanya Ujasusi Wa Kutosha Wa Kulihusu Jeshi La Rwanda na Uwezo Wake Kisha Utanielewa Nilichokimaanisha Hapa Na Narudia Tena Kwa Msisitizo Kuwa HUNA JESHI IMARA LA KUPAMBANA na Taifa La Rwanda na Usidanganyike Na Yale Maonyesho na Kila Lifanyikalo hapa Mwanamume PK Anajulishwa na Kwa Taarifa Yako tu Kuna Principle wa Chuo Chenu Nyeti hapa Tanzania Anampa PK Data Zote za Tz na Mwakani Mwezi wa 5 au wa 7 Anastaafu Rasmi na Anakwenda Kuishi Kigali Kwa Kazi Maalum Ambayo Tayari PK Ameshamwandalia Kwani PK Anamjua Tokea Kipindi Kile Cha Miaka Ya 80 Alipokuwa Anafanya Kazi Maalum ktk Idara Yenu Ya TISS Chini Ya Hayati Kifimbo na Alikuwa Anaishi ktk Nyumba Mbili Oysterbay Moja Ilikuwa Mtaa Wa MKADINI na Nyingine Karibia Na Kilima NYEGE. Nimeamua Kukutolea Uvivu Wewe na Wapuuzi Wenzako Wengine Mnaokurupuka Kushupalia Kuzichapa Na PK........................NIMEMALIZA!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
 
A very poor judgement my brother! A spy who has raised to such a high position should not be a threat to the country. An ambassador, in this case, can't be feared just because his background has a connection with intelligence services. How many ministers and other high ranked officials have such connections being Tanzanians or Rwandese and are openly known by the systems of the two countries. Where on earth you can find an embassy which has no intelligence officers among its staff? This is a poor and uninformed intelligence entity which influenced such a decision. He is an ambassador not informer! Come on guys.
Yap this is because Kagame loves his Country unlike our president who doesn't give a fig about our country's security & safety.
 
Hivi mlitegemea nini kumpelekea Kagame jasusi?
Huyu anatujua mpaka mambo yetu ya ndani.

Swadakta Mkuu, Hebu Endelea Kuwaweka Sawa Wajinga Wajinga Humu Wasiojua Na Wanabaki tu Kukurupuka Na Kushadadia Huku Wakiwa Hakuna Wanachokijua Kuhusu Rwanda, RPF na Kamanda PK.
 
Tumefanikiwa kwa kiasi kikubwa kumvuruga huyu bwana kisaikolojia..mbaya zaidi hii issue ya muungano na yale mavifaru! niliwahi kusema humu..The guy is simply schizophrenic! kudos JK!

Cc: Bobuk huna haja ya kutamani kumtwanga wakati tumekwisha mtandika kiakili!!
Kitendo cha kujua kuwa Mtanzania huyu ni jasusi yule siyo, maana yake anajua mambo yetu nje ndani. Unafikiri tuko salama hapo? Mtikila alishasema Kagame kachomeka vijana elfu 30 serikalini mkampuuza, hayo ndo matokeo yake sasa.
 
Back
Top Bottom